Kutoka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , Mke wa Rais wa zamani wa Nchi hiyo Joseph Kabila Kabange, Olive Lembe Kabila, ametangaza kwamba Wanajeshi wa DR Congo waliopelekwa kwenye Shamba la Ng'ombe la Joseph Kabila lililopo Mkoani Haut-Katanga, waliiba, kuchinja na kula Ng'ombe wao waliowakuta katika Shamba hilo.

Olive Lembe amesema hayo kwamba Wanajeshi hao walikuwa kwenye Shamba la Kundelungu lililoko katika Mkoa wa Haut-Katanga na kwamba hawakuwa na ruhusa ya kuingia kwenye mali ya familia yao. Mbali na kuchukua kompyuta na simu za mkononi za Wafanyakazi wa shamba hilo, Mwanamama huyo alieleza pia kuwa Wanajeshi hao walikuwa wakichinja Ng'ombe wao kwa ajili ya kula kwa sababu hawakuwa na chakula walichobeba.

"Wanajeshi hawa walikuwa wakiiba kompyuta na simu za Wafanyakazi wa shamba. Walikuja bila chakula, sasa walichinja Ng'ombe wetu ili kula." alisema Lembe.

Ikumbukwe kwamba Serikali ya DR Congo ilitangaza kuchukua mali zote za Kabila (kustaafisha) baada ya ziara yake ya tarehe 18 Aprili katika Jiji la Goma linalodhibitiwa na Muungano wa AFC/M23. Serikali ilikuwa ilituma Wanajeshi wa upelelezi kwenye mali zake, ikiwemo Nyumba yake iliyo katika eneo la Limete Mjini Kinshasa, wakisema walikuwa wakitafuta vifaa vya kijeshi ambavyo vinaweza kuwa vimefichwa.

Lembe anasema kuwa Serikali ya DR Congo inaendelea kufanya mateso kwa familia yao, na kudai kwamba ina mpango wa kuwaangamiza.

Kutoka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, Mke wa Rais wa zamani wa Nchi hiyo Joseph Kabila Kabange, Olive Lembe Kabila, ametangaza kwamba Wanajeshi wa DR Congo waliopelekwa kwenye Shamba la Ng'ombe la Joseph Kabila lililopo Mkoani Haut-Katanga, waliiba, kuchinja na kula Ng'ombe wao waliowakuta katika Shamba hilo. Olive Lembe amesema hayo kwamba Wanajeshi hao walikuwa kwenye Shamba la Kundelungu lililoko katika Mkoa wa Haut-Katanga na kwamba hawakuwa na ruhusa ya kuingia kwenye mali ya familia yao. Mbali na kuchukua kompyuta na simu za mkononi za Wafanyakazi wa shamba hilo, Mwanamama huyo alieleza pia kuwa Wanajeshi hao walikuwa wakichinja Ng'ombe wao kwa ajili ya kula kwa sababu hawakuwa na chakula walichobeba. "Wanajeshi hawa walikuwa wakiiba kompyuta na simu za Wafanyakazi wa shamba. Walikuja bila chakula, sasa walichinja Ng'ombe wetu ili kula." alisema Lembe. Ikumbukwe kwamba Serikali ya DR Congo ilitangaza kuchukua mali zote za Kabila (kustaafisha) baada ya ziara yake ya tarehe 18 Aprili katika Jiji la Goma linalodhibitiwa na Muungano wa AFC/M23. Serikali ilikuwa ilituma Wanajeshi wa upelelezi kwenye mali zake, ikiwemo Nyumba yake iliyo katika eneo la Limete Mjini Kinshasa, wakisema walikuwa wakitafuta vifaa vya kijeshi ambavyo vinaweza kuwa vimefichwa. Lembe anasema kuwa Serikali ya DR Congo inaendelea kufanya mateso kwa familia yao, na kudai kwamba ina mpango wa kuwaangamiza.
Like
1
· 0 Kommentare ·0 Anteile ·41 Ansichten