Koffi Olomide atangaza tamasha kubwa Ubelgiji baada ya kufutwa matamasha yake Ufaransa.

Mwanamuziki Nguli wa rumba ya Congo, Koffi Olomide, ametangaza rasmi kufanya tamasha kubwa katika Ubelgiji, baada ya kukumbana na changamoto ya kufutwa kwa matamasha kadhaa nchini Ufaransa.

Tamasha hilo limepangwa kufanyika tarehe 11 Julai 2026 katika Uwanja maarufu wa Stade Roi Baudouin uliopo Jijini Brussels. Tangazo hili limeibua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Congo na rumba kwa ujumla barani Ulaya na Afrika.

Kupitia matangazo yake ya moja kwa moja kwenye TikTok, Msanii huyo alieleza dhamira yake ya kuifanya siku hiyo kuwa ya kipekee katika maisha yake ya muziki.

Amesema kuwa anataka tarehe hiyo iwe tukio la kihistoria, akisherehekea miaka yake 70 ya kuzaliwa akiwa pamoja na mashabiki wake.

Tamasha hilo linatajwa kuwa uzalishaji mkubwa (grande production) unaotarajiwa kuvuta maelfu ya watu katika Uwanja huo wenye historia ya kuandaa matukio makubwa ya kimataifa ya michezo na burudani.

Hatua hii inakuja baada ya kufutwa kwa matamasha kadhaa ya Msanii huyo nchini Ufaransa, jambo lililozua mjadala mpana katika tasnia ya muziki. Hata hivyo, tangazo la Brussels linaonekana kama kurejea kwa nguvu kwa Gwiji huyo wa rumba, akionyesha kuwa bado ana ushawishi mkubwa na soko imara barani Ulaya.

Kwa wapenzi wa rumba na muziki wa Congo, tukio hili tayari linaonekana kuwa miongoni mwa matamasha makubwa zaidi ya mwaka 2026. Kwa historia ndefu ya Koffi Olomide katika muziki, tamasha hili linatarajiwa kuwa zaidi ya burudani bali ni sherehe ya urithi, mafanikio na mchango wake katika kukuza rumba ya Kongo kimataifa.

Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu maandalizi rasmi, mauzo ya tiketi na orodha ya Wasanii watakaoshiriki katika usiku huo unaotarajiwa kuwa wa kipekee.

Toa maoni yako
#Habari
Koffi Olomide atangaza tamasha kubwa Ubelgiji baada ya kufutwa matamasha yake Ufaransa. Mwanamuziki Nguli wa rumba ya Congo, Koffi Olomide, ametangaza rasmi kufanya tamasha kubwa katika Ubelgiji, baada ya kukumbana na changamoto ya kufutwa kwa matamasha kadhaa nchini Ufaransa. Tamasha hilo limepangwa kufanyika tarehe 11 Julai 2026 katika Uwanja maarufu wa Stade Roi Baudouin uliopo Jijini Brussels. Tangazo hili limeibua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Congo na rumba kwa ujumla barani Ulaya na Afrika. Kupitia matangazo yake ya moja kwa moja kwenye TikTok, Msanii huyo alieleza dhamira yake ya kuifanya siku hiyo kuwa ya kipekee katika maisha yake ya muziki. Amesema kuwa anataka tarehe hiyo iwe tukio la kihistoria, akisherehekea miaka yake 70 ya kuzaliwa akiwa pamoja na mashabiki wake. Tamasha hilo linatajwa kuwa uzalishaji mkubwa (grande production) unaotarajiwa kuvuta maelfu ya watu katika Uwanja huo wenye historia ya kuandaa matukio makubwa ya kimataifa ya michezo na burudani. Hatua hii inakuja baada ya kufutwa kwa matamasha kadhaa ya Msanii huyo nchini Ufaransa, jambo lililozua mjadala mpana katika tasnia ya muziki. Hata hivyo, tangazo la Brussels linaonekana kama kurejea kwa nguvu kwa Gwiji huyo wa rumba, akionyesha kuwa bado ana ushawishi mkubwa na soko imara barani Ulaya. Kwa wapenzi wa rumba na muziki wa Congo, tukio hili tayari linaonekana kuwa miongoni mwa matamasha makubwa zaidi ya mwaka 2026. Kwa historia ndefu ya Koffi Olomide katika muziki, tamasha hili linatarajiwa kuwa zaidi ya burudani bali ni sherehe ya urithi, mafanikio na mchango wake katika kukuza rumba ya Kongo kimataifa. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu maandalizi rasmi, mauzo ya tiketi na orodha ya Wasanii watakaoshiriki katika usiku huo unaotarajiwa kuwa wa kipekee. Toa maoni yako #Habari
0 Kommentare 0 Anteile 12 Ansichten