Mahakama ya Katiba ya Nchi ya Korea Kusini imemwondoa madarakani Rais wa Nchi hiyo, Yoon Suk Yeol aliyekuwa amefutwa kazi kwa kura ya kutokuwa na imani naye, leo imefika mwisho safari ya Urais wake. Uamuzi huo umefikiwa na mahakama leo Ijumaa Aprili 4, 2025, baada ya kutangaza kuwa Rais Yoon hapaswi kuendelea tena kuwepo katika Ikulu ya Taifa hilo na kutoa fursa ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine ili kumpa Rais mpya.

Rais Yoon ambaye ni Mwanasheria wa zamani wa Serikali, aliingia kwenye siasa mwaka mmoja tu kabla ya kushinda Urais mwaka 2022, amepitia misukosuko tangu alipotangaza kuiweka Korea Kusini chini ya Sheria ya Kijeshi (Martial Law) mwishoni mwa 2024. Katika uamuzi uliosomwa mubashara kwenye Televisheni, Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama hiyo, Moon Hyung-bae, amesema jopo la Majaji wanane (8) lilithibitisha kuondolewa kwa Yoon kwa sababu tangazo lake la sheria ya kijeshi lilikiuka katiba na sheria nyingine za Nchi hiyo kwa kiwango kikubwa.

Mahakama ya Katiba ya Nchi ya Korea Kusini 🇰🇷imemwondoa madarakani Rais wa Nchi hiyo, Yoon Suk Yeol aliyekuwa amefutwa kazi kwa kura ya kutokuwa na imani naye, leo imefika mwisho safari ya Urais wake. Uamuzi huo umefikiwa na mahakama leo Ijumaa Aprili 4, 2025, baada ya kutangaza kuwa Rais Yoon hapaswi kuendelea tena kuwepo katika Ikulu ya Taifa hilo na kutoa fursa ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine ili kumpa Rais mpya. Rais Yoon ambaye ni Mwanasheria wa zamani wa Serikali, aliingia kwenye siasa mwaka mmoja tu kabla ya kushinda Urais mwaka 2022, amepitia misukosuko tangu alipotangaza kuiweka Korea Kusini chini ya Sheria ya Kijeshi (Martial Law) mwishoni mwa 2024. Katika uamuzi uliosomwa mubashara kwenye Televisheni, Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama hiyo, Moon Hyung-bae, amesema jopo la Majaji wanane (8) lilithibitisha kuondolewa kwa Yoon kwa sababu tangazo lake la sheria ya kijeshi lilikiuka katiba na sheria nyingine za Nchi hiyo kwa kiwango kikubwa.
0 Comments ·0 Shares ·15 Views