AFC/M23 yasisitiza utekelezaji wa makubaliano ya Doha, yaituhumu Kinshasa kwa “Mbinu za mawasiliano”.

Muungano wa Waasi wa AFC/M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umetangaza upya msimamo wake kuhusu wito wa kusitisha mapigano, ukisema uko tayari kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kupitia mchakato wa Doha, huku ukitupia lawama Serikali ya Kinshasa kwa kile ilichokiita “mbinu za mawasiliano” zenye lengo la kupotosha (kutangaza uongo) umma.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Kiongozi wa AFC/M23, Corneille Naanga, Muungano huo ulieleza kuwa uko tayari kuchukua hatua mara moja katika kutekeleza utaratibu wa usitishaji mapigano uliokubaliwa.

Naanga alisema: "Kufuatia wito unaoendelea wa kusitisha mapigano, AFC/M23 inathibitisha tena dhamira yake ya kutekeleza, bila kuchelewa na kwa nia njema, utaratibu uliokubaliwa katika mfumo wa mchakato wa Doha. Hatua hii inaendana na mantiki ya uwajibikaji wa kisiasa na nia ya dhati ya kufikia suluhu ya mazungumzo, ya kudumu na shirikishi ya mzozo huu.”

Kauli hiyo inaashiria msimamo wa AFC/M23 wa kuonyesha utayari wa kushiriki katika juhudi za kidiplomasia zinazolenga kumaliza mzozo wa muda mrefu mashariki mwa DRC.

Hata hivyo, Muungano huo uliikosoa vikali Serikali ya DRC yenye makao yake Kinshasa, ukidai kuwa tangazo la kukubali kusitisha mapigano si la dhati.

Naanga aliongeza: “Kwa AFC, kile kinachodaiwa kuwa kukubali kwa Kinshasa kanuni ya kusitisha mapigano ni mbinu tu ya mawasiliano na jaribio la upotoshaji linalolenga kudanganya maoni ya kitaifa na kimataifa, kujiepusha na wajibu wake na kuficha mwendelezo wa mkakati wa kijeshi usiobadilika.”

Kauli hiyo inaibua mvutano mpya wa kisiasa wakati juhudi za kimataifa zikiongezeka kuhimiza pande husika kurejea katika meza ya mazungumzo kupitia mchakato wa Doha.

Mzozo kati ya serikali ya DRC na AFC/M23 umeendelea kuathiri hali ya usalama na kibinadamu mashariki mwa nchi hiyo, huku jumuiya ya kimataifa ikiendelea kusisitiza umuhimu wa suluhu ya mazungumzo badala ya mapambano ya kijeshi.

Toa maoni yako
#Habari
AFC/M23 yasisitiza utekelezaji wa makubaliano ya Doha, yaituhumu Kinshasa kwa “Mbinu za mawasiliano”. Muungano wa Waasi wa AFC/M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umetangaza upya msimamo wake kuhusu wito wa kusitisha mapigano, ukisema uko tayari kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kupitia mchakato wa Doha, huku ukitupia lawama Serikali ya Kinshasa kwa kile ilichokiita “mbinu za mawasiliano” zenye lengo la kupotosha (kutangaza uongo) umma. Kupitia taarifa iliyotolewa na Kiongozi wa AFC/M23, Corneille Naanga, Muungano huo ulieleza kuwa uko tayari kuchukua hatua mara moja katika kutekeleza utaratibu wa usitishaji mapigano uliokubaliwa. Naanga alisema: "Kufuatia wito unaoendelea wa kusitisha mapigano, AFC/M23 inathibitisha tena dhamira yake ya kutekeleza, bila kuchelewa na kwa nia njema, utaratibu uliokubaliwa katika mfumo wa mchakato wa Doha. Hatua hii inaendana na mantiki ya uwajibikaji wa kisiasa na nia ya dhati ya kufikia suluhu ya mazungumzo, ya kudumu na shirikishi ya mzozo huu.” Kauli hiyo inaashiria msimamo wa AFC/M23 wa kuonyesha utayari wa kushiriki katika juhudi za kidiplomasia zinazolenga kumaliza mzozo wa muda mrefu mashariki mwa DRC. Hata hivyo, Muungano huo uliikosoa vikali Serikali ya DRC yenye makao yake Kinshasa, ukidai kuwa tangazo la kukubali kusitisha mapigano si la dhati. Naanga aliongeza: “Kwa AFC, kile kinachodaiwa kuwa kukubali kwa Kinshasa kanuni ya kusitisha mapigano ni mbinu tu ya mawasiliano na jaribio la upotoshaji linalolenga kudanganya maoni ya kitaifa na kimataifa, kujiepusha na wajibu wake na kuficha mwendelezo wa mkakati wa kijeshi usiobadilika.” Kauli hiyo inaibua mvutano mpya wa kisiasa wakati juhudi za kimataifa zikiongezeka kuhimiza pande husika kurejea katika meza ya mazungumzo kupitia mchakato wa Doha. Mzozo kati ya serikali ya DRC na AFC/M23 umeendelea kuathiri hali ya usalama na kibinadamu mashariki mwa nchi hiyo, huku jumuiya ya kimataifa ikiendelea kusisitiza umuhimu wa suluhu ya mazungumzo badala ya mapambano ya kijeshi. Toa maoni yako #Habari
0 Комментарии 0 Поделились 39 Просмотры