Vurugu mitandaoni! Ned Nwoko amvaa Regina Daniels, asema "ameharibu familia yetu".
Mitandao ya kijamii imewaka moto kufuatia tuhuma nzito zilizotolewa na Bilionea na mwanasiasa mashuhuri kutoka Nigeria, Prince Ned Nwoko, dhidi ya Mke wake, Mwigizaji maarufu wa filamu za Nigeria (Nollywood) Regina Daniels. Kupitia chapisho la video kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nwoko amemshutumu Regina kwa kile alichokiita "vurugu za kupindukia" pamoja na matumizi mabaya ya dawa za kulevya na pombe.
Katika maneno yake, Ned aliandika: “Hakuwa hivi mwanzo… kile kinachotokea sasa kimeharibu kabisa utulivu wa familia yetu.”
Nwoko alieleza kuwa ndani ya saa 48, Regina alifanya fujo kubwa nyumbani kwao akiwapiga Wafanyakazi watatu wa ndani, kuharibu mali, na kusababisha uharibifu mkubwa bila sababu ya msingi.
Kwa mujibu wa chapisho hilo la Instagram: “Nimetoa masharti ya wazi kwake. Lazima akubali kwenda kwenye tiba ya kuacha dawa, iwe ndani au nje ya Nchi. Vinginevyo, naogopa kwa usalama wake.” - Prince Ned Nwoko.
Katika tuhuma hizo, Ned alimtaja mtu aitwaye Sammy kama Muuzaji mkuu wa dawa kwa Regina, huku pia akilitaja jina la Ann, akisema anahusika katika kile alichokiita “mzunguko wa maovu.”
Tukio hili limetikisa jamii ya mtandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakionesha mshangao, wengine wakimtetea Regina, na wengi wakitaka ukweli wa kina juu ya maisha ya kifahari ya wawili hao.
Je, hii ni drama ya ndoa ya Mastaa au kuna jambo kubwa zaidi nyuma ya pazia?

0 Σχόλια
·0 Μοιράστηκε
·16 Views