Isak aanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Liverpool

Mshambuliaji wa Liverpool, Alexander Isak, ameanza rasmi mazoezi na kikosi cha Liverpool.

Mchezaji huyo wa Kiswidi alikamilisha usajili wa rekodi ya Uingereza wa £125 milioni kutoka Newcastle katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili, kisha akaungana na timu ya taifa ya Sweden kwa mechi za kimataifa za Septemba.

Isak alicheza dakika 18 tu katika mechi mbili ambazo Sweden haikushinda dhidi ya Slovenia na Kosovo, lakini sasa ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wapya wa klabu ya Liverpool.

Huenda Isak akacheza mechi yake ya kwanza kwa Liverpool dhidi ya Burnley siku ya jumapili hii.
đź‘€Isak aanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Liverpool 👉Mshambuliaji wa Liverpool, Alexander Isak, ameanza rasmi mazoezi na kikosi cha Liverpool. 👉Mchezaji huyo wa Kiswidi alikamilisha usajili wa rekodi ya Uingereza wa £125 milioni kutoka Newcastle katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili, kisha akaungana na timu ya taifa ya Sweden kwa mechi za kimataifa za Septemba. 👉Isak alicheza dakika 18 tu katika mechi mbili ambazo Sweden haikushinda dhidi ya Slovenia na Kosovo, lakini sasa ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wapya wa klabu ya Liverpool. 👉Huenda Isak akacheza mechi yake ya kwanza kwa Liverpool dhidi ya Burnley siku ya jumapili hii.
0 Comments ·0 Shares ·5 Views