• UGOMVI WA PALESTINA NA ISRAEL NI WA MAPACHA WAWILI TOKA WAKIWA TUMBONI KABLA YA KUZALIWA.

    Nini sababu ya ugomvi ? Siyo tatizo la kugombania ardhi wala kugombania mji wa Yerusalem kunakosababisha ugomvi kati ya mataifa haya mawili ni kwamba kila taifa halitaki kutambulika kwa taifa jingine kama taifa huru.

    Hii inamaanisha kwamba hata kama taifa la Palestina litahamia katika bara jingine au Israel kuhamia bara jingine bado ugomvi na vita ingeendelea kati ya mataifa haya mawili ,ugomvi kati ya mataifa haya unakwenda mbali zaidi tangu watoto wawili mapacha wakiwa tumboni kabla ya kuzaliwa.

    Katika kitabu cha (Mwanzo 25:22) inasomeka;"Bwana akamwambia ,Mataifa mawili yamo tumboni mwako ,Na Kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako, Kabila moja litakuwa hodari Kuliko la pili na mkubwa atamtumikia mdogo."

    Alizaliwa kwanza Esau ambaye baadae aliitwa Edom kisha akafuatia Yakobo ambaye baadae aliitwa Israel. Wakati Edom ni taifa la Palestina, Israel ni taifa la Israeli, hakuna ubishi kwamba Israel ni hodari zaidi ya Palestina.

    Miaka ya 50 iliyopita, yaani mwaka 1967 ,kulitokea vita kati ya Israel na mataifa jirani zake, Vita hii ilipiganwa kwa siku 6 tu(Juni 5---Juni 10,1967) lakini madhara yake yapo mpaka leo ,ilikuwa ni miaka michache kupita baada ya wa--NAZI wa Hitler,kuwaua wayahudi milioni 6 ,ndoto ya kuanzishwa kwa Taifa la Israeli kama ilivyotabiriwa kwenye biblia ilitimia.

    Mwishoni mwa mwaka 1948 ikiwa ni miaka 3 tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia ,Mataifa ya kiarabu majirani mwa Israel yaliivamia Israel yakijaribu kuliangamiza Taifa changa ambalo muda mfupi tu lilikuwa limetangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa Taifa huru, lakini hayakufanikiwa.

    Jeshi la misri lilipigwa lakini askari waliokuwa kwenye eneo dogo linalojulikana kama Falluja walikataa kusalimu amri ,kundi la askari wa Misri na Israeli walipambana vikali ,Miongoni mwa askari Vijana waliokuwa kwenye kikosi cha jeshi la Israel alikuwa ni Yitzhak Rabin ambaye alikuwa na umri wa miaka 26 wakati huo, Pamoja na Meja Gamal Abdel Nasser wa jeshi la Misri aliyekuwa na miaka 30.

    Wapalestina wanauita mwaka 1948 kuwa ni "al--Nakba" yaani 'Janga' .Zaidi ya wapalestina 750,000 walifukuzwa kutoka kwenye eneo ambalo sasa linajulikana kama Taifa la Israel na hawakuruhusiwa kurudi tena mahali hapo.

    Mataifa ya Misri, Jordani, na Syria yaliungana pamoja kuishambulia Israel ambayo hata hivyo ndiyo kwanza ilikuwa imepewa hadhi ya kuwa taifa huru. Lakini kwasababu Mungu alikuwa amesema kwamba "Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili" ni wazi kuwa Israel ,likiwa taifa changa ,bado lilifanikiwa kuwashinda majirani zake tena ndani ya siku 6 tu.

    Ingawa vita kati ya Israel na Palestina ilianzia tumboni ,lakini vita nyingi hutengenezwa na wajenzi huru kwa faida yao, Februari 17 mwaka 1950 James Paul Warburg mwenye asili ya kiyahudi alihutubia Baraza la Senate la Marekani na kusema " Government creates a crisis for which the public demands a solution.
    That solution instigates the changes that the government initially wanted but which the people would have been unwilling to accept.

    It is order out of chaos !!! Worldwide chaos will lead to worldwide solutions which will establish the one world order " yaani; Serikali hutengeneza migogoro ambayo umma hutaka pawepo na suruhisho.
    Suruhisho hilo hulazimisha mabadiliko ambayo awali Serikali iliyataka lakini umma ulikuwa hauyataki, ni utaratibu unaopatikana Kutokana na machafuko !! Machafuko ya kidunia yataleta suruhisho la kidunia ambalo litaanzisha utaratibu mmoja wa ulimwengu.

    Katika hotuba yake inayojulikana kama "Urbi et Orbi ", Papa Francis alisema ;" Pepo za vita zinavuma katika ulimwengu wetu na maendeleo yanaendelea kusababisha mmomonyoko wa maadili na uharibifu wa mazingira " Urbi et Orbi ni maneno yanayomaanisha " To the city and to the world" yaani " kwenda kwa mji na kwenda kwa ulimwengu" kumaanisha kwamba hotuba za Papa Francis zinakwenda kwa wakazi wa mji wa Vatican city na wakazi wa ulimwenguni kote.

    Tishio la silaha za nyuklia kutoka Korea kaskazini ,mgogoro wa peninsula ya Korea pamoja na mgogoro wa mji wa Yerusalem baada ya Rais Trump kutangaza kuwa Yerusalem ni mji Mkuu wa Israel na tangazo hilo kupingwa na Umoja wa Mataifa, ni pepo zinazoonyesha dalili ya kufumka kwa vita duniani kote.

    Katika hotuba hiyo papa Francis alipendekeza kutambuliwa kwa mataifa mawili yaani Israel na Palestina, kama suruhisho la mgogoro wa Mashariki ya kati pamoja na kutatua mgogoro wa Korea kaskazini kwa njia ya kidiplomasia.

    Itakumbukwa kwamba, Mwanasayansi mashuhuri aliyejulikana kama Albert Einstein alitoa tafsiri ya neno " Insanity" yaani " kuchanganyikiwa au uwendawazimu " akisema ;"wakati mtu anapojaribu kutumia kanuni ya zamani ambayo ilishindwa kwa wakati na wakati mwingine tena, akiamini kwamba ,kwa vyovyote atapata matokeo tofauti mtu huyo amechanganyikiwa au ana uwendawazimu.

    Israel, Palestina, Marekani na Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya miaka 50 wamekuwa wakijadili uwezekano wa kuleta suluhu kwa kuifanya Palestina kuwa Taifa huru pamoja na Israeli. Hata hivyo ,wapalestina wamekuwa wakijiondoa kwenye suruhisho hilo kwa sababu mpango huo unaifanya Israel iendelee kuwa Taifa huru ,wapalestina wamekuwa wakipinga wazo kwamba Israel ina haki ya kuwepo na kuishi kama Taifa.

