Upgrade to Pro

  • My Sister! Are you Under a Spell?.

    Naona wadada wengi ambao hawajaolewa, wazuri na wengine wakiwa na careers zao nzuri tu wapo kwenye mahusiano ya hovyo kupata kutokea. Sijajua ni kwanini lakini nashangaa bado waking'ang'ania hali hiyo.

    Mwanaume anakupiga, lakini bado upo, anakusaliti mbele ya macho yako lakini bado umeng'ang'ana tu...anakuumiza hisia zako, anakuongelea vibaya, haku-support, hajawahi kukununulia hata nguo ya ndani na hakuheshimu lakini bado upo tu.

    Sehemu pekee anayokupeleka ni kitandani au Bar, hamjawahi kutembea pamoja maeneo ya wazi, sehemu mnayoonekana pamoja ni kwenye giza giza lakini bado unaona sawa tu.

    Anakwambia anaweka mahusiano yenu private, lakini wewe bado unajionyesha kwake na unamuacha ana-enjoy sehemu zako za siri za mwili wako mzuri.

    Nafikiri unahitaji semina binafsi...watu pekee wanaokufahamu kwa upande wake ni marafiki na binamu zake basi, mwanaume anaekutambulisha kwa marafiki tu sio wa kumuamini moja kwa moja..yeye hajali ni kwa kiasi gani hao watu wanamfahamu kwa kuwa obvious watamfichia siri yake tu.

    Umefungwa na nini..?
    Nani amekuroga...?

    Ngoja nikwambie kitu kuhusiana na sisi wanaume. Hatuna tofauti sana na yule mwajiriwa wa kawaida...mwajiriwa wa kawaida yuko radhi afanye chochote kile ilimradi mwisho wa mwezi alipwe mshahara..sawa na sisi: hufanya lolote lile ilimradi tupate sex.

    Ndio, hata kuwadanganyeni kuwa tutawaoa, hata kuonekana kwa wazazi wenu as long as you guarantee us a sex...sasa imagine unaolewa na mwanaume wa hivyo, unafikiri atakua mume bora? Unafikiri atakupa furaha? Au unafikiri atabadilika? Hilo sahau..unaloliona ndilo utakalolipata.

    My sister, unatakiwa ujue thamani yako. Hata siku moja usijaribu kujishushia heshima na thamani yako ili tu umkamate mwanaume. Mwanaume ambae hawezi kukuheshimu na kuku-treat vizuri hakustahili hata kidogo.

    Ni bora uwe single, ukijigeuza huku na huku kitandani pekeyako kuhangaika na network ya Tigo kuliko kugeuzwa geuzwa kitandani na mwanaume ambae hastahili kupewa hiyo asali.

    Kamwe usiuze utu wako kwa minajili kwamba na wewe ujiite "am in a relationship"... hapana dada yangu hayo sio mahusiano, hizo ni personal benefits na tena anafaidi kweli, maana kila anapokuhitaji anakupata na unampa tu, anakuchafua na baada ya hapo maumivu tu kwa upande wako ukitarajia atabadilika na kuja kukuoa.

    My sister, hold yourself in so high esteem kiasi ya kwamba hata ukipita katikati ya kundi la wanaume, hakuna hata mmoja atainua kidole chake na kusema kwamba "nimeshakula ile mambo".

    Jiheshimu na heshimu hisia na mwili wako, hilo tunda anastahili mume wako tu, litunze ili usije ukampa likiwa limeliwa vya kutosha na limechacha...It's starts with you, if you don't know your value, you will be as common as a coin... Know your value and never be demeaned by anyone.

    Najua wanaume hawataipenda hii, ila muda mwingine lazima tuwaelimishe hawa dada zetu, ndio walezi wa kizazi kijacho.

    #KnowYourValueAndAct
    #MarriageUnderGodFoundation
    #MarriageIsBeautifu
    My Sister! Are you Under a Spell?. Naona wadada wengi ambao hawajaolewa, wazuri na wengine wakiwa na careers zao nzuri tu wapo kwenye mahusiano ya hovyo kupata kutokea. Sijajua ni kwanini lakini nashangaa bado waking'ang'ania hali hiyo. Mwanaume anakupiga, lakini bado upo, anakusaliti mbele ya macho yako lakini bado umeng'ang'ana tu...anakuumiza hisia zako, anakuongelea vibaya, haku-support, hajawahi kukununulia hata nguo ya ndani na hakuheshimu lakini bado upo tu. Sehemu pekee anayokupeleka ni kitandani au Bar, hamjawahi kutembea pamoja maeneo ya wazi, sehemu mnayoonekana pamoja ni kwenye giza giza lakini bado unaona sawa tu. Anakwambia anaweka mahusiano yenu private, lakini wewe bado unajionyesha kwake na unamuacha ana-enjoy sehemu zako za siri za mwili wako mzuri. Nafikiri unahitaji semina binafsi...watu pekee wanaokufahamu kwa upande wake ni marafiki na binamu zake basi, mwanaume anaekutambulisha kwa marafiki tu sio wa kumuamini moja kwa moja..yeye hajali ni kwa kiasi gani hao watu wanamfahamu kwa kuwa obvious watamfichia siri yake tu. Umefungwa na nini..? Nani amekuroga...? Ngoja nikwambie kitu kuhusiana na sisi wanaume. Hatuna tofauti sana na yule mwajiriwa wa kawaida...mwajiriwa wa kawaida yuko radhi afanye chochote kile ilimradi mwisho wa mwezi alipwe mshahara..sawa na sisi: hufanya lolote lile ilimradi tupate sex. Ndio, hata kuwadanganyeni kuwa tutawaoa, hata kuonekana kwa wazazi wenu as long as you guarantee us a sex...sasa imagine unaolewa na mwanaume wa hivyo, unafikiri atakua mume bora? Unafikiri atakupa furaha? Au unafikiri atabadilika? Hilo sahau..unaloliona ndilo utakalolipata. My sister, unatakiwa ujue thamani yako. Hata siku moja usijaribu kujishushia heshima na thamani yako ili tu umkamate mwanaume. Mwanaume ambae hawezi kukuheshimu na kuku-treat vizuri hakustahili hata kidogo. Ni bora uwe single, ukijigeuza huku na huku kitandani pekeyako kuhangaika na network ya Tigo kuliko kugeuzwa geuzwa kitandani na mwanaume ambae hastahili kupewa hiyo asali. Kamwe usiuze utu wako kwa minajili kwamba na wewe ujiite "am in a relationship"... hapana dada yangu hayo sio mahusiano, hizo ni personal benefits na tena anafaidi kweli, maana kila anapokuhitaji anakupata na unampa tu, anakuchafua na baada ya hapo maumivu tu kwa upande wako ukitarajia atabadilika na kuja kukuoa. My sister, hold yourself in so high esteem kiasi ya kwamba hata ukipita katikati ya kundi la wanaume, hakuna hata mmoja atainua kidole chake na kusema kwamba "nimeshakula ile mambo". Jiheshimu na heshimu hisia na mwili wako, hilo tunda anastahili mume wako tu, litunze ili usije ukampa likiwa limeliwa vya kutosha na limechacha...It's starts with you, if you don't know your value, you will be as common as a coin... Know your value and never be demeaned by anyone. Najua wanaume hawataipenda hii, ila muda mwingine lazima tuwaelimishe hawa dada zetu, ndio walezi wa kizazi kijacho. #KnowYourValueAndAct #MarriageUnderGodFoundation #MarriageIsBeautifu
    ·728 Views