Ayatollah Khamenei amuonya Trump: “Tunasubiri watushambulie”
Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, ametoa onyo kali kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, akisema kuwa shambulio lolote litakalofanywa na Marekani dhidi ya Iran litakuwa na madhara makubwa kwa Washington na washirika wake.
Akizungumza katika hotuba yake ya hivi karibuni, Ayatollah Khamenei alisisitiza kuwa Iran iko tayari kujibu hatua yoyote ya kijeshi itakayochukuliwa dhidi yake.
“Shambulio lolote la Marekani dhidi ya Iran litakuwa funzo kwa Marekani na washirika wake.” amesema Kiongozi huyo.
Ayatollah Khamenei aliendelea kueleza kuwa taifa lake halitaogopa vitisho vya nje, bali litasimama imara kulinda mamlaka na heshima yake katika jukwaa la kimataifa.
“Tunataka tutoe somo kwa ulimwengu. Tunasubiri watushambulie.”
Kauli hiyo imeongeza joto katika mvutano wa muda mrefu kati ya Tehran na Washington, hasa katika kipindi ambacho kumekuwa na sintofahamu kuhusu masuala ya usalama wa eneo la Mashariki ya Kati, programu ya nyuklia ya Iran, pamoja na ushawishi wa kijeshi wa pande zote mbili katika kanda hiyo.
Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaona kauli hii kama ujumbe wa wazi wa kuonyesha msimamo mkali wa Iran dhidi ya kile kinachoonekana kuwa shinikizo la Marekani. Hata hivyo, bado haijabainika iwapo matamshi haya yatafuatiwa na hatua za moja kwa moja za kijeshi au yatabaki katika kiwango cha tahadhari za kisiasa.
Mvutano kati ya Marekani na Iran umekuwa ukipanda na kushuka kwa miaka kadhaa, huku kila upande ukitoa matamshi makali yanayoashiria uwezekano wa mzozo mkubwa zaidi endapo diplomasia haitapewa kipaumbele.
Toa maoni yako
#Habari

0 Commentarios
0 Acciones
17 Views