Cristiano Ronaldo amkingia kifua Garnacho: “Waacheni Watoto wafurahie mpira”.

Cristiano Ronaldo ameibuka na kutetea kijana wa Manchester United, Alejandro Garnacho, kufuatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa Argentina wanaompinga kuiga mtindo wa kusherehekea mabao wa Ronaldo anapofunga mabao.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Ronaldo alionyesha mshangao wake juu ya jinsi mashabiki wa Argentina wanavyomshambulia Garnacho kwa sababu ya kusherehekea kama yeye badala ya Lionel Messi, ambaye ni Mchezaji wa taifa lao.

“Nchini Argentina, wanasema Garnacho asisherehekee kama Cristiano, kwamba si jambo jema. Ninaliona hilo kuwa la ajabu, ni Mtoto tu, waacheni acheze,” alisema Ronaldo kwa msisitizo.

Nyota huyo mwenye mafanikio makubwa pia aliongeza kuwa hajawahi kuwazuia Wachezaji wa Ureno kumpenda Messi, akisema: "Sijawahi kumwambia Mchezaji yeyote wa Ureno asimpenda Messi.”

Kauli hii ya Ronaldo imepokelewa kwa hisia tofauti mtandaoni, huku wengi wakimpongeza kwa kukubali tofauti na kuonyesha ukomavu wa hali ya juu katika soka. Ronaldo na Messi wamekuwa wakilinganishwa kwa miaka mingi, lakini kauli hii inaonesha dalili ya kuheshimiana zaidi kuliko ushindani.

Mashabiki wanaendelea kufuatilia kwa karibu uhusiano huu unaoibuka kati ya kizazi kipya kama Garnacho na Wachezaji wakongwe waliowatangulia.
Cristiano Ronaldo amkingia kifua Garnacho: “Waacheni Watoto wafurahie mpira”. Cristiano Ronaldo ameibuka na kutetea kijana wa Manchester United, Alejandro Garnacho, kufuatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa Argentina wanaompinga kuiga mtindo wa kusherehekea mabao wa Ronaldo anapofunga mabao. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Ronaldo alionyesha mshangao wake juu ya jinsi mashabiki wa Argentina wanavyomshambulia Garnacho kwa sababu ya kusherehekea kama yeye badala ya Lionel Messi, ambaye ni Mchezaji wa taifa lao. “Nchini Argentina, wanasema Garnacho asisherehekee kama Cristiano, kwamba si jambo jema. Ninaliona hilo kuwa la ajabu, ni Mtoto tu, waacheni acheze,” alisema Ronaldo kwa msisitizo. Nyota huyo mwenye mafanikio makubwa pia aliongeza kuwa hajawahi kuwazuia Wachezaji wa Ureno kumpenda Messi, akisema: "Sijawahi kumwambia Mchezaji yeyote wa Ureno asimpenda Messi.” Kauli hii ya Ronaldo imepokelewa kwa hisia tofauti mtandaoni, huku wengi wakimpongeza kwa kukubali tofauti na kuonyesha ukomavu wa hali ya juu katika soka. Ronaldo na Messi wamekuwa wakilinganishwa kwa miaka mingi, lakini kauli hii inaonesha dalili ya kuheshimiana zaidi kuliko ushindani. Mashabiki wanaendelea kufuatilia kwa karibu uhusiano huu unaoibuka kati ya kizazi kipya kama Garnacho na Wachezaji wakongwe waliowatangulia.
0 Commentaires ·0 Parts ·28 Vue