    Lengo ni kuwafutilia mbali wayahudi wote, jambo ambalo hata Adolf Hitler alikuwa nalo lakini hakuweza ,kwa mujibu wa Mwanasayansi Albert Einstein " suruhisho la mataifa mawili ( two state solution) limeshindwa kufanya kazi na wale wanaoendelea kupendekeza suruhisho hilo, ama wamechanganyikiwa na ni wendawazimu au wanafanya kwa makusudi wakiwa wanafahamu matokeo yake.

    Raia wa mataifa yote mawili wanamtambua Ibrahimu kama Baba wa Mataifa yao, Ibrahimu aliishi miaka 4000 iliyopita akisafiri Kwenye eneo la Taifa linalojulikana leo kama Iraqi, na akafika Kwenye eneo la taifa linalojulikana leo kama Israeli.

    Ibrahimu aliahidiwa na Mungu Kwamba atapata mtoto Katika uzee wake .Akiwa amesubiri utimilifu wa ahadi hii kwa muda mrefu bila kupata mtoto ,alimchukua kijakazi wake na akafanikiwa kuzaa naye mtoto aliyeitwa ishmail. Lakini mungu hakuwa amepanga kumpatia Ibrahim mtoto kwa njia hiyo, bado aliendelea kumhakikishia kwamba atapata mtoto kupitia kwa mkewe. Kwa sababu alikuwa na imani ,alifanikiwa kumpata mtoto aliyepewa jina la Isaka.

    Kisha Mungu akamuagiza kwenda kwenye mlima Moria, ili akamtoe kafara mtoto wake Isaka ambaye alikuwa amemsubiri Kwa muda mrefu. Huu mlima Moria upo wapi? Ingawa wakati wa siku za Ibrahimu ,miaka 2000KK ,eneo kubwa lilikuwa jangwa ,miaka 1000KK baadae Mfalme Daudi alijenga mji wa Yerusalem katika eneo hilo na mtoto wake aliyejulikana kama Mfalme Sulemani alijenga hekalu la kwanza kwenye eneo hilo la mlima Moria .

    Imeandikwa " ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya bwana huko Yerusalem ,juu ya mlima Moria ..." (2 Nyakati 3:1). Lakini kwa Ibrahimu Mungu anamwambia : " umchukue mwanao ,mwana wako wa pekee, umpendaye ,Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka, ..." ( Mzo. 22:2) Hivyo basi mji wa Yerusalem anajulikana kama nchi ya Moria au mlima wa Moria au mji wa Daudi mahali palepale alipoambiwa nabii Ibrahimu kwenda kutoa kafara ,ndipo Hapo hapo Mfalme Sulemani alipojenga hekalu la kumuabudia Mungu na kumtolea kafara za wanyama.

    Lakini zaidi ni katika mji wa Yerusalem ndipo yesu aliposulubiwa msalabani na hapo ndipo lilipo chimbuko la dini ya ukristo iliyoanzishwa kwa ujumla uzao wa Ibrahimu ndio chimbuko la dini kubwa tatu ,yaani uyahudi, uislamu ,na ukristo.

    Dini zingine zote zimetokana na dini hizi tatu ,Kutokana na ukweli huu ,wajenzi huru wamefanikiwa kuwashawishi viongozi wa dini zote na kuziunganisha kuwa dini moja. Ingawa majina ya dini hizi yanaendelea kutumika kiasi cha kuonekana kwamba hakuna tofauti ,lakini matunda ya dini hizi yanaonyesha wazi kuwa yanatokea kwenye mti mmoja.

    Katika mambo ya kiroho jina la dini ya mtu au dhehebu lake haliwezi kumfanya muumini afike mbinguni bali kitu muhimu ni matunda ya dini hiyo au dhehebu hilo. Kwa kujua hili mwanzilishi wa illuminati Dkt Adam Weishaupt aliandika akisema , The great strength of our order lies in its concealment " yaani nguvu kubwa ya Utaratibu wetu Iko katika kuficha na kufanya kazi zetu kwa siri kubwa " Hata huu muunganiko wa dini umefanywa kwa siri kubwa kiasi kwamba waumini wengi hawajui kinachoendelea.

