• Cristiano Ronaldo arejea Uwanjani baada ya mvutano Al Nassr na Saudi PIF.

    Ripoti zinazonukuliwa kutoka vyanzo mbalimbali nchini Saudi Arabia zinaeleza kuwa Staa wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, amesitisha rasmi mgomo wake na yuko tayari kurejea Uwanjani kuitumikia klabu ya Al Nassr. Hatua hiyo inakuja baada ya Wafanyakazi wote wa klabu hiyo kulipwa mishahara yao pamoja na posho walizokuwa wakidai kwa muda.

    Kwa mujibu wa taarifa hizo, mgomo wa Ronaldo ulihusishwa na mvutano uliokuwepo kati yake na Tume ya Uwekezaji ya Saudi Arabia, maarufu kama Saudi PIF. Inadaiwa kuwa Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno alikuwa akilalamikia kile kilichoelezwa kuwa ni upendeleo kwa baadhi ya klabu, hususan katika masuala ya usajili wa Wachezaji na uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye timu fulani.

    Zaidi ya hayo, chanzo cha mgomo huo hakikujikita tu kwenye masuala ya usajili aliyoyaona kuwa hayaridhishi, bali pia katika kuhakikisha haki za Wafanyakazi wa klabu zinalindwa. Ronaldo alisisitiza kuwa Wafanyakazi wote, hasa wale wa ngazi za chini, walipaswa kulipwa stahiki zao kwa wakati na kwa ukamilifu.

    Hatua ya kulipwa kwa Wafanyakazi wote imeonekana kufungua ukurasa mpya ndani ya Al Nassr, na kurejesha hali ya utulivu kambini. Mashabiki wengi sasa wanasubiri kwa hamu kumuona Ronaldo akirejea Uwanjani, wakitumaini kuwa tukio hilo litaleta mabadiliko chanya ndani ya klabu hiyo na kwenye ligi kwa ujumla.

    Kwa kurejea kwake, Ronaldo anaonekana si tu kama Mchezaji mkubwa Uwanjani, bali pia kama sauti ya Wafanyakazi na mdau anayeonyesha kujali masuala ya haki na usawa ndani ya soka la kulipwa.

    Toa maoni yako
    #Tarifazauwakika
    Cristiano Ronaldo arejea Uwanjani baada ya mvutano Al Nassr na Saudi PIF. Ripoti zinazonukuliwa kutoka vyanzo mbalimbali nchini Saudi Arabia zinaeleza kuwa Staa wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, amesitisha rasmi mgomo wake na yuko tayari kurejea Uwanjani kuitumikia klabu ya Al Nassr. Hatua hiyo inakuja baada ya Wafanyakazi wote wa klabu hiyo kulipwa mishahara yao pamoja na posho walizokuwa wakidai kwa muda. Kwa mujibu wa taarifa hizo, mgomo wa Ronaldo ulihusishwa na mvutano uliokuwepo kati yake na Tume ya Uwekezaji ya Saudi Arabia, maarufu kama Saudi PIF. Inadaiwa kuwa Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno alikuwa akilalamikia kile kilichoelezwa kuwa ni upendeleo kwa baadhi ya klabu, hususan katika masuala ya usajili wa Wachezaji na uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye timu fulani. Zaidi ya hayo, chanzo cha mgomo huo hakikujikita tu kwenye masuala ya usajili aliyoyaona kuwa hayaridhishi, bali pia katika kuhakikisha haki za Wafanyakazi wa klabu zinalindwa. Ronaldo alisisitiza kuwa Wafanyakazi wote, hasa wale wa ngazi za chini, walipaswa kulipwa stahiki zao kwa wakati na kwa ukamilifu. Hatua ya kulipwa kwa Wafanyakazi wote imeonekana kufungua ukurasa mpya ndani ya Al Nassr, na kurejesha hali ya utulivu kambini. Mashabiki wengi sasa wanasubiri kwa hamu kumuona Ronaldo akirejea Uwanjani, wakitumaini kuwa tukio hilo litaleta mabadiliko chanya ndani ya klabu hiyo na kwenye ligi kwa ujumla. Kwa kurejea kwake, Ronaldo anaonekana si tu kama Mchezaji mkubwa Uwanjani, bali pia kama sauti ya Wafanyakazi na mdau anayeonyesha kujali masuala ya haki na usawa ndani ya soka la kulipwa. Toa maoni yako #Tarifazauwakika
    0 Commentaires 0 Parts 81 Vue