Mise à niveau vers Pro

  • TAFAKARI :

    Kulikuwa na Mwalimu mmoja aliyezoea kumchapa viboko mwanafunzi mmoja mchelewaji shuleni, Mwanafunzi huyo alikuwa ni mtoto wa kimasikini pia mpole sana na mwenye huruma na alikuwa akiishi eneo lenye umbali kiasi mpaka kufika shuleni, kwa hivyo Mwanafunzi yule takriban miaka 3 alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza kila siku. Kwa hiyo siku ambazo Mwalimu huyo alikuwa na kipindi cha kwanza darasani kwao Mwanafunzi huyo alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu, jambo la kushangaza wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana kabisa shuleni!

    Wiki ililoyofuata yule Mwanafunzi alifika shuleni mapema kabla ya Mwanafunzi mwingine yeyote. Mwalimu yule alishangaa sana alipomwona alifurahi sana alipoingia Darasani alimwita na kumsifia sana mbele ya Darasa kabla ya kumuuliza jambo lo lote.

    "Mwalimu akamwambia yule Mwanafunzi hebu simama akatii amri ya Mwalimu wake akasimama, Mwalimu akawaambia wanafunzi wenzake wampigie makofi kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika shuleni. Mwalim akasema kumbe zile fimbo ninazomchapa zimesaidia sana eeeeenh?"

    Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka na kumdhihaki. Baada ya dakika kadhaa yule Mwanafunzi akamwomba Mwalimu ampe nafasi aseme jambo kidogo ili wapate kujua ni nini anataka kuwaelezea, Mwalimu akamruhusu huku akiwa amemkodolea macho haya tuambie.

    "Kwanza akawaomba radhi kwa kusema Mwalimu pamoja na wanafunzi wenzangu nyote kwa jumla, nakuombeni unisamehe iwapo nilikuwa nikiwaudhi kwa sababu siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shuleni nilikuwa namuuguza Mama yangu mzazi. Baba yangu alifariki kabla sijazaliwa, kwa hivyo sikujaaliwa kumuona nililelewa na Mama yangu tu naye alitengwa na ndugu kutokana na ufukara kwa hakika unyonge ni kitu kibaya sana simjui ndugu ye yote, Mama yangu alipopatwa na Maradhi tulimpeleka hospitalini Mimi ni jirani zetu lakini maradhi yake hayakuonekana. Akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na Dawa za kutuliza maumivu tu." Kwa sababu hatukuwa na pesa sikuweza kumpeleka popote kwa vipimo zaidi."

    Mara akafuta machozi yaliyoanza kumtiririka kwa wingi mashavuni, na akasema kwa unyonge ewe Mwalimu wangu pamoja na wanafunzi wenzangu.

    "Kwa hivyo kila siku nilitakiwa kufanya usafi wa nyumba kuchota maji, kumsafisha Mama yangu pamoja na kumstiri, kumwandalia chakula chake kabla ya kuondoka kuja hapa shuleni na kazi zingine zote." Akanyamaza kidogo kwa uchungu."

    "Na sikitika kusema leo hii nimewahi kuja Shuleni kwa sababu Mama yangu alifariki wiki moja iliyopita ambayo sikuonekana shuleni nilikuwa nikimalizia msiba wa Mama yangu. Yote ndio mipango yake Mwenyezi Mungu kwa hiyo kilichokuwa kinanichelewesha kimeondoka ndio maana leo nimewahi kufika mapema shuleni."

    Hakuweza kuongea tena kutokana na uchungu, akakaa taratibu kitini huku akilia kwa kwikwi

    Hatimae Darasa zima nalo liligeuka mahala pa msiba kila mmoja akilia pamoja na Mwalimu wao, huku wakimpa pole na kumuomba msamaha kwa jinsi walivyokuwa wakimdhihaki. Naye akawaambia nimekusameheni kwa moyo safi kabisa.