    Weishaupt akaendelea kusema, " let it never appear in any place in its own name, but always covered by another name and another occupation " yaani; " hebu isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima ifanyike kwa jina lingine na kwa namna nyingine." ( Robin's Proofs of a Conspiracy, P. 195).
    UGOMVI WA PALESTINA NA ISRAEL NI WA MAPACHA WAWILI TOKA WAKIWA TUMBONI KABLA YA KUZALIWA. Nini sababu ya ugomvi ? Siyo tatizo la kugombania ardhi wala kugombania mji wa Yerusalem kunakosababisha ugomvi kati ya mataifa haya mawili ni kwamba kila taifa halitaki kutambulika kwa taifa jingine kama taifa huru. Hii inamaanisha kwamba hata kama taifa la Palestina litahamia katika bara jingine au Israel kuhamia bara jingine bado ugomvi na vita ingeendelea kati ya mataifa haya mawili ,ugomvi kati ya mataifa haya unakwenda mbali zaidi tangu watoto wawili mapacha wakiwa tumboni kabla ya kuzaliwa. Katika kitabu cha (Mwanzo 25:22) inasomeka;"Bwana akamwambia ,Mataifa mawili yamo tumboni mwako ,Na Kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako, Kabila moja litakuwa hodari Kuliko la pili na mkubwa atamtumikia mdogo." Alizaliwa kwanza Esau ambaye baadae aliitwa Edom kisha akafuatia Yakobo ambaye baadae aliitwa Israel. Wakati Edom ni taifa la Palestina, Israel ni taifa la Israeli, hakuna ubishi kwamba Israel ni hodari zaidi ya Palestina. Miaka ya 50 iliyopita, yaani mwaka 1967 ,kulitokea vita kati ya Israel na mataifa jirani zake, Vita hii ilipiganwa kwa siku 6 tu(Juni 5---Juni 10,1967) lakini madhara yake yapo mpaka leo ,ilikuwa ni miaka michache kupita baada ya wa--NAZI wa Hitler,kuwaua wayahudi milioni 6 ,ndoto ya kuanzishwa kwa Taifa la Israeli kama ilivyotabiriwa kwenye biblia ilitimia. Mwishoni mwa mwaka 1948 ikiwa ni miaka 3 tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia ,Mataifa ya kiarabu majirani mwa Israel yaliivamia Israel yakijaribu kuliangamiza Taifa changa ambalo muda mfupi tu lilikuwa limetangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa Taifa huru, lakini hayakufanikiwa. Jeshi la misri lilipigwa lakini askari waliokuwa kwenye eneo dogo linalojulikana kama Falluja walikataa kusalimu amri ,kundi la askari wa Misri na Israeli walipambana vikali ,Miongoni mwa askari Vijana waliokuwa kwenye kikosi cha jeshi la Israel alikuwa ni Yitzhak Rabin ambaye alikuwa na umri wa miaka 26 wakati huo, Pamoja na Meja Gamal Abdel Nasser wa jeshi la Misri aliyekuwa na miaka 30. Wapalestina wanauita mwaka 1948 kuwa ni "al--Nakba" yaani 'Janga' .Zaidi ya wapalestina 750,000 walifukuzwa kutoka kwenye eneo ambalo sasa linajulikana kama Taifa la Israel na hawakuruhusiwa kurudi tena mahali hapo. Mataifa ya Misri, Jordani, na Syria yaliungana pamoja kuishambulia Israel ambayo hata hivyo ndiyo kwanza ilikuwa imepewa hadhi ya kuwa taifa huru. Lakini kwasababu Mungu alikuwa amesema kwamba "Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili" ni wazi kuwa Israel ,likiwa taifa changa ,bado lilifanikiwa kuwashinda majirani zake tena ndani ya siku 6 tu. Ingawa vita kati ya Israel na Palestina ilianzia tumboni ,lakini vita nyingi hutengenezwa na wajenzi huru kwa faida yao, Februari 17 mwaka 1950 James Paul Warburg mwenye asili ya kiyahudi alihutubia Baraza la Senate la Marekani na kusema " Government creates a crisis for which the public demands a solution. That solution instigates the changes that the government initially wanted but which the people would have been unwilling to accept. It is order out of chaos !!! Worldwide chaos will lead to worldwide solutions which will establish the one world order " yaani; Serikali hutengeneza migogoro ambayo umma hutaka pawepo na suruhisho. Suruhisho hilo hulazimisha mabadiliko ambayo awali Serikali iliyataka lakini umma ulikuwa hauyataki, ni utaratibu unaopatikana Kutokana na machafuko !! Machafuko ya kidunia yataleta suruhisho la kidunia ambalo litaanzisha utaratibu mmoja wa ulimwengu. Katika hotuba yake inayojulikana kama "Urbi et Orbi ", Papa Francis alisema ;" Pepo za vita zinavuma katika ulimwengu wetu na maendeleo yanaendelea kusababisha mmomonyoko wa maadili na uharibifu wa mazingira " Urbi et Orbi ni maneno yanayomaanisha " To the city and to the world" yaani " kwenda kwa mji na kwenda kwa ulimwengu" kumaanisha kwamba hotuba za Papa Francis zinakwenda kwa wakazi wa mji wa Vatican city na wakazi wa ulimwenguni kote. Tishio la silaha za nyuklia kutoka Korea kaskazini ,mgogoro wa peninsula ya Korea pamoja na mgogoro wa mji wa Yerusalem baada ya Rais Trump kutangaza kuwa Yerusalem ni mji Mkuu wa Israel na tangazo hilo kupingwa na Umoja wa Mataifa, ni pepo zinazoonyesha dalili ya kufumka kwa vita duniani kote. Katika hotuba hiyo papa Francis alipendekeza kutambuliwa kwa mataifa mawili yaani Israel na Palestina, kama suruhisho la mgogoro wa Mashariki ya kati pamoja na kutatua mgogoro wa Korea kaskazini kwa njia ya kidiplomasia. Itakumbukwa kwamba, Mwanasayansi mashuhuri aliyejulikana kama Albert Einstein alitoa tafsiri ya neno " Insanity" yaani " kuchanganyikiwa au uwendawazimu " akisema ;"wakati mtu anapojaribu kutumia kanuni ya zamani ambayo ilishindwa kwa wakati na wakati mwingine tena, akiamini kwamba ,kwa vyovyote atapata matokeo tofauti mtu huyo amechanganyikiwa au ana uwendawazimu. Israel, Palestina, Marekani na Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya miaka 50 wamekuwa wakijadili uwezekano wa kuleta suluhu kwa kuifanya Palestina kuwa Taifa huru pamoja na Israeli. Hata hivyo ,wapalestina wamekuwa wakijiondoa kwenye suruhisho hilo kwa sababu mpango huo unaifanya Israel iendelee kuwa Taifa huru ,wapalestina wamekuwa wakipinga wazo kwamba Israel ina haki ya kuwepo na kuishi kama Taifa. Lengo ni kuwafutilia mbali wayahudi wote, jambo ambalo hata Adolf Hitler alikuwa nalo lakini hakuweza ,kwa mujibu wa Mwanasayansi Albert Einstein " suruhisho la mataifa mawili ( two state solution) limeshindwa kufanya kazi na wale wanaoendelea kupendekeza suruhisho hilo, ama wamechanganyikiwa na ni wendawazimu au wanafanya kwa makusudi wakiwa wanafahamu matokeo yake. Raia wa mataifa yote mawili wanamtambua Ibrahimu kama Baba wa Mataifa yao, Ibrahimu aliishi miaka 4000 iliyopita akisafiri Kwenye eneo la Taifa linalojulikana leo kama Iraqi, na akafika Kwenye eneo la taifa linalojulikana leo kama Israeli. Ibrahimu aliahidiwa na Mungu Kwamba atapata mtoto Katika uzee wake .Akiwa amesubiri utimilifu wa ahadi hii kwa muda mrefu bila kupata mtoto ,alimchukua kijakazi wake na akafanikiwa kuzaa naye mtoto aliyeitwa ishmail. Lakini mungu hakuwa amepanga kumpatia Ibrahim mtoto kwa njia hiyo, bado aliendelea kumhakikishia kwamba atapata mtoto kupitia kwa mkewe. Kwa sababu alikuwa na imani ,alifanikiwa kumpata mtoto aliyepewa jina la Isaka. Kisha Mungu akamuagiza kwenda kwenye mlima Moria, ili akamtoe kafara mtoto wake Isaka ambaye alikuwa amemsubiri Kwa muda mrefu. Huu mlima Moria upo wapi? Ingawa wakati wa siku za Ibrahimu ,miaka 2000KK ,eneo kubwa lilikuwa jangwa ,miaka 1000KK baadae Mfalme Daudi alijenga mji wa Yerusalem katika eneo hilo na mtoto wake aliyejulikana kama Mfalme Sulemani alijenga hekalu la kwanza kwenye eneo hilo la mlima Moria . Imeandikwa " ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya bwana huko Yerusalem ,juu ya mlima Moria ..." (2 Nyakati 3:1). Lakini kwa Ibrahimu Mungu anamwambia : " umchukue mwanao ,mwana wako wa pekee, umpendaye ,Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka, ..." ( Mzo. 22:2) Hivyo basi mji wa Yerusalem anajulikana kama nchi ya Moria au mlima wa Moria au mji wa Daudi mahali palepale alipoambiwa nabii Ibrahimu kwenda kutoa kafara ,ndipo Hapo hapo Mfalme Sulemani alipojenga hekalu la kumuabudia Mungu na kumtolea kafara za wanyama. Lakini zaidi ni katika mji wa Yerusalem ndipo yesu aliposulubiwa msalabani na hapo ndipo lilipo chimbuko la dini ya ukristo iliyoanzishwa kwa ujumla uzao wa Ibrahimu ndio chimbuko la dini kubwa tatu ,yaani uyahudi, uislamu ,na ukristo. Dini zingine zote zimetokana na dini hizi tatu ,Kutokana na ukweli huu ,wajenzi huru wamefanikiwa kuwashawishi viongozi wa dini zote na kuziunganisha kuwa dini moja. Ingawa majina ya dini hizi yanaendelea kutumika kiasi cha kuonekana kwamba hakuna tofauti ,lakini matunda ya dini hizi yanaonyesha wazi kuwa yanatokea kwenye mti mmoja. Katika mambo ya kiroho jina la dini ya mtu au dhehebu lake haliwezi kumfanya muumini afike mbinguni bali kitu muhimu ni matunda ya dini hiyo au dhehebu hilo. Kwa kujua hili mwanzilishi wa illuminati Dkt Adam Weishaupt aliandika akisema , The great strength of our order lies in its concealment " yaani nguvu kubwa ya Utaratibu wetu Iko katika kuficha na kufanya kazi zetu kwa siri kubwa " Hata huu muunganiko wa dini umefanywa kwa siri kubwa kiasi kwamba waumini wengi hawajui kinachoendelea. Weishaupt akaendelea kusema, " let it never appear in any place in its own name, but always covered by another name and another occupation " yaani; " hebu isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima ifanyike kwa jina lingine na kwa namna nyingine." ( Robin's Proofs of a Conspiracy, P. 195).
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·1كيلو بايت مشاهدة
  • TARABUSHI - KOFIA ZA KIHISTORIA.

