RDC: Majeshi ya Congo na Uganda yatathmini operesheni SHUJAA Beni.

Luteni Jenerali Ychalingonza Nduru Jacques ameongoza kikao cha tathmini ya operesheni za pamoja za kijeshi kati ya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) katika Mji wa Beni, Mkoa wa Nord-Kivu.

Kikao hicho kilifanyika siku ya Jana Jumanne na kuhudhuriwa pia na Luteni Jenerali Kayanja Muhanga kutoka Uganda pamoja na Makamanda wengine waandamizi wa majeshi ya mataifa hayo mawili. Mkutano huo ni mwendelezo wa kikao kilichofanyika Mjini Kinshasa mwezi Juni 2025, kilicholenga kutathmini operesheni ya kuwasaka Wapiganaji wa kundi la ADF-MTN-ISCARP na kurekebisha mikakati ya kukabiliana na vitisho vipya vya kiusalama.

Operesheni SHUJAA ni ushirikiano wa kijeshi kati ya Congo na Uganda unaolenga kutokomeza makundi ya Waasi na magaidi yanayohatarisha usalama mashariki mwa Congo, hususan katika maeneo ya Beni, Lubero na Ituri.

Katika tathmini hiyo, Viongozi hao wa kijeshi wamepongeza mafanikio ya kimkakati yaliyopatikana katika operesheni hizo, wakieleza kuwa mashambulizi kadhaa ya makundi yenye silaha yamezuiwa na miundombinu yao kuvurugwa. Hata hivyo, wamebainisha kuwa bado kuna mashambulizi yanayoendelea katika baadhi ya maeneo, jambo linaloashiria umuhimu wa kuimarisha zaidi operesheni za usalama.

Maeneo ya Lubero, Beni na Ituri yamekuwa yakikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa makundi yenye silaha, hasa ADF, hali inayosababisha vifo vya Raia na maelfu ya wananchi kulazimika kuyahama makazi yao.

Viongozi hao wawili wa kijeshi wameisisitiza haja ya kuongeza nguvu katika operesheni za pamoja, kuimarisha uratibu wa kijasusi na kuendelea na mikakati madhubuti ili kurejesha amani ya kudumu katika ukanda huo.

Tathmini hiyo inatajwa kuwa hatua muhimu katika kuendeleza ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili, huku ikionyesha dhamira ya pamoja ya kukabiliana na vitisho vya usalama vinavyoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Toa maoni yako

#Habari
RDC: Majeshi ya Congo na Uganda yatathmini operesheni SHUJAA Beni. Luteni Jenerali Ychalingonza Nduru Jacques ameongoza kikao cha tathmini ya operesheni za pamoja za kijeshi kati ya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) katika Mji wa Beni, Mkoa wa Nord-Kivu. Kikao hicho kilifanyika siku ya Jana Jumanne na kuhudhuriwa pia na Luteni Jenerali Kayanja Muhanga kutoka Uganda pamoja na Makamanda wengine waandamizi wa majeshi ya mataifa hayo mawili. Mkutano huo ni mwendelezo wa kikao kilichofanyika Mjini Kinshasa mwezi Juni 2025, kilicholenga kutathmini operesheni ya kuwasaka Wapiganaji wa kundi la ADF-MTN-ISCARP na kurekebisha mikakati ya kukabiliana na vitisho vipya vya kiusalama. Operesheni SHUJAA ni ushirikiano wa kijeshi kati ya Congo na Uganda unaolenga kutokomeza makundi ya Waasi na magaidi yanayohatarisha usalama mashariki mwa Congo, hususan katika maeneo ya Beni, Lubero na Ituri. Katika tathmini hiyo, Viongozi hao wa kijeshi wamepongeza mafanikio ya kimkakati yaliyopatikana katika operesheni hizo, wakieleza kuwa mashambulizi kadhaa ya makundi yenye silaha yamezuiwa na miundombinu yao kuvurugwa. Hata hivyo, wamebainisha kuwa bado kuna mashambulizi yanayoendelea katika baadhi ya maeneo, jambo linaloashiria umuhimu wa kuimarisha zaidi operesheni za usalama. Maeneo ya Lubero, Beni na Ituri yamekuwa yakikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa makundi yenye silaha, hasa ADF, hali inayosababisha vifo vya Raia na maelfu ya wananchi kulazimika kuyahama makazi yao. Viongozi hao wawili wa kijeshi wameisisitiza haja ya kuongeza nguvu katika operesheni za pamoja, kuimarisha uratibu wa kijasusi na kuendelea na mikakati madhubuti ili kurejesha amani ya kudumu katika ukanda huo. Tathmini hiyo inatajwa kuwa hatua muhimu katika kuendeleza ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili, huku ikionyesha dhamira ya pamoja ya kukabiliana na vitisho vya usalama vinavyoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Toa maoni yako #Habari
0 Comments 0 Shares 87 Views