    WITO:

    Msiharakishe kuadhibu wenzenu bila kuwapa nafasi ya kujieleza, sababu huwezi kujua jambo gani linalowasibu bila kuwapa fursa ya kujielezea au kukwambia ili upatikane ufumbuzi wa tatizo.

    Unapo muona mwenzako hayupo sawa kifikra, kiafya, au jambo lo lote muulize kwanza kabla ya kuanza kumshutumu.

    Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujalie tuwe ni wenye kupendana, kuuliza na kusaidiana kwa kila jambo.
    TAFAKARI : Kulikuwa na Mwalimu mmoja aliyezoea kumchapa viboko mwanafunzi mmoja mchelewaji shuleni, Mwanafunzi huyo alikuwa ni mtoto wa kimasikini pia mpole sana na mwenye huruma na alikuwa akiishi eneo lenye umbali kiasi mpaka kufika shuleni, kwa hivyo Mwanafunzi yule takriban miaka 3 alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza kila siku. Kwa hiyo siku ambazo Mwalimu huyo alikuwa na kipindi cha kwanza darasani kwao Mwanafunzi huyo alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu, jambo la kushangaza wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana kabisa shuleni! Wiki ililoyofuata yule Mwanafunzi alifika shuleni mapema kabla ya Mwanafunzi mwingine yeyote. Mwalimu yule alishangaa sana alipomwona alifurahi sana alipoingia Darasani alimwita na kumsifia sana mbele ya Darasa kabla ya kumuuliza jambo lo lote. "Mwalimu akamwambia yule Mwanafunzi hebu simama akatii amri ya Mwalimu wake akasimama, Mwalimu akawaambia wanafunzi wenzake wampigie makofi kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika shuleni. Mwalim akasema kumbe zile fimbo ninazomchapa zimesaidia sana eeeeenh?" Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka na kumdhihaki. Baada ya dakika kadhaa yule Mwanafunzi akamwomba Mwalimu ampe nafasi aseme jambo kidogo ili wapate kujua ni nini anataka kuwaelezea, Mwalimu akamruhusu huku akiwa amemkodolea macho haya tuambie. "Kwanza akawaomba radhi kwa kusema Mwalimu pamoja na wanafunzi wenzangu nyote kwa jumla, nakuombeni unisamehe iwapo nilikuwa nikiwaudhi kwa sababu siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shuleni nilikuwa namuuguza Mama yangu mzazi. Baba yangu alifariki kabla sijazaliwa, kwa hivyo sikujaaliwa kumuona nililelewa na Mama yangu tu naye alitengwa na ndugu kutokana na ufukara kwa hakika unyonge ni kitu kibaya sana simjui ndugu ye yote, Mama yangu alipopatwa na Maradhi tulimpeleka hospitalini Mimi ni jirani zetu lakini maradhi yake hayakuonekana. Akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na Dawa za kutuliza maumivu tu." Kwa sababu hatukuwa na pesa sikuweza kumpeleka popote kwa vipimo zaidi." Mara akafuta machozi yaliyoanza kumtiririka kwa wingi mashavuni, na akasema kwa unyonge ewe Mwalimu wangu pamoja na wanafunzi wenzangu. "Kwa hivyo kila siku nilitakiwa kufanya usafi wa nyumba kuchota maji, kumsafisha Mama yangu pamoja na kumstiri, kumwandalia chakula chake kabla ya kuondoka kuja hapa shuleni na kazi zingine zote." Akanyamaza kidogo kwa uchungu." "Na sikitika kusema leo hii nimewahi kuja Shuleni