#PART11
Baada ya Ntaganda kupelekwa The Heague, M23 iliongozwa na Sultan Makenga, Mtutsi wa Rutshuru huko Kivu Kaskazini. Mwaka 1990 Makenga akiwa na miaka 17 tu alienda Rwanda kujiunga na kikundi cha waasi RPF kilichokuwa kinaongozwa na Jenerali Fredy Rwigyema. Sultan Makenga akiwa askari wa RPF alipigana msituni dhidi ya serikali ya kihutu ya Juvenile Habyarimana.
Baada RPF ilishika dola, Askari wote wa RPF waliingizwa katika jeshi la Rwanda akiwemo Sultan Makenga. Alihudumu katika jeshi hilo kwa muda mrefu hadi kufikia cheo cha Kanali kabla ya kurudi "nyumbani" Congo, kujiunga na kikundi cha waasi cha CNDP. Baada ya mkataba wa amani wa March 23, 2009 Sultan Makenga alikuwa miongoni mwa askari 600 wa CNDP waliokataa kujiunga na jeshi la Congo (FARDC).
Mwaka 2012 Bosco Ntaganda alipojitoa kwenye jeshi la Congo na kuunga kikundi cha waasi cha M23, Sultan Makenga alikua wa kwanza kujiunga. Baada ya Ntaganda kujisalimisha, Makenga akapewa uongozi wa M23. Akaongoza kuanzia 2013 hadi 2016 alipotoweka ghafla. Haijulikani alipo, japo inasemekana alienda Rwanda na hakurudi tena.
Baada ya Makenga kutoweka katika mazingira ya "kutatanisha" M23 ikawa na viongozi ambao hawakuwa mashuhuri sana hadi 2022 ilipompata Corneille Nangaa. Huyu alikua Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Congo (CENI) na ndiye aliyemtangaza Tshikeshedi kuwa mshindi wa kiti cha Urais wa Congo kwenye uchaguzi wa December 30 mwaka 2018.
Katika mambo yanayoshangaza na kufanya vita ya Congo kuonekana ngumu, ni jinsi Nangaa alivyotoka kuwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, hadi kuanzisha coalition ya vikundi vya waasi, Congo River Alliance (CRA) kikiwemo M23. Jenerali Nangaa ndiye aliyeongoza M23 kuutwaa mji wa Goma January 2025, na kuyafurusha majeshi ya serikali. Nangaa ametangaza nia ya kumuondoa madarakani Rais Tshisekedi, ambaye mwaka 2018 ni Nangaa huyohuyo aliyemtangaza Tshikeshedi kuwa Rais.
August 2024 Mahakama ya kijeshi mjini Kinshasa ilimhukumu Nangaa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kosa la uhaini. Hukumu hiyo ilitolewa bila yeye kuwepo mahakamani (death sentence in absentia). Nangaa amesema ikiwa M23 itashika dola, wale waliomhukumu ndio watanyongwa kwa niaba yake.!
(Malisa GJ)