Trump afikiria kutuma Meli ya pili ya kubeba Ndege Mashariki ya Kati wakati mazungumzo na Iran yakirejea.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anafikiria kuongeza uwepo wa kijeshi wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati kwa kutuma Meli ya pili ya kivita ya kubeba ndege, licha ya juhudi zinazoendelea za kidiplomasia kati ya Washington na Tehran.

Akizungumza na vyombo vya habari vya Channel 12 na Axios, Trump alithibitisha kuwa wazo hilo liko mezani, akisema kuwa “anafikiria kutuma Meli ya pili ya kubeba ndege Mashariki ya Kati.” Kauli hiyo inakuja wakati Marekani na Iran zikijiandaa kuanza tena mazungumzo yanayolenga kuepusha mzozo mpya wa kijeshi au wa kisiasa katika ukanda huo wenye mvutano wa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa za kijeshi, Manowari za kivita zinazotajwa kuweza kupelekwa ni USS George Washington iliyoko barani Asia na USS George HW Bush iliyoko katika Pwani ya mashariki ya Marekani. Aidha, Pentagon inaweza pia kupeleka Meli ya kivita ya USS Gerald R. Ford kutoka eneo la Karibiani kwenda Mashariki ya Kati, iwapo uamuzi huo utapitishwa rasmi.

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Israeli, Trump alionya kuwa hatua kali zinaweza kuchukuliwa endapo mazungumzo hayatatoa matokeo. Alisema Marekani italazimika kufanya “jambo gumu sana” ikiwa makubaliano hayatafikiwa na Iran.

Hatua hiyo inayozingatiwa na Washington inakuja wakati Oman ikiendelea kuwa msuluhishi muhimu katika juhudi za kupunguza mvutano kati ya pande hizo mbili. Wiki iliyopita, Oman iliwezesha mazungumzo kati ya Iran na Marekani, hatua ambayo imeelezwa na Tehran kuwa ya kutia matumaini.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema mazungumzo hayo “yameiruhusu Tehran kupima uzito wa Washington na kuonyesha makubaliano ya kutosha kwa diplomasia kuendelea.” Kauli hiyo inaashiria kuwa licha ya maandalizi ya kijeshi, milango ya mazungumzo bado iko wazi.

Kwa sasa, macho ya jumuiya ya kimataifa yanaelekezwa katika mwenendo wa mazungumzo hayo na maamuzi ya kijeshi yatakayochukuliwa na Marekani, hatua ambazo zinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa utulivu wa Mashariki ya Kati.

Toa maoni yako
#Habari
Trump afikiria kutuma Meli ya pili ya kubeba Ndege Mashariki ya Kati wakati mazungumzo na Iran yakirejea. Rais wa Marekani Donald Trump amesema anafikiria kuongeza uwepo wa kijeshi wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati kwa kutuma Meli ya pili ya kivita ya kubeba ndege, licha ya juhudi zinazoendelea za kidiplomasia kati ya Washington na Tehran. Akizungumza na vyombo vya habari vya Channel 12 na Axios, Trump alithibitisha kuwa wazo hilo liko mezani, akisema kuwa “anafikiria kutuma Meli ya pili ya kubeba ndege Mashariki ya Kati.” Kauli hiyo inakuja wakati Marekani na Iran zikijiandaa kuanza tena mazungumzo yanayolenga kuepusha mzozo mpya wa kijeshi au wa kisiasa katika ukanda huo wenye mvutano wa muda mrefu. Kwa mujibu wa taarifa za kijeshi, Manowari za kivita zinazotajwa kuweza kupelekwa ni USS George Washington iliyoko barani Asia na USS George HW Bush iliyoko katika Pwani ya mashariki ya Marekani. Aidha, Pentagon inaweza pia kupeleka Meli ya kivita ya USS Gerald R. Ford kutoka eneo la Karibiani kwenda Mashariki ya Kati, iwapo uamuzi huo utapitishwa rasmi. Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Israeli, Trump alionya kuwa hatua kali zinaweza kuchukuliwa endapo mazungumzo hayatatoa matokeo. Alisema Marekani italazimika kufanya “jambo gumu sana” ikiwa makubaliano hayatafikiwa na Iran. Hatua hiyo inayozingatiwa na Washington inakuja wakati Oman ikiendelea kuwa msuluhishi muhimu katika juhudi za kupunguza mvutano kati ya pande hizo mbili. Wiki iliyopita, Oman iliwezesha mazungumzo kati ya Iran na Marekani, hatua ambayo imeelezwa na Tehran kuwa ya kutia matumaini. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema mazungumzo hayo “yameiruhusu Tehran kupima uzito wa Washington na kuonyesha makubaliano ya kutosha kwa diplomasia kuendelea.” Kauli hiyo inaashiria kuwa licha ya maandalizi ya kijeshi, milango ya mazungumzo bado iko wazi. Kwa sasa, macho ya jumuiya ya kimataifa yanaelekezwa katika mwenendo wa mazungumzo hayo na maamuzi ya kijeshi yatakayochukuliwa na Marekani, hatua ambazo zinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa utulivu wa Mashariki ya Kati. Toa maoni yako #Habari
0 Commenti 0 condivisioni 78 Views