Upgrade to Pro

  • NI KWELI YANGA IMEFUNGWA, LAKINI...

    Masaa yangu manne (4) mtandaoni nikipitia maoni ya wadau wa soka kuhusu matokeo ya @yangasc kufungwa mabao 2-0 na Al Hilal leo, yamenikumbusha Novemba 24, 2023 wakati Yanga hii hii ikifungwa mabao 3-0 na CR Belouizdad (ugenini).

    Maoni hayo ya wadau yakanipeleka Disemba 2, 2023 wakati Yanga ikilazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Al Ahly (nyumbani), yote hayo kwenye hatua ya makundi ya michuano hii hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Mnakumbuka kilichofuata baada ya hapo?.

    Yanga walimaliza hatua ya makundi wakiwa nafasi ya pili na wakafuzu hatua ya robo fainali ambako waliondolewa tu kwa mambo yasiyofaa kuyaelezea sana.

    Leo wameanza tena hatua ya makundi kwa kupoteza, ni matokeo mabaya kwa klabu na watanzania kwa ujumla....ila nadhani kuna umuhimu wa kuhifadhi baadhi ya maneno yetu. Football ina mambo yake na inapenda sana kuheshimiwa na watu wa rika zote, tusijimalize.

    #Kumbukeni, 'wakali' kutoka @ligikuu ya @nbc_tanzania hawaanguki jumla, wanajikwaa wanainuka haraka, safari inaendelea

    #LadhaZaLigiKuu
    NI KWELI YANGA IMEFUNGWA, LAKINI... Masaa yangu manne (4) mtandaoni nikipitia maoni ya wadau wa soka kuhusu matokeo ya @yangasc kufungwa mabao 2-0 na Al Hilal leo, yamenikumbusha Novemba 24, 2023 wakati Yanga hii hii ikifungwa mabao 3-0 na CR Belouizdad (ugenini). Maoni hayo ya wadau yakanipeleka Disemba 2, 2023 wakati Yanga ikilazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Al Ahly (nyumbani), yote hayo kwenye hatua ya makundi ya michuano hii hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mnakumbuka kilichofuata baada ya hapo?. Yanga walimaliza hatua ya makundi wakiwa nafasi ya pili na wakafuzu hatua ya robo fainali ambako waliondolewa tu kwa mambo yasiyofaa kuyaelezea sana. Leo wameanza tena hatua ya makundi kwa kupoteza, ni matokeo mabaya kwa klabu na watanzania kwa ujumla....ila nadhani kuna umuhimu wa kuhifadhi baadhi ya maneno yetu. Football ina mambo yake na inapenda sana kuheshimiwa na watu wa rika zote, tusijimalize. #Kumbukeni, 'wakali' kutoka @ligikuu ya @nbc_tanzania hawaanguki jumla, wanajikwaa wanainuka haraka, safari inaendelea 🔥 #LadhaZaLigiKuu
    Like
    Love
    4
    ·487 Views