Serikali ya Kenya yachukua hatua kali dhidi ya tuhuma za Raia wa Urusi kusambaza video za faragha.
Serikali ya Kenya imeibuka hadharani na kulaani vikali tuhuma zinazomhusu raia mmoja wa Urusi anayeshukiwa kurekodi na kusambaza video zenye maudhui ya faragha zikihusisha Wanawake wa Kenya bila ridhaa yao.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Jijini Nairobi, mamlaka za Kenya zimeeleza kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na haliwezi kuvumiliwa katika jamii inayoheshimu utu na haki za binadamu.
Katika tamko hilo, serikali imeeleza kuwa tukio hilo ni “kubwa na lisilokubalika”, ikisisitiza kuwa hatua zote muhimu zitachukuliwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke. Aidha, imewahakikishia waathirika wanaodaiwa kuwa watapatiwa msaada stahiki wa kisheria na kisaikolojia.
Vilevile, mamlaka hizo zimeweka bayana kuwa Wahusika wote watakaobainika kuhusika na kitendo hicho watawajibishwa kwa mujibu wa sheria. Serikali imeongeza kuwa haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote anayekiuka faragha na heshima ya wananchi.
Kashfa hiyo imezua hasira kubwa katika mitandao ya kijamii na miongoni mwa Wananchi, huku wengi wakitaka sheria kali zaidi zichukuliwe dhidi ya wanaosambaza maudhui ya faragha bila idhini. Tukio hili limeibua tena mjadala mpana kuhusu ulinzi wa maisha binafsi na mapambano dhidi ya usambazaji wa maudhui ya faragha bila ridhaa nchini Kenya.
Mamlaka husika zimebainisha kuwa uchunguzi rasmi unaendelea, na matokeo yake yatatangazwa pindi yatakapokamilika.
Toa maoni yako
#Habari

0 التعليقات
0 المشاركات
26 مشاهدة