Upgrade to Pro

Shindano linalofanyika kila mwaka liitwalo ‘Space-out’ Nchini Korea Kusini hutumika kusaka aliyekuwa bora kwenye sekta ya ‘kukaa tu bila kufanya kitu chochote’ ambapo Mshiriki haruhusiwi kusinzia, kuangalia simu yake au kuzungumza kwa dakika 90.

Unaambiwa hadi mapigo ya moyo ya Washiriki hufuatiliwa kwa makini huku Watazamaji wakipewa nafasi ya kuwapigia kura Washiriki 10 wanaowapenda ambapo yeyote aliye na mapigo ya moyo yaliyotulia zaidi kati ya hao 10 anatunukiwa kombe.

Zaidi ya Watu 4,000 waliomba kushiriki katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Serikali ya jiji la Seoul ambapo Washiriki 117 waliochaguliwa walikuwa kwenye rika la kuanzia mtoto wa darasa la pili hadi watu wenye umri wa miaka 60.

Tangu shindano la kwanza la ‘Space-out’ lifanyike jijini Seoul mwaka 2014 umaarufu wake umezidi kuwa mkubwa zaidi kimataifa ambako Miji mbalimbali kama vile Beijing nchini China, Rotterdam Uholanzi, Taipei, Hong Kong na Tokyo, Japan yamefanya shindano hilo. #MillardAyoUPDATES
Shindano linalofanyika kila mwaka liitwalo ‘Space-out’ Nchini Korea Kusini hutumika kusaka aliyekuwa bora kwenye sekta ya ‘kukaa tu bila kufanya kitu chochote’ ambapo Mshiriki haruhusiwi kusinzia, kuangalia simu yake au kuzungumza kwa dakika 90. Unaambiwa hadi mapigo ya moyo ya Washiriki hufuatiliwa kwa makini huku Watazamaji wakipewa nafasi ya kuwapigia kura Washiriki 10 wanaowapenda ambapo yeyote aliye na mapigo ya moyo yaliyotulia zaidi kati ya hao 10 anatunukiwa kombe. Zaidi ya Watu 4,000 waliomba kushiriki katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Serikali ya jiji la Seoul ambapo Washiriki 117 waliochaguliwa walikuwa kwenye rika la kuanzia mtoto wa darasa la pili hadi watu wenye umri wa miaka 60. Tangu shindano la kwanza la ‘Space-out’ lifanyike jijini Seoul mwaka 2014 umaarufu wake umezidi kuwa mkubwa zaidi kimataifa ambako Miji mbalimbali kama vile Beijing nchini China, Rotterdam Uholanzi, Taipei, Hong Kong na Tokyo, Japan yamefanya shindano hilo. #MillardAyoUPDATES
Like
Love
Haha
Wow
14
4 Comments ·570 Views