Zelensky asema Putin ameanzisha vita ya tatu ya Dunia.
Volodymyr Zelensky ametoa kauli nzito akidai kuwa Vladimir Putin tayari ameanzisha Vita ya tatu ya Dunia, akisisitiza kuwa suluhisho pekee ni kuiwekea Urusi shinikizo kali kijeshi na kiuchumi ili kuizuia isisambaze zaidi mgogoro huo.
Katika mahojiano aliyofanya na BBC Mjini Kyiv, Kiongozi huyo wa Ukraine alieleza kuwa nchi yake haitaanguka mikononi mwa Urusi, bali itaibuka mshindi mwishoni mwa vita. Alisisitiza kuwa Ukraine haiwezi kutoa ardhi yake kama gharama ya amani, hasa ikizingatiwa kuwa majeshi ya Urusi hayajafanikiwa kuiteka kikamilifu licha ya kupeleka wanajeshi wengi vitani.
“Nafikiri Putin tayari ameanzisha Vita ya Tatu ya Dunia. Swali si tu kwamba ameianzisha, bali ni wapi anaweza kufika na namna gani dunia inaweza kumzuia,” alisema Zelensky.
Aliongeza kuwa Urusi inalenga kubadili mfumo wa kimataifa na kuwalazimisha watu kuishi katika mfumo ambao hawajauchagua wenyewe.
Akizungumzia pendekezo la Urusi la kutaka Ukraine ikabidhi takribani asilimia 20 ya maeneo yake, ikiwemo sehemu za Mkoa wa Donetsk na maeneo ya kusini, Zelensky alikataa wazo hilo vikali.
Kwa mujibu wake, suala hilo halihusu ardhi pekee, bali linahusu maisha ya Raia wa Ukraine na mustakabali wa taifa. Alisema kukubali masharti hayo kungekuwa sawa na kuwasaliti Wananchi na kuipokonya nchi hadhi yake.
Zelensky ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Moscow pamoja na kuimarisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Anaamini kuwa presha ya pamoja ndiyo njia pekee ya kuzuia mzozo huo kuenea zaidi na kuathiri usalama wa dunia kwa upana wake.
Kauli yake inakuja wakati mapigano kati ya Ukraine na Urusi yakiendelea katika maeneo kadhaa ya mashariki na kusini mwa nchi hiyo, huku hali ya kisiasa na kiusalama ikiendelea kuwa tete katika ukanda wa Ulaya Mashariki.
Toa maoni yako
#Habari

0 Comments
0 Shares
21 Views