Mbunge wa Congo aibua taharuki baada ya kudaiwa kuchaguliwa pia Uganda.
Kashfa ya kisiasa imeibuka na kuzua mjadala mzito katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya taarifa kudai kuwa Mbunge wa kitaifa aliyechaguliwa mwaka 2023 nchini humo, amechaguliwa tena kuwa Mbunge wa kitaifa nchini Uganda mwaka 2026.
Robert Agenonga, ambaye alichaguliwa mwaka 2023 katika jimbo la Mahagi, Mkoani Ituri, kwa takribani kura 20,000, sasa anatajwa kuwa katikati ya mzozo mkubwa wa kisiasa.
Agenonga aliingia Bungeni kupitia Muungano wa kisiasa wa 4AC, unaohusishwa kwa karibu na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu wa zamani, Peter Kazadi, pamoja na Waziri Msaidizi wa sasa wa Ulinzi, Eliezer Ntambwe.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vinavyoelezwa kuwa vinafanana katika taarifa zao, Mbunge huyo wa Congo alichaguliwa kuwa Mbunge wa kitaifa nchini Uganda mwaka 2026. Ikiwa madai hayo yatathibitishwa rasmi, hali hiyo inaweza kuibua maswali mazito ya kisheria na kisiasa.
Wachambuzi wa masuala ya utawala wanaeleza kuwa tukio hilo linaweza kugusa moja kwa moja hoja ya uraia wa nchi mbili, uaminifu wa kikatiba kwa taasisi za taifa, pamoja na uhalali wa mchakato wa uchaguzi katika nchi zote mbili. Sheria za uchaguzi na katiba za mataifa hayo zina masharti yanayohusu utiifu wa Viongozi kwa dola moja, jambo linaloweza kuathiri hadhi ya uwakilishi wake.
Hadi kufikia sasa, hakuna tamko rasmi lililotolewa na Robert Agenonga mwenyewe wala mamlaka za Congo kuhusiana na taarifa hizo. Hata hivyo, sakata hili linaelezwa kuwa linaweza kuchukua sura ya kitaifa na hata kuathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kinshasa na Kampala iwapo litathibitishwa.
Maendeleo zaidi yanatarajiwa huku umma ukisubiri kauli ya Wahusika na taasisi husika kuhusu uhalali wa madai hayo.
Toa maoni yako
#Habari

0 Commenti
0 condivisioni
58 Views