Ramadhani na Kwaresma: Msimu wa tafakari kwa Waumini Duniani.
Kwa sasa, Waumini wa dini mbili kubwa duniani wanaishi katika kipindi muhimu cha kiroho, Waislamu wako ndani ya mfungo wa Ramadhani huku Wakristo wakitekeleza Kwaresma. Hiki ni kipindi ambacho kinahusisha kujinyima, kutafakari na kujisafisha kiroho.
Kwaresma ni nini?
Kwaresma ni kipindi cha siku 40 kwa Wakristo, kinachoanza rasmi Jumatano ya Majivu na kumalizika Jumapili ya Pasaka. Hata hivyo, Wakristo hawafungi siku za Jumapili katika kipindi hiki.
Katika kipindi hiki, Waumini wanahimizwa kufanya toba, kujitathmini na kujizuia na matendo mabaya. Kufunga ni wajibu kwa baadhi ya siku maalum pekee.
“Kufunga ni lazima tu kwa waumini siku ya Jumatano ya Majivu na Ijumaa Kuu.”
Wanaofunga katika siku hizo huruhusiwa kula mlo mmoja kwa siku.
Ramadhani ni nini?
Kwa upande wa Uislamu, Ramadhani ni mwezi mtakatifu wa kufunga ambao hudumu kwa siku 29 au 30 kulingana na mwandamo wa mwezi katika kalenda ya Kiislamu.
Kufunga katika Ramadhani ni nguzo ya nne kati ya nguzo tano za Uislamu.
“Nguzo nyingine ni kukiri Mungu ni mmoja, kusali mara tano kwa siku, kutoa zaka kwa mwenye uwezo na kuhiji katika Mji mtakatifu wa Makka angalau mara moja katika maisha.”
Katika mwezi huu, Waislamu huanza siku yao kwa kula kabla ya alfajiri, mlo unaojulikana kama daku.
“Waislamu hula chakula cha mwisho kabla jua kuchomoza, kinachoitwa daku.”
Kuanzia alfajiri hadi machweo: “Wakati wa mchana, hawatakiwi kula au kunywa chochote au kuvuta sigara au tumbaku pamoja na kuzuiwa kunywa maji au kufanya ngono.”
Saumu hufunguliwa jioni kwa mlo uitwao futari.
Msamaha wa Kufunga
Sio kila Muislamu analazimika kufunga. Wapo waliosamehewa kwa sababu za kiafya au hali maalum za maisha.
“Baadhi ya Waislamu wamesamehewa kufunga, mfano Wanawake wajawazito au wanaonyonyesha na Wanawake walio katika hedhi.”
“Wengine ni Wagonjwa au ambao afya zao zinaweza kuathiriwa na kufunga na watu wanaosafiri.”
Katika hali hizi: “Watatakiwa kulipa funga zao au kulisha masikini.”
Tofauti kuu lakini lengo lilelile
Ingawa Ramadhani na Kwaresma zinatofautiana katika utekelezaji, zote zina msingi mmoja kujinyima, toba, na kujenga ukaribu na Mungu.
Ni kipindi kinachowakumbusha Waumini umuhimu wa nidhamu ya kiroho, huruma kwa wahitaji, na maisha yenye maadili.
Toa maoni yako
#Habari

0 Yorumlar
0 hisse senetleri
3 Views