“NATULIZANA” NI WIMBO MBOVU MNO

Msanii mkubwa kama Diamond Platnumz, kutoa wimbo dhaifu ni kosa lisilosameheka. Natulizana siyo wimbo mbaya tu, bali ni mfano wa wazi kabisa ni kazi isiyoendana na hadhi aliyonayo Diamond Platnumz.

Maneno aliyoyatumia kwenye wimbo huu ni mepesi mno kupita kiasi hayana ujumbe wa maana, Bali ni mkusanyiko wa maneno ya kawaida ambayo yanasikika mara nyingi kwenye nyimbo nyingine. Kwa Diamond, huu ni uzembe wa kisanaa unaokatisha tamaa kwa sisi mashabiki ambao tunatamani siku moja Grammy Ije hapa nchini.

Hata nilivyo sikiliza mdundo (beat) nao ni wa kawaida kupita kiasi, hauja nivutia hata kidogo, na hauleti ladha mpya kabisa hasa kwenye hizi harakati za kuinua Bongo fleva kimataifa.

Samahani sana Diamond Platinumz lakini huu wimbo kwa upande wangu naona kama ni wimbo unaopita tu kwenye masikioni ya watu bila kuacha athari yoyote ile..🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿

Ukweli mchungu ni huu: Nadhani "Natulizana" ni wimbo unaozungumziwa kwasababu jina la Diamond Platnumz lipo juu yake. Kama ungeimbwa na msanii mwingine, usingepata hata nusu ya attention inayopata sasa. Hapa sikosoi kwa chuki, bali ni kwa kisanaa.

Pia, kwa kifupi "Natulizana" ni wimbo mbovu kabisa, usio na sifa halali za kusifiwa. Diamond Platinumz anauwezo mkubwa sana zaidi ya huu wimbo na mashabiki wanapaswa kuongea ukweli ili wachochee mafanikio zaidi na sio kila kitu kusifia.

Ni maoni na uchambuzi wa FredMastori

Toa maoni yako
#Music
#Habari
“NATULIZANA” NI WIMBO MBOVU MNO Msanii mkubwa kama Diamond Platnumz, kutoa wimbo dhaifu ni kosa lisilosameheka. Natulizana siyo wimbo mbaya tu, bali ni mfano wa wazi kabisa ni kazi isiyoendana na hadhi aliyonayo Diamond Platnumz. Maneno aliyoyatumia kwenye wimbo huu ni mepesi mno kupita kiasi hayana ujumbe wa maana, Bali ni mkusanyiko wa maneno ya kawaida ambayo yanasikika mara nyingi kwenye nyimbo nyingine. Kwa Diamond, huu ni uzembe wa kisanaa unaokatisha tamaa kwa sisi mashabiki ambao tunatamani siku moja Grammy Ije hapa nchini. Hata nilivyo sikiliza mdundo (beat) nao ni wa kawaida kupita kiasi, hauja nivutia hata kidogo, na hauleti ladha mpya kabisa hasa kwenye hizi harakati za kuinua Bongo fleva kimataifa. Samahani sana Diamond Platinumz lakini huu wimbo kwa upande wangu naona kama ni wimbo unaopita tu kwenye masikioni ya watu bila kuacha athari yoyote ile..🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿 Ukweli mchungu ni huu: Nadhani "Natulizana" ni wimbo unaozungumziwa kwasababu jina la Diamond Platnumz lipo juu yake. Kama ungeimbwa na msanii mwingine, usingepata hata nusu ya attention inayopata sasa. Hapa sikosoi kwa chuki, bali ni kwa kisanaa. Pia, kwa kifupi "Natulizana" ni wimbo mbovu kabisa, usio na sifa halali za kusifiwa. Diamond Platinumz anauwezo mkubwa sana zaidi ya huu wimbo na mashabiki wanapaswa kuongea ukweli ili wachochee mafanikio zaidi na sio kila kitu kusifia. Ni maoni na uchambuzi wa FredMastori Toa maoni yako #Music #Habari
0 Yorumlar 0 hisse senetleri 58 Views