Nchi ya Marekani imeunda sera mpya inayozuia Wafanyakazi wa Serikali, Wanafamilia, na Wakandarasi walio na vibali vya usalama kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi au kingono na Raia wa China . Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press.

Sera hiyo imewekwa na aliyekuwa Balozi wa Marekani, Nicholas Burns mnamo Januari, ikiwa ni uondoaji mkubwa kutoka kwa miongo ya awali, ambayo ilizuia uhusiano na Raia wa China wanaofanya kazi katika majukumu maalum, kama vile Walinzi wa ubalozi. Inaripotiwa kuwa uamuzi huo umechukuliwa kutokana na hofu kwamba Mawakala wa China wanaweza kuchukua taarifa za siri za Serikali ya Marekani na kuziwasilisha kwa Serikali ya China.

Sera hiyo inatumika kwa Wafanyakazi wa Marekani walioko China Bara, ikiwa ni pamoja na ubalozi wa Beijing na balozi ndogo huko Guangzhou, Shanghai, Shenyang na Wuhan, pamoja na ubalozi mdogo wa Marekani huko Hong Kong. Pia haitumiki kwa Wafanyakazi wa Marekani walioko nje ya China ambao wana uhusiano uliokuwepo hapo awali na Raia wa China ingawa wanaweza kutuma maombi ya misamaha, lakini wakikataliwa, lazima wasitishe uhusiano huo au waache nafasi zao.

Ikiwa sera hiyo itakiukwa, Wafanyakazi wanaohusika wataamriwa kuondoka China mara moja. Hata hivyo, Sera hiyo inaashiria mabadiliko makubwa katika mtazamo wa Serikali ya Marekani kuhusu usalama Nchini China, ikionyesha mvutano unaoongezeka kati ya Washington na Beijing kuhusu biashara, teknolojia na ushindani wa kijiografia na kisiasa.

Kwaupande wa Wizara ya mambo ya nje ya China imekataa kutoa maoni yake kuhusu sera hiyo, ikisema kwamba "ni sahihi zaidi kuuliza Marekani kuhusu swali hilo." imekadiriwa ikisema Wizara hiyo ya China.

Nchi ya Marekani πŸ‡ΊπŸ‡Έ imeunda sera mpya inayozuia Wafanyakazi wa Serikali, Wanafamilia, na Wakandarasi walio na vibali vya usalama kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi au kingono na Raia wa China πŸ‡¨πŸ‡³. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press. Sera hiyo imewekwa na aliyekuwa Balozi wa Marekani, Nicholas Burns mnamo Januari, ikiwa ni uondoaji mkubwa kutoka kwa miongo ya awali, ambayo ilizuia uhusiano na Raia wa China wanaofanya kazi katika majukumu maalum, kama vile Walinzi wa ubalozi. Inaripotiwa kuwa uamuzi huo umechukuliwa kutokana na hofu kwamba Mawakala wa China wanaweza kuchukua taarifa za siri za Serikali ya Marekani na kuziwasilisha kwa Serikali ya China. Sera hiyo inatumika kwa Wafanyakazi wa Marekani walioko China Bara, ikiwa ni pamoja na ubalozi wa Beijing na balozi ndogo huko Guangzhou, Shanghai, Shenyang na Wuhan, pamoja na ubalozi mdogo wa Marekani huko Hong Kong. Pia haitumiki kwa Wafanyakazi wa Marekani walioko nje ya China ambao wana uhusiano uliokuwepo hapo awali na Raia wa China ingawa wanaweza kutuma maombi ya misamaha, lakini wakikataliwa, lazima wasitishe uhusiano huo au waache nafasi zao. Ikiwa sera hiyo itakiukwa, Wafanyakazi wanaohusika wataamriwa kuondoka China mara moja. Hata hivyo, Sera hiyo inaashiria mabadiliko makubwa katika mtazamo wa Serikali ya Marekani kuhusu usalama Nchini China, ikionyesha mvutano unaoongezeka kati ya Washington na Beijing kuhusu biashara, teknolojia na ushindani wa kijiografia na kisiasa. Kwaupande wa Wizara ya mambo ya nje ya China imekataa kutoa maoni yake kuhusu sera hiyo, ikisema kwamba "ni sahihi zaidi kuuliza Marekani kuhusu swali hilo." imekadiriwa ikisema Wizara hiyo ya China.
0 Comments Β·0 Shares Β·27 Views