"Kifuta jasho" ni maneno mawili maarufu sana kuyakuta midomoni mwa Watu ambao wanazitazama kesho zao kwa kuogopa kuadhirika, Watu wanaoogopa kutaabika huko mbeleni na kujutia nguvu za ujana wao, ni herufi kumi na moja ambazo ukizizingatia zinaweza kukupatia kitambaa cha bei ghali zaidi utapofika muda wa kujifuta jasho ambapo bei hiyo kubwa itatokana na maamuzi yako ya leo kwenye swala la kujiwekea akiba.

Nimeyasema haya baada ya kushuhudia Benki ya NMB ikituletea bidhaa mpya kabisa sokoni katika sekta ya kibenki iitwayo "NMB JIWEKEE" ikiwa ni akaunti maalum ya kidijitali inayolenga kuleta ukombozi wa maisha ya baadaye ya Watu walio nje ya mfumo rasmi wa ajira kama vile Wafanyabiashara wadogo na wa kati, watoa huduma wa sekta ya usafirishaji kwa pikipiki 'bodaboda', Mama na Baba lishe na hata Waajiriwa wanaopenda kujiongezea vyanzo vya akiba ya uzee.

Uzinduzi wa NMB Jiwekee uliowakutanisha pamoja Watu mbalimbali waliokula kiapo cha 'Chama la Watunza Pesa,' ulifanyika jijini Dar es salaam Jumatatu May 13 na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi huku mwenyeji wa hafla hiyo akiwa ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi.

Akizingumza katika uzinduzi huo uliofanyika kwa mfumo wa kipindi cha runinga kilichoongozwa na Mtangazaji Millard Ayo, Waziri Ndejembi alisema NMB Jiwekee inayoambatana na faida lukuki kwa Wajasiriamali na kada zingine, ni mwendelezo wa juhudi za wazi za Taasisi hiyo kuunga mkono jitihada za Serikali kuyawezesha makundi maalum ya kijamii.

"Kwa jambo hili Taasisi nyingine zinapaswa kufuata nyayo za NMB kwa kuanzisha huduma bora na rahisi, nafuu na salama kama hizi, sasa NMB ijikite katika kutoa elimu kwa Watanzania juu ya umuhimu wa huduma hii mpya, Serikali haiwezi 'ku-cover' kila kitu ndio maana tunasisitiza nguvu za Wadau hususani Taasisi za fedha katika kuwaunganisha Watanzania na huduma Jumuishi za fedha, zaidi niwapongeze NMB kwa kuwapa uhuru Watumiaji wa NMB Jiwekee wa kuchagua asilimia za kujitunzia kutokana na matumizi ya fedha zilizo kwenye akaunti zao" —— Ndejembi. #MillardAyoUPDATES
"Kifuta jasho" ni maneno mawili maarufu sana kuyakuta midomoni mwa Watu ambao wanazitazama kesho zao kwa kuogopa kuadhirika, Watu wanaoogopa kutaabika huko mbeleni na kujutia nguvu za ujana wao, ni herufi kumi na moja ambazo ukizizingatia zinaweza kukupatia kitambaa cha bei ghali zaidi utapofika muda wa kujifuta jasho ambapo bei hiyo kubwa itatokana na maamuzi yako ya leo kwenye swala la kujiwekea akiba. Nimeyasema haya baada ya kushuhudia Benki ya NMB ikituletea bidhaa mpya kabisa sokoni katika sekta ya kibenki iitwayo "NMB JIWEKEE" ikiwa ni akaunti maalum ya kidijitali inayolenga kuleta ukombozi wa maisha ya baadaye ya Watu walio nje ya mfumo rasmi wa ajira kama vile Wafanyabiashara wadogo na wa kati, watoa huduma wa sekta ya usafirishaji kwa pikipiki 'bodaboda', Mama na Baba lishe na hata Waajiriwa wanaopenda kujiongezea vyanzo vya akiba ya uzee. Uzinduzi wa NMB Jiwekee uliowakutanisha pamoja Watu mbalimbali waliokula kiapo cha 'Chama la Watunza Pesa,' ulifanyika jijini Dar es salaam Jumatatu May 13 na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi huku mwenyeji wa hafla hiyo akiwa ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi. Akizingumza katika uzinduzi huo uliofanyika kwa mfumo wa kipindi cha runinga kilichoongozwa na Mtangazaji Millard Ayo, Waziri Ndejembi alisema NMB Jiwekee inayoambatana na faida lukuki kwa Wajasiriamali na kada zingine, ni mwendelezo wa juhudi za wazi za Taasisi hiyo kuunga mkono jitihada za Serikali kuyawezesha makundi maalum ya kijamii. "Kwa jambo hili Taasisi nyingine zinapaswa kufuata nyayo za NMB kwa kuanzisha huduma bora na rahisi, nafuu na salama kama hizi, sasa NMB ijikite katika kutoa elimu kwa Watanzania juu ya umuhimu wa huduma hii mpya, Serikali haiwezi 'ku-cover' kila kitu ndio maana tunasisitiza nguvu za Wadau hususani Taasisi za fedha katika kuwaunganisha Watanzania na huduma Jumuishi za fedha, zaidi niwapongeze NMB kwa kuwapa uhuru Watumiaji wa NMB Jiwekee wa kuchagua asilimia za kujitunzia kutokana na matumizi ya fedha zilizo kwenye akaunti zao" —— Ndejembi. #MillardAyoUPDATES
Like
Love
Yay
Angry
9
6 Comments 0 Shares 371 Views