    Leo hii ni aghalabu sana kukutana na mtu aliyevaa tarabushi kutokana na kutoweka kwa kofia hizi. Ni watu wachache sana wenye nazo, hususani wazee au wenye umri wa makamo, kwa kutaja wachache ni mbunge wa Musoma vijijini, Mh. Nimrod Mkono, na msanii wa maigizo, marehemu 'mzee small.

    Hizi ni kofia zenye rangi hasa nyekundu zikiwa na shada ya nyuzi nyeusi. Kwa kingereza zikijulikana kama 'Fez', kwa kiarabu 'Tarboosh' huku waswahili tukiita Tarabushi. Katika kuelezea historia ya Tarabushi, yanipasa kurudi miaka mia mbili iliyopita, pale ambapo Sultan Mahmud II wa dola ya Ottoman alipotangaza kofia za Fez/tarabushi kutumika kama vazi rasmi la dola hiyo. Sultani alifanya hivyo kufuatia kampeni yake ya kuboresha 'empire' ambapo alitamani watu wa Ottoman kuwa na utambulisho wao utakaowatofautisha na watu wengine.

    Kufuatia kampeni hiyo, tarabushi zilipata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Ottoman ambapo watu wengi walianza kuvaa. Mwaka 1829, Mfalme Mahmud II alipitisha sheria kwamba tarabushi zianze kutumika katika jeshi lake, hivyo kwanzia siku hiyo tuliona wanajeshi wa Ottoman Empire wakienda kwenye uwanja wa vita wakiwa wamevaa tarabushi.

    Kabla ya wazo la kutumia Tarabushi, Sultani Mahmud II alichagua aina fulani ya kofia zenye asili ya Uingereza ambazo zina umbo la pembe tatu. Lakini watu wake wa karibu walimshauri kutotumia kofia hizo, kwasababu waliona hiyo pembe tatu humaanisha 'utatu mtakatifu' hivyo isingeleta tafsiri nzuri kwa watu wa Ottoman ambao asilimia kubwa ni waislamu. Wakristo huamini katika "utatu mtakatifu" yaani Mungu, Mwana na Roho mtakatifu.

    Wakati Sultani anaendelea kuwaza mbadala wa kofia, ikatokea siku mabaharia wa Ottoman walikuwa wanarudi kutoka Morroco. Kichwani wakiwa wamevaa kofia nyekundu zenye shada ya nyuzi nyeusi. Sultani akavutiwa na kofia hizo na hapo ndio chanzo cha kuzichagua kutumika kama utamaduni wa Ottoman Empire. Morroco ndipo zilipokuwa zinatengenezwa kwa wingi kwasababu rangi ya kutengeneza kofia hizo ilikuwa inatokana na matunda fulani ambayo yalistawi kwa wingi hapo Morroco katika mji wa Fez. Ndio maana hata jina la kofia hizo 'Fez', limetokana na mji huo ambao hadi mwaka 1912 ndio ulikuwa mji mkuu wa Morroco.

    Umaarufu wa kofia hizi uliendelea kutapakaa kote ulimwenguni, ukizingatia kwamba dola ya Ottoman ilikuwa ni dola kubwa iliyoenea sehemu nyingi. Hivyo baadhi ya nchi zikaanza kutumia kofia hizi hususani katika majeshi yao-mfano Cyprus, Ugiriki, Albania. Pia India, Misri, Ufaransa n.k.

    Kwa huku kwetu Afrika Mashariki, umaarufu wa kofia hizi ulikuja baada ya ujio wa ukoloni. Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba katika kipindi cha Uingereza, waAfrika walijumuishwa katika jeshi la kikoloni ambalo lilikuja kuitwa 'King's African Rifles KAR' wakivaa sare za rangi ya khaki na kichwani walivaa Fez/ tarabushi. Jeshi hili lilianzishwa mwaka 1902 huko Kenya na baadae kuenea katika nchi zingine za Afrika Mashariki na hata kujumuishwa kwenye vita ya kwanza ya Dunia mwaka 1914.

    Pia katika makoloni ya Ujerumani, Tanganyika ikiwemo, kuliundwa jeshi la kikoloni 'Schutztruppe' ambapo waAfrika wengi walijumuishwa humo na kuwa Askari wa kikoloni 'Polizei-Askari', ambao sare zao zilikuwa za rangi ya khaki pamoja na kofia za tarabushi.

    Umaarufu wa kofia hizi za ulikuja kupungua mara baada kuanguka kwa dola ya Ottoman na kuzaliwa kwa nchi ya Uturuki ambapo mwaka 1925 Rais wa kwanza wa Uturuki bwana *Mustapha Kemal Artatuk,* alipiga marufuku kofia hizo. Hiyo ni katika hatua ya kuanzisha Uturuki mpya isiyo na mabaki ya kisultani. Pia huko Misri, mwaka 1956 Mara baada ya Gamer Abdel Nasser kumpindua mfalme, alipiga marufuku kofia za Tarboosh.

    Pia hata huku kwetu Afrika Mashariki, muda mfupi kidogo baada ya kupata uhuru, serikali ziliamua kubadilisha sare za majeshi yetu ambapo kofia zingine zilianza kutumika badala ya Tarabushi ambazo zilionekana ni kama za kikoloni. Na huo ndio ukawa mwanzo wa kupotea kwa kofia za Tarabushi japokuwa kuna baadhi ya watu waliendelea kubaki nazo.

