Waziri wa Habari Uganda akemea shambulio la kijeshi nyumbani kwa Bobi Wine.
Waziri wa Habari nchini Uganda, Chris Baryomunsi, amelaani vikali madai ya shambulio la kijeshi lililofanyika katika makazi ya Mwanasiasa wa upinzani Bobi Wine, akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kisheria ya kumzuia kurejea nyumbani kwake.
Akizungumza na shirika la habari la Reuters, Baryomunsi alisema kuwa Bobi Wine hakufanya kosa lolote na anastahili kulindwa kama raia mwingine yeyote wa Uganda. Alieleza wazi kuwa hatua zozote za vitisho au uvamizi dhidi ya makazi ya raia hazikubaliki. Alisema, “Bobi Wine hana kosa lolote alilofanya, na ana haki kamili ya kurejea nyumbani kwake bila hofu.”
Kwa upande wake, Bobi Wine amekuwa akidai kwa muda mrefu kuwa yuko mafichoni akihofia usalama wake, baada ya kudai kuwa jeshi la Uganda lilipewa maagizo ya kumtafuta na kumkamata. Kiongozi huyo wa upinzani pia amedai kuwa baadhi ya Wanafamilia wake waliwahi kukamatwa kwa nguvu, jambo lililoongeza hofu juu ya usalama wake binafsi.
Katika mazingira hayo ya mvutano, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amekuwa akitoa kauli kupitia mtandao wa X (Zamani Twitter), akidokeza kuwa kumkamata Bobi Wine si jambo gumu kwani wanajua alipojificha. Kauli hizo zimeibua mjadala mkubwa ndani na nje ya Uganda kuhusu heshima ya haki za binadamu na uhuru wa kisiasa.
Tukio hili linaendelea kufuatiliwa kwa karibu na wadau wa siasa pamoja na mashirika ya haki za binadamu, huku wito ukitolewa kwa mamlaka za Uganda kuheshimu sheria, kulinda raia wao, na kuhakikisha kuwa tofauti za kisiasa hazigeuki kuwa vitisho vya usalama kwa watu binafsi.
Toa maoni yako
#Habari

0 Comments
0 Shares
9 Views