Denis Mukwege ataka “Mazungumzo ya Kitaifa” kutatua tatizo la uongozi DRC.
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Dkt. Denis Mukwege, amesema kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inahitaji haraka “Mazungumzo ya Kitaifa” ili kupata suluhisho la kudumu kwa changamoto zinazoikabili nchi hiyo, hususan katika eneo la uongozi.
Akizungumza kuhusu hali ya sasa ya nchi yake, Dkt. Mukwege alieleza kuwa kiini cha matatizo mengi yanayoikumba Congo ni ukosefu wa uongozi bora.
“Iwapo leo Congo inapitia mateso yote tunayoshuhudia, ni kwa sababu tu ya uwepo wa uongozi mbovu. Kama kungekuwa na uongozi mzuri, kwa kawaida Congo ingeweza kulinda raia wake na kusimamia ipasavyo rasilimali zake za madini ambazo kwa sasa zinavunwa na kila aina ya walafi wanaozunguka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.”
Kauli hiyo imekuja wakati nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama, migogoro ya silaha katika maeneo ya mashariki, pamoja na lawama za muda mrefu kuhusu usimamizi wa rasilimali asilia.
Kwa mujibu wa Dkt. Mukwege, suluhisho la kweli halitapatikana kwa hatua za juu juu, bali kupitia mchakato mpana wa kitaifa utakaowaleta pamoja wadau wote muhimu—serikali, vyama vya siasa, Asasi za kiraia na Wawakilishi wa wananchi.
Anaamini kuwa kupitia jukwaa hilo, taifa linaweza kujadili kwa uwazi matatizo ya kiutawala, uwajibikaji wa Viongozi, pamoja na namna bora ya kusimamia utajiri mkubwa wa madini uliopo nchini humo.
DRC ni miongoni mwa mataifa yenye utajiri mkubwa wa madini duniani, ikiwemo cobalt, dhahabu na coltan. Hata hivyo, kwa miaka mingi, rasilimali hizo zimehusishwa na migogoro, rushwa na uingiliaji wa maslahi ya ndani na nje ya nchi.
Kauli ya Dkt. Mukwege inachukuliwa na Wachambuzi wengi kama wito wa mageuzi ya kina katika mifumo ya uongozi na uwajibikaji, ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha Wananchi badala ya makundi machache yenye nguvu.
Kwa sasa, macho ya wengi yanaelekezwa kuona iwapo wito huo wa “Mazungumzo ya Kitaifa” utapokelewa na mamlaka husika na kuwa mwanzo wa mabadiliko yanayohitajika nchini Congo.
Toa maoni yako
#Habari

0 Kommentare
0 Anteile
18 Ansichten