Arnold Schwarzenegger awasilisha mpango wa kuokoa demokrasia Marekani.
Mwigizaji Nguli wa Hollywood na Gavana wa zamani wa Jimbo la California, Arnold Schwarzenegger, ameibuka na pendekezo la kina la kuimarisha demokrasia Nchini Marekani. Katika mahojiano yake kwenye kipindi maarufu cha Real Time with Bill Maher, Schwarzenegger alifichua mpango wa hatua tatu ambao anauona kama njia ya “kupatanisha pande zote mbili” yaani Republican na Democratic. Katika maelezo yake rasmi, Schwarzenegger alisema:
“Tunapaswa kutangaza Siku ya Uchaguzi kuwa likizo ya kitaifa, kuhakikisha kuwa ramani za kisiasa zinatengenezwa na tume huru zisizoegemea upande wowote, na kuimarisha mifumo ya utambulisho wa wapiga kura.”
Mpango huu, ambao una lengo la kuhamasisha ushiriki mpana wa Wananchi na kulinda uadilifu wa chaguzi, umeungwa mkono na hoja za kisera zinazoegemea misingi ya haki, usawa na uwazi.
Schwarzenegger pia hakusita kuelezea wasiwasi wake kuhusu Pendekezo la 50 la California, akiliona kama:
“Hila kubwa ambayo inaweza kurudisha ramani za uchaguzi mikononi mwa Wanasiasa badala ya Wataalamu huru.”
Kwa mujibu wake, hatua hiyo ya kuruhusu Wanasiasa kushiriki katika uundwaji wa ramani ya majimbo inaweza kuathiri vibaya uwakilishi wa haki kwa Wananchi.
Mpango huu wa Schwarzenegger una mvuto wa kipekee kwa kuwa unachanganya ushawishi wa jina kubwa na hoja nzito za kisera. Hata hivyo, utekelezaji wake unategemea mabadiliko ya kisheria, mjadala wa kina wa kitaifa, na maridhiano kati ya vyama viwili vikuu vya siasa.
Kwa mujibu wa Wachambuzi wa siasa za Marekani, hoja za Schwarzenegger zinaibua maswali mapana kuhusu:
- Usawa katika chaguzi,
- Usalama wa mfumo wa upigaji kura,
- Na mwelekeo wa demokrasia ya Marekani kwa vizazi vijavyo.
Mpaka sasa, bado haijajulikana iwapo pendekezo hili litaungwa mkono na Wabunge, lakini bila shaka, Schwarzenegger amejipambanua tena, safari hii siyo kwenye sinema au siasa za majimbo tu, bali kwenye uwanja mpana wa mustakabali wa kidemokrasia wa taifa lake.

0 Σχόλια
·0 Μοιράστηκε
·17 Views