Mwigizaji wa Nollywood Maurice Sam, mtandaoni yachafukwa baada ya shambulio la risasi.

Mwigizaji wa filamu za Nollywood, Nigeria, Maurice Sam, amesambaa kwenye vichwa vya habari mtandaoni baada ya taarifa zinazodai kuwa alishambuliwa kwa risasi jana Februari 13, 2026 akiwa kwenye seti ya filamu yake mpya. Tukio hili lilianza kuchipuka mtandaoni baada ya Mwanaharakati maarufu wa mitandao, Very Dark Man, kuposti picha na madai ya kwamba Mwigizaji huyo alikuwa amejeruhiwa vibaya na alikuwa akifikiria kuondoka Nigeria ili kulinda usalama wake.

Ripoti kutoka tovuti ya Latest Nigerian News inaeleza kuwa baadhi ya picha zilizosambazwa mtandaoni zinaonyesha Gari lililoharibiwa na alama za risasi, jambo lililoashiria hatari kubwa aliyokabiliana nayo Mwigizaji huyo. Mada hii iliibua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki, wadau wa filamu, na Watumiaji wa mitandao ya kijamii, huku wengi wakihoji ni nini hasa kilichosababisha tukio hili na kuzingatia juhudi za Maurice Sam kujijenga kibiashara na kupata nafasi kubwa ndani ya tasnia ya Nollywood.

Mchambuzi mmoja wa tasnia ya filamu alisema: “Ni jambo linalotia wasiwasi kuona msanii chipukizi akikabiliwa na tukio la aina hii. Inaleta mjadala juu ya usalama wa wasanii na hali ya kazi kwenye tasnia ya filamu nchini Nigeria.”

Hata hivyo, ripoti hizo pia zinaonyesha wazi kuwa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa Mwigizaji, Polisi, au vyombo vya habari vikuu. Taarifa hizi zinazozagaa zinatokana zaidi na mitandao ya kijamii, na bado hazina uthibitisho wa moja kwa moja wa jeraha lolote lililopatikana.

Kwa sasa, Maurice Sam yupo salama, ingawa duru zinaeleza kuwa tukio hili limemuathiri kisaikolojia kiasi cha kuanza kufikiria kuachana na uigizaji na kuwekeza katika shughuli nyingine za kibiashara. Tukio hili limeibua mjadala wa kimataifa kuhusu hatari zinazoweza kutokea kwa Wasanii chipukizi, huku wadau wa tasnia wakihimiza tahadhari na uangalizi zaidi kwenye seti za filamu.

Toa maoni yako
#Filamu
#Habari
Mwigizaji wa Nollywood Maurice Sam, mtandaoni yachafukwa baada ya shambulio la risasi. Mwigizaji wa filamu za Nollywood, Nigeria, Maurice Sam, amesambaa kwenye vichwa vya habari mtandaoni baada ya taarifa zinazodai kuwa alishambuliwa kwa risasi jana Februari 13, 2026 akiwa kwenye seti ya filamu yake mpya. Tukio hili lilianza kuchipuka mtandaoni baada ya Mwanaharakati maarufu wa mitandao, Very Dark Man, kuposti picha na madai ya kwamba Mwigizaji huyo alikuwa amejeruhiwa vibaya na alikuwa akifikiria kuondoka Nigeria ili kulinda usalama wake. Ripoti kutoka tovuti ya Latest Nigerian News inaeleza kuwa baadhi ya picha zilizosambazwa mtandaoni zinaonyesha Gari lililoharibiwa na alama za risasi, jambo lililoashiria hatari kubwa aliyokabiliana nayo Mwigizaji huyo. Mada hii iliibua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki, wadau wa filamu, na Watumiaji wa mitandao ya kijamii, huku wengi wakihoji ni nini hasa kilichosababisha tukio hili na kuzingatia juhudi za Maurice Sam kujijenga kibiashara na kupata nafasi kubwa ndani ya tasnia ya Nollywood. Mchambuzi mmoja wa tasnia ya filamu alisema: “Ni jambo linalotia wasiwasi kuona msanii chipukizi akikabiliwa na tukio la aina hii. Inaleta mjadala juu ya usalama wa wasanii na hali ya kazi kwenye tasnia ya filamu nchini Nigeria.” Hata hivyo, ripoti hizo pia zinaonyesha wazi kuwa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa Mwigizaji, Polisi, au vyombo vya habari vikuu. Taarifa hizi zinazozagaa zinatokana zaidi na mitandao ya kijamii, na bado hazina uthibitisho wa moja kwa moja wa jeraha lolote lililopatikana. Kwa sasa, Maurice Sam yupo salama, ingawa duru zinaeleza kuwa tukio hili limemuathiri kisaikolojia kiasi cha kuanza kufikiria kuachana na uigizaji na kuwekeza katika shughuli nyingine za kibiashara. Tukio hili limeibua mjadala wa kimataifa kuhusu hatari zinazoweza kutokea kwa Wasanii chipukizi, huku wadau wa tasnia wakihimiza tahadhari na uangalizi zaidi kwenye seti za filamu. Toa maoni yako #Filamu #Habari
0 Commentarios 0 Acciones 12 Views