    TARABUSHI - KOFIA ZA KIHISTORIA. Leo hii ni aghalabu sana kukutana na mtu aliyevaa tarabushi kutokana na kutoweka kwa kofia hizi. Ni watu wachache sana wenye nazo, hususani wazee au wenye umri wa makamo, kwa kutaja wachache ni mbunge wa Musoma vijijini, Mh. Nimrod Mkono, na msanii wa maigizo, marehemu 'mzee small. Hizi ni kofia zenye rangi hasa nyekundu zikiwa na shada ya nyuzi nyeusi. Kwa kingereza zikijulikana kama 'Fez', kwa kiarabu 'Tarboosh' huku waswahili tukiita Tarabushi. Katika kuelezea historia ya Tarabushi, yanipasa kurudi miaka mia mbili iliyopita, pale ambapo Sultan Mahmud II wa dola ya Ottoman alipotangaza kofia za Fez/tarabushi kutumika kama vazi rasmi la dola hiyo. Sultani alifanya hivyo kufuatia kampeni yake ya kuboresha 'empire' ambapo alitamani watu wa Ottoman kuwa na utambulisho wao utakaowatofautisha na watu wengine. Kufuatia kampeni hiyo, tarabushi zilipata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Ottoman ambapo watu wengi walianza kuvaa. Mwaka 1829, Mfalme Mahmud II alipitisha sheria kwamba tarabushi zianze kutumika katika jeshi lake, hivyo kwanzia siku hiyo tuliona wanajeshi wa Ottoman Empire wakienda kwenye uwanja wa vita wakiwa wamevaa tarabushi. Kabla ya wazo la kutumia Tarabushi, Sultani Mahmud II alichagua aina fulani ya kofia zenye asili ya Uingereza ambazo zina umbo la pembe tatu. Lakini watu wake wa karibu walimshauri kutotumia kofia hizo, kwasababu waliona hiyo pembe tatu humaanisha 'utatu mtakatifu' hivyo isingeleta tafsiri nzuri kwa watu wa Ottoman ambao asilimia kubwa ni waislamu. Wakristo huamini katika "utatu mtakatifu" yaani Mungu, Mwana na Roho mtakatifu. Wakati Sultani anaendelea kuwaza mbadala wa kofia, ikatokea siku mabaharia wa Ottoman walikuwa wanarudi kutoka Morroco. Kichwani wakiwa wamevaa kofia nyekundu zenye shada ya nyuzi nyeusi. Sultani akavutiwa na kofia hizo na hapo ndio chanzo cha kuzichagua kutumika kama utamaduni wa Ottoman Empire. Morroco ndipo zilipokuwa zinatengenezwa kwa wingi kwasababu rangi ya kutengeneza kofia hizo ilikuwa inatokana na matunda fulani ambayo yalistawi kwa wingi hapo Morroco katika mji wa Fez. Ndio maana hata jina la kofia hizo 'Fez', limetokana na mji huo ambao hadi mwaka 1912 ndio ulikuwa mji mkuu wa Morroco. Umaarufu wa kofia hizi uliendelea kutapakaa kote ulimwenguni, ukizingatia kwamba dola ya Ottoman ilikuwa ni dola kubwa iliyoenea sehemu nyingi. Hivyo baadhi ya nchi zikaanza kutumia kofia hizi hususani katika majeshi yao-mfano Cyprus, Ugiriki, Albania. Pia India, Misri, Ufaransa n.k. Kwa huku kwetu Afrika Mashariki, umaarufu wa kofia hizi ulikuja baada ya ujio wa ukoloni. Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba katika kipindi cha Uingereza, waAfrika walijumuishwa katika jeshi la kikoloni ambalo lilikuja kuitwa 'King's African Rifles KAR' wakivaa sare za rangi ya khaki na kichwani walivaa Fez/ tarabushi. Jeshi hili lilianzishwa mwaka 1902 huko Kenya na baadae kuenea katika nchi zingine za Afrika Mashariki na hata kujumuishwa kwenye vita ya kwanza ya Dunia mwaka 1914. Pia katika makoloni ya Ujerumani, Tanganyika ikiwemo, kuliundwa jeshi la kikoloni 'Schutztruppe' ambapo waAfrika wengi walijumuishwa humo na kuwa Askari wa kikoloni 'Polizei-Askari', ambao sare zao zilikuwa za rangi ya khaki pamoja na kofia za tarabushi. Umaarufu wa kofia hizi za ulikuja kupungua mara baada kuanguka kwa dola ya Ottoman na kuzaliwa kwa nchi ya Uturuki ambapo mwaka 1925 Rais wa kwanza wa Uturuki bwana *Mustapha Kemal Artatuk,* alipiga marufuku kofia hizo. Hiyo ni katika hatua ya kuanzisha Uturuki mpya isiyo na mabaki ya kisultani. Pia huko Misri, mwaka 1956 Mara baada ya Gamer Abdel Nasser kumpindua mfalme, alipiga marufuku kofia za Tarboosh. Pia hata huku kwetu Afrika Mashariki, muda mfupi kidogo baada ya kupata uhuru, serikali ziliamua kubadilisha sare za majeshi yetu ambapo kofia zingine zilianza kutumika badala ya Tarabushi ambazo zilionekana ni kama za kikoloni. Na huo ndio ukawa mwanzo wa kupotea kwa kofia za Tarabushi japokuwa kuna baadhi ya watu waliendelea kubaki nazo.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·1كيلو بايت مشاهدة
  • SABABU YA FERGUSON KUITWA 'SIR'.

    Mwaka 1983, Alex Ferguson alitunukiwa heshima ya 'Officer of the Order of British Empire OBE', kutoka kwa malkia wa Uingereza baada ya kuonesha mchango mkubwa kwenye soka, kipindi hiko akiwa anafundisha klabu ya Aberdeen ya huko Scotland.

    Ifahamike kwamba tuzo hiyo hutolewa na Malkia/Mfalme wa Uingereza kama ishara ya kutambua mchango wa watu mbalimbali katika kuleta mafanikio katika jamii. Hivyo Alex Ferguson alipokea heshima hiyo baada ya kuiongoza klabu ya Aberdeen FC kutwaa mataji 4 -kombe la shirikisho Scotland, kombe la Euro mwaka 1983, na matatu ya ligi kuu ya Scotland mwaka 1985.

    Mafanikio hayo ndio yalipelekea viongozi wa Manchester United kuanza 'kutafuta saini' ya Alex Ferguson ambaye bila kusita alisaini kandarasi ya kuinoa klabu hiyo kuanzia Novemba 1986. Alex Ferguson alionesha mafanikio makubwa sana akiwa klabuni hapo kiasi cha kuweza kutunukiwa heshima nyingine ya 'Commander of the Order of British Empire CBE' mnamo mwaka 1995.

    Miaka minne baadae, pamoja na mataji mengine, Alex Ferguson aliiongoza klabu ya Manchester Utd kutwaa mataji matatu ndani ya mwaka mmoja. Hiyo ndiyo ikapelekea mwaka 1999 atunukiwe heshima nyingine tena ya 'Knight commander of the order of British Empire KBE ambayo inamuwezesha mtu kupata hadhi ya kuitwa 'Sir'. Hivyo kwanzia siku hiyo Mzee Ferg akaanza kuitwa 'Sir Alex Ferguson'.

