Jay-Z: Nguzo ya kulinda haki na mustakabali wa Wasanii wa Hip-Hop Marekani.
Katika historia ya muziki wa hip-hop, jina la Jay-Z linasimama kama alama ya uongozi, mshikamano na utetezi wa haki za Wasanii. Mbali na mafanikio yake ya kisanii na kibiashara, Jay-Z amejijengea heshima kubwa kwa vitendo vya moja kwa moja vilivyobadili maisha na taaluma za Wasanii wengi wakubwa.
Moja ya hatua zake zilizoacha alama ni kulipia deni la kodi la Lil Wayne lililofikia dola milioni saba za Marekani, hatua iliyomwondolea mzigo mkubwa Mwanamuziki huyo. Aidha, Jay-Z alichangia kwa kiwango kikubwa katika kumtoa Meek Mill Gerezani na baadaye kumsaidia kusaini mkataba wake wa kwanza na kampuni kubwa ya muziki, hatua iliyofungua ukurasa mpya katika maisha yake ya kisanii.
Katika masuala ya uhamiaji, Jay-Z alitumia rasilimali zake kuajiri Mawakili bingwa na kuzuia kufukuzwa nchini Marekani kwa 21 Savage, akisisitiza kuwa haki na utu wa Msanii ni muhimu kuliko taratibu kandamizi. Kwa upande wa biashara ya muziki, alimrudishia Rihanna umiliki kamili wa masters zake, hatua inayowapa Wasanii udhibiti kamili wa kazi zao.
Jay-Z pia alihusika katika kumwondoa DMX kwenye mkataba mgumu na kampuni ya Def Jam, akilenga kumpa uhuru zaidi wa kiubunifu. Alimsaini J. Cole na kumpa uhuru kamili wa ubunifu, mfano hai wa jinsi anavyothamini sauti halisi ya Msanii. Kwa miaka mingi, amekuwa mstari wa mbele kutetea haki za Wasanii na kuhakikisha wanalindwa kisheria.
Katika sakata la mikataba dhalimu, Jay-Z alimsaidia Hit-Boy kujinasua kutoka mkataba wa uchapishaji wa miaka 18 uliokuwa wa kinyonyaji. Vilevile, ametoa msaada mkubwa kwa Wanamuziki Wanawake na Watayarishaji wa muziki, pamoja na kusimamia utetezi wa maandishi ya Wasanii Mahakamani.
Hatua nyingine kubwa ni kununua masters za Kanye West na kumrudishia mmiliki halali, sambamba na juhudi zake kuhakikisha Wasanii wanapata royalties na haki zao za uchapishaji kwa wakati na kwa haki.
Kwa kuzingatia mchango huu mpana, wengi wanakubaliana na kauli kwamba “Hakuna aliyefanya makubwa zaidi kwa ajili ya Marapa na Wasanii wa hip-hop kama Jay-Z.” Ni urithi wa vitendo, si maneno, unaoendelea kuunda mustakabali bora wa tasnia ya muziki.
Toa maoni yako

0 Kommentare
0 Anteile
64 Ansichten