kwa sababu Mama yangu alifariki wiki moja iliyopita ambayo sikuonekana shuleni nilikuwa nikimalizia msiba wa Mama yangu. Yote ndio mipango yake Mwenyezi Mungu kwa hiyo kilichokuwa kinanichelewesha kimeondoka ndio maana leo nimewahi kufika mapema shuleni." Hakuweza kuongea tena kutokana na uchungu, akakaa taratibu kitini huku akilia kwa kwikwi Hatimae Darasa zima nalo liligeuka mahala pa msiba kila mmoja akilia pamoja na Mwalimu wao, huku wakimpa pole na kumuomba msamaha kwa jinsi walivyokuwa wakimdhihaki. Naye akawaambia nimekusameheni kwa moyo safi kabisa. WITO: Msiharakishe kuadhibu wenzenu bila kuwapa nafasi ya kujieleza, sababu huwezi kujua jambo gani linalowasibu bila kuwapa fursa ya kujielezea au kukwambia ili upatikane ufumbuzi wa tatizo. Unapo muona mwenzako hayupo sawa kifikra, kiafya, au jambo lo lote muulize kwanza kabla ya kuanza kumshutumu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujalie tuwe ni wenye kupendana, kuuliza na kusaidiana kwa kila jambo.
    Like
    3
    ·706 Vue
  • Nikicheki muda Ni saa 4 usiku Napiga Dua namshukuru mungu
    Kwa kunilinda Hii Siku na Wenye #Bifu
    Naomba Tena Atulinde huu usiku #Mrefu
    Mungu Mimi kwako si #Mkamilifu
    Najua nakosea Nina mengi #Madhaifu
    Kwa wema wako nioshe niwe #Nadhifu
    Nakusifu kwa mdomo maana hujaniumba #BuBu
    Wape Tumaini wenye matatizo yanayo #Wasibu
    Wagonjwa mahospitali wema wako #Ukawatibu
    Wategemee Dua na sio sangoma Wala #Chifu
    Waombewe na watumishi mashekh wakina #Sharifu
    Wasirogane kwa kuvunjiana Nazi na #Madafu
    Nashukuru kwa hii pumzi inayoingia kwenye #Mapafu
    Nitimize sakramenti takwa Mimi nilie #Mkristu
    Niepushe Na zinaa niogope kufungua #Zipu
    Niepushe Na tamaa nisipende Sana #Chipu
    Niwe mwema ndugu zangu nisiwachezee #Rafu
    Niiheshimu ndoa nilale chumbani niogee #Bafu
    Kesho nijalie riziki yangu niingojee kwa #Safu
    Nisishawishike na ulevi nikaja lala #Club
    Ee mungu tulinde Huu usiku na kila #Tabu
    Dua zetu zipokee kwako ndo liliko #Jawabu
    Nikicheki muda Ni saa 4 usiku Napiga Dua namshukuru mungu🎤 Kwa kunilinda Hii Siku na Wenye #Bifu Naomba Tena Atulinde huu usiku #Mrefu Mungu Mimi kwako si #Mkamilifu Najua nakosea Nina mengi #Madhaifu Kwa wema wako nioshe niwe #Nadhifu Nakusifu kwa mdomo maana hujaniumba #BuBu Wape Tumaini wenye matatizo yanayo #Wasibu Wagonjwa mahospitali wema wako #Ukawatibu Wategemee Dua na sio sangoma Wala #Chifu Waombewe na watumishi mashekh wakina #Sharifu Wasirogane kwa kuvunjiana Nazi na #Madafu Nashukuru kwa hii pumzi inayoingia kwenye #Mapafu Nitimize sakramenti takwa Mimi nilie #Mkristu Niepushe Na zinaa niogope kufungua #Zipu Niepushe Na tamaa nisipende Sana #Chipu Niwe mwema ndugu zangu nisiwachezee #Rafu Niiheshimu ndoa nilale chumbani niogee #Bafu Kesho nijalie riziki yangu niingojee kwa #Safu Nisishawishike na ulevi nikaja lala #Club Ee mungu tulinde Huu usiku na kila #Tabu Dua zetu zipokee kwako ndo liliko #Jawabu
    ·1KB Vue