    Leo hii, dunia inamtambua Sir Alex Ferguson kama kocha mwenye mafanikio makubwa sana kwenye historia ya soka la Uingereza kwani ameweza kutwaa jumla ya *mataji 49* katika career yake ya ukocha na hivyo kustahili kuitwa 'Sir'.

    Pichani ni mwaka 1999 alipotunukiwa heshima hiyo.

    Ahsante.

    SABABU YA FERGUSON KUITWA 'SIR'. Mwaka 1983, Alex Ferguson alitunukiwa heshima ya 'Officer of the Order of British Empire OBE', kutoka kwa malkia wa Uingereza baada ya kuonesha mchango mkubwa kwenye soka, kipindi hiko akiwa anafundisha klabu ya Aberdeen ya huko Scotland. Ifahamike kwamba tuzo hiyo hutolewa na Malkia/Mfalme wa Uingereza kama ishara ya kutambua mchango wa watu mbalimbali katika kuleta mafanikio katika jamii. Hivyo Alex Ferguson alipokea heshima hiyo baada ya kuiongoza klabu ya Aberdeen FC kutwaa mataji 4 -kombe la shirikisho Scotland, kombe la Euro mwaka 1983, na matatu ya ligi kuu ya Scotland mwaka 1985. Mafanikio hayo ndio yalipelekea viongozi wa Manchester United kuanza 'kutafuta saini' ya Alex Ferguson ambaye bila kusita alisaini kandarasi ya kuinoa klabu hiyo kuanzia Novemba 1986. Alex Ferguson alionesha mafanikio makubwa sana akiwa klabuni hapo kiasi cha kuweza kutunukiwa heshima nyingine ya 'Commander of the Order of British Empire CBE' mnamo mwaka 1995. Miaka minne baadae, pamoja na mataji mengine, Alex Ferguson aliiongoza klabu ya Manchester Utd kutwaa mataji matatu ndani ya mwaka mmoja. Hiyo ndiyo ikapelekea mwaka 1999 atunukiwe heshima nyingine tena ya 'Knight commander of the order of British Empire KBE ambayo inamuwezesha mtu kupata hadhi ya kuitwa 'Sir'. Hivyo kwanzia siku hiyo Mzee Ferg akaanza kuitwa 'Sir Alex Ferguson'. Leo hii, dunia inamtambua Sir Alex Ferguson kama kocha mwenye mafanikio makubwa sana kwenye historia ya soka la Uingereza kwani ameweza kutwaa jumla ya *mataji 49* katika career yake ya ukocha na hivyo kustahili kuitwa 'Sir'. Pichani ni mwaka 1999 alipotunukiwa heshima hiyo. Ahsante.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·316 مشاهدة
  • TAMBUA MASHARTI YA NJIWA KABLA YA KUCHUKUA HATUA YA KUWAFUGA.

    1:Kwanza kabisa Njiwa ukiwanunua kwa mtu,sharti wawe wawili pair (dume na jike).

    2:Kama muuzaji aliwafuga kwa banda la juu,hakikisha unakowapeleka uwaandalie banda la juu,ukiwaweka banda la chini wanaondoka.

    3:Kama banda lako la chini,tafuta muuzaji mwenye banda la chini ndipo ununue vinginevyo unashauliwa uwanyonyoe manyoya na kuwafungia siku 40 kabla ya kuwafungulia.

    4:Njiwa wakiwa mbele yako usipende kuwajadili,hawapendi masimango wataondoka!.

    5:Ukifuga Njiwa nao hufatilia nyendo zako,ukiwa mlevi hawakai wanaondoka.Vurugu na kelele hawapendi.

    6:Njiwa wana nguvu kiimani,hawapendi mfugaji awe Mmbea,kugombana na majirani.Kwa sababu wakatika wa ugomvi Njiwa hukaa juu ya Paa wakisikiliza halafu huondoka na hawarudi tena.

    7:Njiwa hawapendi kuona umechinja Njiwa mwenzao mbele yao,wakiona wanahama wote kwa sababu wanahisi utawachinja.

    8:Njiwa hawapendi makelele ya kushtukiza kams honi kali,kuwarushia jiwe na miziki mikubwa.Ukifanya hayo wanahama.

    9:Njiwa akifa mmoja,huomboleza.Unashauliwa umtafute mwenza haraka kwa Njiwa anaebaki la sivyo wanaondoka/kuondoka.

    10:Hakikisha Njiwa huwachanganyi na kuku mwenye vifaranga,wakiparuliwa huondoka mazima.

    11:Njiwa wanaofugwa banda la Uani/nyuma/jikoni huzaliana haraka zaidi kwa sababu ya mazingira tulivu.

    12:Hakikisha Pakashume hawazoei kufika nyumbani kwako!.Njiwa hawapatani na Paka pori la sivyo wanahama wote!

    13:Inasemekana Njiwa ni wa pili kwa wivu baada ya Nyegele!,Nyegere anawivu sana kwa jike lake na huwa anatembea akiwa nyuma ya jike.Kama ikitokea hata jani likagusa sehemu ya uzazi wa jike,Nyegere dume huanzisha vita na jani hilo.

    #Note: Hakikisha unawafuga Njiwa wawili wawili.

    ~Tukutane siku nyingine kwa habari za kuhusu mnyama hatari sana Nyegere...
    TAMBUA MASHARTI YA NJIWA KABLA YA KUCHUKUA HATUA YA KUWAFUGA. 1:Kwanza kabisa Njiwa ukiwanunua kwa mtu,sharti wawe wawili pair (dume na jike). 2:Kama muuzaji aliwafuga kwa banda la juu,hakikisha unakowapeleka uwaandalie banda la juu,ukiwaweka banda la chini wanaondoka. 3:Kama banda lako la chini,tafuta muuzaji mwenye banda la chini ndipo ununue vinginevyo unashauliwa uwanyonyoe manyoya na kuwafungia siku 40 kabla ya kuwafungulia. 4:Njiwa wakiwa mbele yako usipende kuwajadili,hawapendi masimango wataondoka!. 5:Ukifuga Njiwa nao hufatilia nyendo zako,ukiwa mlevi hawakai wanaondoka.Vurugu na kelele hawapendi. 6:Njiwa wana nguvu kiimani,hawapendi mfugaji awe Mmbea,kugombana na majirani.Kwa sababu wakatika wa ugomvi Njiwa hukaa juu ya Paa wakisikiliza halafu huondoka na hawarudi tena. 7:Njiwa hawapendi kuona umechinja Njiwa mwenzao mbele yao,wakiona wanahama wote kwa sababu wanahisi utawachinja. 8:Njiwa hawapendi makelele ya kushtukiza kams honi kali,kuwarushia jiwe na miziki mikubwa.Ukifanya hayo wanahama. 9:Njiwa akifa mmoja,huomboleza.Unashauliwa umtafute mwenza haraka kwa Njiwa anaebaki la sivyo wanaondoka/kuondoka. 10:Hakikisha Njiwa huwachanganyi na kuku mwenye vifaranga,wakiparuliwa huondoka mazima. 11:Njiwa wanaofugwa banda la Uani/nyuma/jikoni huzaliana haraka zaidi kwa sababu ya mazingira tulivu. 12:Hakikisha Pakashume hawazoei kufika nyumbani kwako!.Njiwa hawapatani na Paka pori la sivyo wanahama wote! 13:Inasemekana Njiwa ni wa pili kwa wivu baada ya Nyegele!,Nyegere anawivu sana kwa jike lake na huwa anatembea akiwa nyuma ya jike.Kama ikitokea hata jani likagusa sehemu ya uzazi wa jike,Nyegere dume huanzisha vita na jani hilo. #Note: Hakikisha unawafuga Njiwa wawili wawili. ~Tukutane siku nyingine kwa habari za kuhusu mnyama hatari sana Nyegere...
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·660 مشاهدة
  • PICHANI anaonekana aliyekuwa kiongozi wa Ujerumani bwana Adolf Hitler akipiga saluti. Hiyo inaitwa saluti ya kinazi, au kwa kingereza *'Nazi Salute'* ambayo ilikuwa ikipigwa na wananchi wa ujerumani kama ishara ya kutoa heshima kwa kiongozi wao.

