Manchester City ilipata shujaa mpya kutoka kwa nyota wao wakubwa katika harakati zao za kunyakua taji la nne mfululizo la ligi ya Premier.

Pep Guardiola alichukua hatua ya tahadhari alipomtoa kipa Ederson, huku City wakiwa kifua mbele kwa bao 1-0, baada ya mlinda lango namba moja kupata pigo baya kichwani baada ya kugongana na beki wa Tottenham, Cristian Romero.

Ederson, ambaye alikuwa na tatizo la jicho lake, hakuonekana kufurahishwa na uamuzi huo - uliotokana na ushauri wa daktari wa klabu - lakini meneja wake alikuwa na haki kabisa, sio tu kumlinda kipa huyo wa Brazil lakini pia alikuwa na imani na mbadala wake Stefan Ortega.

Na katika kipindi cha dakika 21 cha mchezo wa hali ya juu, Ortega - ambaye amefanya vyema kila anapotoka benchi kuchukua mahala pake Ederson msimu huu – huenda amekaribia kuipatia City taji lake la sita katika misimu saba.

Wakati filimbi ya mwisho ilipolia na klabu ikasalia na ushindi mmoja kabla ya kutawazwa mabingwa kwa mara ya nne mfululizo, Guardiola alielekea moja kwa moja kwa Ortega na kumsalimia Mjerumani huyo kwa busu shavuni kwa mchango wake muhimu.

Guardiola hakujizuia kwani alisema: "Ortega ni kipa wa kiwango cha kimataifa. Kipa wa kipekee. Ederson hakupata mtikisiko, alikuwa na tatizo kwenye jicho lake. Hakuona vizuri hivyo daktari alisema. Ninapaswa kumbadilisha."

Spurs waliwafanyia dhihaka wakosoaji ambao walipendekeza wanaweza kutocheza vizuri kimakusudi kwa sababu matokeo yoyote chanya yanaweza kuwapa wapinzani wao Arsenal taji lao la kwanza la Ligi ya Premia ndani ya miaka 20.

Athari ya Ortega ilikuwa ya papo hapo, akimnyima goli mchezaji wa akiba wa Spurs, Dejan Kulusevski , halafu akaokoa shambulio jingine la mchezaji huyo huyo muda mfupi baadaye.

Hatari kubwa zaidi ilikuwa katika dakika za lala salama, huku City wakiwa mbele kwa bao moja, wakati Son Heung-min alipouchukua mpira na kusalia na Ortega pekee.

Ilikuwa ni aina ya fursa ambayo Mkorea Kusini huyo angetumia kwa ustadi mara nyingi katika maisha yake ya Spurs.

.
Manchester City ilipata shujaa mpya kutoka kwa nyota wao wakubwa katika harakati zao za kunyakua taji la nne mfululizo la ligi ya Premier. Pep Guardiola alichukua hatua ya tahadhari alipomtoa kipa Ederson, huku City wakiwa kifua mbele kwa bao 1-0, baada ya mlinda lango namba moja kupata pigo baya kichwani baada ya kugongana na beki wa Tottenham, Cristian Romero. Ederson, ambaye alikuwa na tatizo la jicho lake, hakuonekana kufurahishwa na uamuzi huo - uliotokana na ushauri wa daktari wa klabu - lakini meneja wake alikuwa na haki kabisa, sio tu kumlinda kipa huyo wa Brazil lakini pia alikuwa na imani na mbadala wake Stefan Ortega. Na katika kipindi cha dakika 21 cha mchezo wa hali ya juu, Ortega - ambaye amefanya vyema kila anapotoka benchi kuchukua mahala pake Ederson msimu huu – huenda amekaribia kuipatia City taji lake la sita katika misimu saba. Wakati filimbi ya mwisho ilipolia na klabu ikasalia na ushindi mmoja kabla ya kutawazwa mabingwa kwa mara ya nne mfululizo, Guardiola alielekea moja kwa moja kwa Ortega na kumsalimia Mjerumani huyo kwa busu shavuni kwa mchango wake muhimu. Guardiola hakujizuia kwani alisema: "Ortega ni kipa wa kiwango cha kimataifa. Kipa wa kipekee. Ederson hakupata mtikisiko, alikuwa na tatizo kwenye jicho lake. Hakuona vizuri hivyo daktari alisema. Ninapaswa kumbadilisha." Spurs waliwafanyia dhihaka wakosoaji ambao walipendekeza wanaweza kutocheza vizuri kimakusudi kwa sababu matokeo yoyote chanya yanaweza kuwapa wapinzani wao Arsenal taji lao la kwanza la Ligi ya Premia ndani ya miaka 20. Athari ya Ortega ilikuwa ya papo hapo, akimnyima goli mchezaji wa akiba wa Spurs, Dejan Kulusevski , halafu akaokoa shambulio jingine la mchezaji huyo huyo muda mfupi baadaye. Hatari kubwa zaidi ilikuwa katika dakika za lala salama, huku City wakiwa mbele kwa bao moja, wakati Son Heung-min alipouchukua mpira na kusalia na Ortega pekee. Ilikuwa ni aina ya fursa ambayo Mkorea Kusini huyo angetumia kwa ustadi mara nyingi katika maisha yake ya Spurs. .
Like
Love
5
· 1 Reacties ·0 aandelen ·214 Views