Upgrade to Pro

Taarifa ya hali ya dawa za kulevya Duniani ya mwaka 2023 imeonesha kuwa takribani Watu milioni 219 walitumia bangi mwaka 2021, sawa na 4% ya idadi ya Watu duniani ambapo idadi hiyo imeongezeka kwa 21% katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Taarifa hiyo ambayo imeandaliwa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Nchini (DCEA) na kuwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma leo May 16,2024 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista J. Mhagama inaonesha kuwa matumizi ya bangi yanaendelea kuongezeka kwa kasi duniani kote na kwamba matumizi ya bangi yameendelea kuwa ya juu zaidi Amerika Kaskazini ambapo 17.4% ya Watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 walitumia bangi mwaka 2021.

Barani Afrika taarifa imeonesha kuwa Afrika Kaskazini ni kitovu cha biashara haramu ya bangi iliyosindikwa (cannabis resin) kuelekea Ulaya Magharibi na matumizi ya bangi ni ya juu katika Afrika Magharibi na Kati na kufikia mwaka 2021, karibu 10% ya Watu (milioni 30) waliripotiwa kutumia bangi katika kipindi cha mwaka 2020, hususan katika Nchi ya Nigeria.

Nchi nyingi Afrika zina uzalishaji wa bangi na imeendelea kuwa moja ya dawa inayosababisha athari kubwa miongoni mwa Watu wanaopatiwa matibabu ya uraibu. #MillardAyoUPDATES
Taarifa ya hali ya dawa za kulevya Duniani ya mwaka 2023 imeonesha kuwa takribani Watu milioni 219 walitumia bangi mwaka 2021, sawa na 4% ya idadi ya Watu duniani ambapo idadi hiyo imeongezeka kwa 21% katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Taarifa hiyo ambayo imeandaliwa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Nchini (DCEA) na kuwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma leo May 16,2024 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista J. Mhagama inaonesha kuwa matumizi ya bangi yanaendelea kuongezeka kwa kasi duniani kote na kwamba matumizi ya bangi yameendelea kuwa ya juu zaidi Amerika Kaskazini ambapo 17.4% ya Watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 walitumia bangi mwaka 2021. Barani Afrika taarifa imeonesha kuwa Afrika Kaskazini ni kitovu cha biashara haramu ya bangi iliyosindikwa (cannabis resin) kuelekea Ulaya Magharibi na matumizi ya bangi ni ya juu katika Afrika Magharibi na Kati na kufikia mwaka 2021, karibu 10% ya Watu (milioni 30) waliripotiwa kutumia bangi katika kipindi cha mwaka 2020, hususan katika Nchi ya Nigeria. Nchi nyingi Afrika zina uzalishaji wa bangi na imeendelea kuwa moja ya dawa inayosababisha athari kubwa miongoni mwa Watu wanaopatiwa matibabu ya uraibu. #MillardAyoUPDATES
Like
Love
Wow
11
3 Reacties ·429 Views