KWANINI NCHI MASIKINI HUWA NA WANASIASA MATAJIRI SANA?

Hii ni moja ya mafumbo makubwa ya kisiasa Afrika:
Nchi ni masikini...
Raia hawana huduma...
Lakini wanasiasa wana nyumba za kifahari, magari ya kifahari, na watoto wao wanasoma nje ya nchi.

Unawezaje kuongoza nchi yenye njaa, lakini wewe unanenepa?

Sababu ya kwanza: Siasa ni Biashara.
Watu wengi wanaingia kwenye siasa si kwa sababu ya maono, bali kwa sababu wanajua kuna "return on investment".
Unatumia milioni 100 kugombea, lakini ukishinda, unaweza rudisha mara 10 zaidi kupitia dili.

Sababu ya pili: Rushwa Iliyohalalishwa.
Nchi nyingi masikini zina mifumo dhaifu ya ukaguzi.
Mwanasiasa anaweza toa tenda kwa kampuni yake mwenyewe kupitia proxies.
Hakuna accountability.
"Public office" inageuka kuwa ATM ya binafsi.

Sababu ya tatu: Ukosefu wa elimu ya uraia.
Raia wengi hawajui haki zao.
Wanapewa kilo ya unga au t-shirt wakati wa uchaguzi, wanapitisha mwizi mwingine.
Siasa zinageuka kuwa mashindano ya maigizo, si sera.

Sababu ya nne: Tabaka la kimasikini linaogopa mabadiliko.
Wengi wetu tunaishi kwa matumaini ya kusaidiwa binafsi na si kwa kutengeneza mfumo unaosaidia wote.
Tunapenda “mheshimiwa” badala ya mfumo bora.
Hili linafanya mafisadi waendelee kutawala.

Sababu ya tano: Woga wa taasisi.
Asasi za kiraia, vyombo vya habari na mahakama huwa dhaifu au vimetiwa mfukoni.
Hii inawapa wanasiasa uhuru wa kuiba bila hofu ya kushtakiwa.

Na mwisho kabisa:
Wanasiasa hawawajibiki kwa wananchi bali kwa wafadhili wao.
Wale waliowasaidia kugombea (wakubwa wa biashara, makampuni ya kigeni, n.k.) ndio wanaoamua sera.
Mwananchi? Yuko pembeni kabisa.

Hii ndiyo sababu utaona mtu anakuwa mbunge kwa miaka 15 lakini eneo lake halina maji wala barabara.
Lakini yeye ana ghorofa 3, magari 4, na clinic binafsi Nairobi.

Umasikini wa raia si bahati mbaya ni mpango wa kisiasa.

Suluhisho?

Elimu ya uraia

Uwajibikaji

Sheria kali za kupiga vita ufisadi

Vyombo huru vya habari

Raia wasioogopa kuuliza maswali

Je, wewe unaona nini kifanyike ili tuwajibishe viongozi wetu?
Tumezoea maisha magumu kiasi kwamba tumeyakubali kama kawaida.
Ni muda wa kubadilika.

#Kireportel #Ufisadi #Siasa #Africa #Kujitambua

Follow me pia X (Twitter): x.com/DullahWrites
KWANINI NCHI MASIKINI HUWA NA WANASIASA MATAJIRI SANA? Hii ni moja ya mafumbo makubwa ya kisiasa Afrika: Nchi ni masikini... Raia hawana huduma... Lakini wanasiasa wana nyumba za kifahari, magari ya kifahari, na watoto wao wanasoma nje ya nchi. Unawezaje kuongoza nchi yenye njaa, lakini wewe unanenepa? Sababu ya kwanza: Siasa ni Biashara. Watu wengi wanaingia kwenye siasa si kwa sababu ya maono, bali kwa sababu wanajua kuna "return on investment". Unatumia milioni 100 kugombea, lakini ukishinda, unaweza rudisha mara 10 zaidi kupitia dili. Sababu ya pili: Rushwa Iliyohalalishwa. Nchi nyingi masikini zina mifumo dhaifu ya ukaguzi. Mwanasiasa anaweza toa tenda kwa kampuni yake mwenyewe kupitia proxies. Hakuna accountability. "Public office" inageuka kuwa ATM ya binafsi. Sababu ya tatu: Ukosefu wa elimu ya uraia. Raia wengi hawajui haki zao. Wanapewa kilo ya unga au t-shirt wakati wa uchaguzi, wanapitisha mwizi mwingine. Siasa zinageuka kuwa mashindano ya maigizo, si sera. Sababu ya nne: Tabaka la kimasikini linaogopa mabadiliko. Wengi wetu tunaishi kwa matumaini ya kusaidiwa binafsi na si kwa kutengeneza mfumo unaosaidia wote. Tunapenda “mheshimiwa” badala ya mfumo bora. Hili linafanya mafisadi waendelee kutawala. Sababu ya tano: Woga wa taasisi. Asasi za kiraia, vyombo vya habari na mahakama huwa dhaifu au vimetiwa mfukoni. Hii inawapa wanasiasa uhuru wa kuiba bila hofu ya kushtakiwa. Na mwisho kabisa: Wanasiasa hawawajibiki kwa wananchi bali kwa wafadhili wao. Wale waliowasaidia kugombea (wakubwa wa biashara, makampuni ya kigeni, n.k.) ndio wanaoamua sera. Mwananchi? Yuko pembeni kabisa. Hii ndiyo sababu utaona mtu anakuwa mbunge kwa miaka 15 lakini eneo lake halina maji wala barabara. Lakini yeye ana ghorofa 3, magari 4, na clinic binafsi Nairobi. Umasikini wa raia si bahati mbaya ni mpango wa kisiasa. Suluhisho? Elimu ya uraia Uwajibikaji Sheria kali za kupiga vita ufisadi Vyombo huru vya habari Raia wasioogopa kuuliza maswali Je, wewe unaona nini kifanyike ili tuwajibishe viongozi wetu? Tumezoea maisha magumu kiasi kwamba tumeyakubali kama kawaida. Ni muda wa kubadilika. #Kireportel #Ufisadi #Siasa #Africa #Kujitambua Follow me pia X (Twitter): x.com/DullahWrites
0 Commentaires ·0 Parts ·88 Vue