    Saluti hiyo hupigwa kwa kunyoosha mkono wa kulia mbele usawa wa uso, huku vidole vikiwa vimenyooka....Na Mara zote, saluti hiyo huenda sanjari na maneno ..'''Heil Hitler..Heil, mein Führer""..yaani "Salaam Hitler, Salaam kiongozi wangu"

    Saluti hii ilianza kutumika katika miaka ya 1930, wakati wa kipindi cha Adolf Hitler na chama chake cha *Nazi Party.* Saluti hii ilikuwa ikifanywa na raia wa wajerumani, hususani wanajeshi, katika kutoa salamu na heshima kwa Hitler pamoja na kulitukuza taifa la ujerumani.

    Tarehe 13 Julai 1933, Serikali ilitoa Agizo kuwaamuru wafanyakazi wote wa serikali ya ujerumani kutumia saluti hiyo. Pia agizo hilo liliwataka watu wote kupiga saluti hiyo wakati wa kuimba wimbo wa taifa au wimbo wa chama...Na yeyote atakayekaidi, adhabu kali itatolewa juu yake.

    Mwaka 1934, tulishuhudia kuanzishwa kwa mahakama maalumu kwa ajili ya kuwahukumu wale wanaopinga saluti hiyo. Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Paul Schneider, alipokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa itikadi za kiNazi baada ya kugoma kupiga saluti hiyo. Kwa ufupi niseme kwamba saluti hiyo ilikuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ambapo Watu walikuwa wakisalimiana kwa saluti hiyo au kwa kutamka 'Hail Hilter'.

    Kama nilivyosema hapo awali kwamba, Saluti hii ilikuwa ikitumika wakati wa Adolf Hitler tuu, kwani baada ya kuanguka kwa utawala wake, saluti hii ilikomeshwa.

    Leo hii, ni kosa kubwa sana kutumia saluti hii. Na mtu yeyote atakayebainika kuonesha ishara hii, adhabu kali itatolewa dhidi yake. Mfano, Mwaka 2007 kuna mtu mmoja aliyeitwa Horst Mahler, alihukumiwa miezi sita jela baada ya kuonekana kutumia ishara hii.

    Pia mwaka 2013, mchezaji wa klabu ya soka ya AEK Athens FC, alifungiwa kucheza soka katika timu yake ya taifa ya Ugiriki, baada ya kutumia saluti hiyo wakati akishangilia goli aliloshinda katika mechi dhidi ya klabu ya Veria F.C.

    Naam!..Na hiyo ndio 'Nazi Salute' ambayo Mara nyingine huitwa Hitler Salute, ambayo Leo hii ni marufuku kutumika, na endapo utakamatwa umenyoosha mkono hivyo, Utapata tabu sana!!

    ***

    PICHANI anaonekana aliyekuwa kiongozi wa Ujerumani bwana Adolf Hitler akipiga saluti. Hiyo inaitwa saluti ya kinazi, au kwa kingereza *'Nazi Salute'* ambayo ilikuwa ikipigwa na wananchi wa ujerumani kama ishara ya kutoa heshima kwa kiongozi wao. Saluti hiyo hupigwa kwa kunyoosha mkono wa kulia mbele usawa wa uso, huku vidole vikiwa vimenyooka....Na Mara zote, saluti hiyo huenda sanjari na maneno ..'''Heil Hitler..Heil, mein Führer""..yaani "Salaam Hitler, Salaam kiongozi wangu" Saluti hii ilianza kutumika katika miaka ya 1930, wakati wa kipindi cha Adolf Hitler na chama chake cha *Nazi Party.* Saluti hii ilikuwa ikifanywa na raia wa wajerumani, hususani wanajeshi, katika kutoa salamu na heshima kwa Hitler pamoja na kulitukuza taifa la ujerumani. Tarehe 13 Julai 1933, Serikali ilitoa Agizo kuwaamuru wafanyakazi wote wa serikali ya ujerumani kutumia saluti hiyo. Pia agizo hilo liliwataka watu wote kupiga saluti hiyo wakati wa kuimba wimbo wa taifa au wimbo wa chama...Na yeyote atakayekaidi, adhabu kali itatolewa juu yake. Mwaka 1934, tulishuhudia kuanzishwa kwa mahakama maalumu kwa ajili ya kuwahukumu wale wanaopinga saluti hiyo. Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Paul Schneider, alipokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa itikadi za kiNazi baada ya kugoma kupiga saluti hiyo. Kwa ufupi niseme kwamba saluti hiyo ilikuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ambapo Watu walikuwa wakisalimiana kwa saluti hiyo au kwa kutamka 'Hail Hilter'. Kama nilivyosema hapo awali kwamba, Saluti hii ilikuwa ikitumika wakati wa Adolf Hitler tuu, kwani baada ya kuanguka kwa utawala wake, saluti hii ilikomeshwa. Leo hii, ni kosa kubwa sana kutumia saluti hii. Na mtu yeyote atakayebainika kuonesha ishara hii, adhabu kali itatolewa dhidi yake. Mfano, Mwaka 2007 kuna mtu mmoja aliyeitwa Horst Mahler, alihukumiwa miezi sita jela baada ya kuonekana kutumia ishara hii. Pia mwaka 2013, mchezaji wa klabu ya soka ya AEK Athens FC, alifungiwa kucheza soka katika timu yake ya taifa ya Ugiriki, baada ya kutumia saluti hiyo wakati akishangilia goli aliloshinda katika mechi dhidi ya klabu ya Veria F.C. Naam!..Na hiyo ndio 'Nazi Salute' ambayo Mara nyingine huitwa Hitler Salute, ambayo Leo hii ni marufuku kutumika, na endapo utakamatwa umenyoosha mkono hivyo, Utapata tabu sana!! ***
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·718 مشاهدة
  • MAANA YA 'HANSARD' ZA BUNGE

    NENO "Hansard" ni maarufu sana katika shughuli za Bunge nchini Tanzania, na pia katika nchi zote za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Countries). Hutamkwa kwa haraka, "han-sadi."

    Maana yake ni Kumbukumbu Rasmi za Majadiliano katika mijadala na hoja kati ya Wabunge na Serikali , ambayo hufanyika ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri.

    Kimsingi, ni mtiririko wa nukuu mbalimbali za hoja za wabunge (ambao ni wawakilishi wa wananchi) na Mawaziri (ambao ni Serikali), katika mijadala yao kwa ruksa ya Spika wa Bunge.

    Ni mtiririko wa nukuu ya majadiliano ya wabunge wakati wote wa vikao vya Bunge la Jamhuri, ambapo kila baada ya vikao husika majadiliano hayo huchapishwa na huhifadhiwa kama kumbukumbu mahsusi, hususan kwa ajili ya matumizi katika kumbukumbu za historia.

    Aidha, Hansard ni jina la heshima kutokana na kazi ya mwandishi na mchapishaji wa nyaraka na vitabu wa nchini Uingereza, Thomas Curson Hansard, ambaye alikuwa mwandishi na mchapishaji wa kwanza wa kumbukumbu za Bunge la Uingereza kule Westminster, mjini London.

    Kutokana na kazi hiyo ya mwandishi huyo, Thomas Hansard, ndipo majadiliano ya wabunge wa Uingereza yakapewa jina la Hansard.

    Hiyo ni kwa vile kila baada ya vikao husika vya wabunge, majadiliano yao yalikuwa tayari yamechapishwa na kusomwa na wao wenyewe, na pia watu wengine, kuhusiana na kile kilichokuwa kinajadiliwa na wabunge ndani ya Bunge.

    PICHA: Thomas Curson Hansard, ambaye alifariki mwaka 1833 akiwa na umri wa miaka 57.
    MAANA YA 'HANSARD' ZA BUNGE NENO "Hansard" ni maarufu sana katika shughuli za Bunge nchini Tanzania, na pia katika nchi zote za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Countries). Hutamkwa kwa haraka, "han-sadi." Maana yake ni Kumbukumbu Rasmi za Majadiliano katika mijadala na hoja kati ya Wabunge na Serikali , ambayo hufanyika ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri. Kimsingi, ni mtiririko wa nukuu mbalimbali za hoja za wabunge (ambao ni wawakilishi wa wananchi) na Mawaziri (ambao ni Serikali), katika mijadala yao kwa ruksa ya Spika wa Bunge. Ni mtiririko wa nukuu ya majadiliano ya wabunge wakati wote wa vikao vya Bunge la Jamhuri, ambapo kila baada ya vikao husika majadiliano hayo huchapishwa na huhifadhiwa kama kumbukumbu mahsusi, hususan kwa ajili ya matumizi katika kumbukumbu za historia. Aidha, Hansard ni jina la heshima kutokana na kazi ya mwandishi na mchapishaji wa nyaraka na vitabu wa nchini Uingereza, Thomas Curson Hansard, ambaye alikuwa mwandishi na mchapishaji wa kwanza wa kumbukumbu za Bunge la Uingereza kule Westminster, mjini London. Kutokana na kazi hiyo ya mwandishi huyo, Thomas Hansard, ndipo majadiliano ya wabunge wa Uingereza yakapewa jina la Hansard. Hiyo ni kwa vile kila baada ya vikao husika vya wabunge, majadiliano yao yalikuwa tayari yamechapishwa na kusomwa na wao wenyewe, na pia watu wengine, kuhusiana na kile kilichokuwa kinajadiliwa na wabunge ndani ya Bunge. PICHA: Thomas Curson Hansard, ambaye alifariki mwaka 1833 akiwa na umri wa miaka 57.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·618 مشاهدة
  • HISTORIA YA *MBIO ZA MARATHON*

    WATU WENGI TUMEZOEA KUANGALIA MASHINDANO YA MBIO ZA MARATHON KATIKA MICHEZO YA OLIMPIKI AU KWENGINEKO LAKINI HATUJAPATA KUFAHAMU NINI CHANZO AU HISTORIA YA MBIO HIZI.

    SASA UNGANA NAMI ILI KUJUA HISTORIA YAKE.

    Hebu fatilia kisa hiki👇🏿

    Mnamo miaka ya 490 BC, Dola ya uajemi *(Persian empire)* ikiwa chini ya mfalme Darius ilikuwa inavamia mji wa *anthens* ambao ndio makao makuu ya *ugiriki*

    Uvamizi huo ulikuja kama shambulio la kutaka kulipa kisasi kwa anthens kufuatia kitendo chao cha kuwasaidia watu wa mji wa *Ionia* waliokuwa wanataka kupindua utawala wa *Darius*(mfalme wa Persia) katika mapambano yaliyofanyika katika mji wa lade *(battle of lade)*mnamo 493BC

    Ingawa Persia waliweza kushinda vita hiyo dhidi ya watu wa ionia , Mfalme Darius wa Persia aliapa kuwaadhibu miji ya anthens na eretria kwa kitendo chao cha kuisaidia Ionia.

    Hivyo basi, mwaka 490BC, mfalme Darius alipeleka majeshi yakiongozwa na kamanda Datis, kwenda kuvamia, kuangamiza na kuteka miji ya anthens na eretria, na hatimaye kuitawala ugiriki yote.

    Persian ilivamia miji ya Aegean, kupitia cyclade na kufanikiwa kuiteka eretrea, na kuendelea kuukaribia mji wa anthen.

    Lakini walipofika mji wa marathon, majeshi ya anthens wakawa tayari wamefika eneo hilo. Na ndipo mapigano yalifanyika katika mji huo wa *marathon*

    Anthens walimtuma mtu mmoja aitwaye *Philippides* kwenda mji wa Spartan ili kuwaomba msaada wa kuongezewa nguvu dhidi ya Persian.

    *Philippides* akakimbia mojakwa moja hadi mji wa Spartans, lakini siku ile akakuta watu wa mji huo (spartan) wapo katika sherehe za kuabudu, hivyo hawakuweza kuja kuwasaidia anthens kwenye vita.

    Vita iliendelea na hatimaye anthens wakaweza kushinda vita dhidi ya Persian empire.
    *philippides* kama ilivyo kawaida yake, alivoona anthens wameshinda vita akajawa na furaha kubwa, akakimbia bila kupumzika kutoka mji wa *marathon* ambapo vita vilifanyika hadi mji wa anthens kwenda kutoa ripoti ya ushindi.

    Alipofika offisini aliingia kwa pupa pasipo kubisha hodi.
    kulikuwa na viongozi kadhaa ofisini humo.

    Phillipides akatamka maneno haya *"we have won"* (tumeshinda) na akakata roho papo hapo.

    ......

    Hivyo basi, haya mashindano ya mbio za marathon , yalianzishwa kama kumbukumbu ya shujaa *phillippides* ambaye alikimbia kutoka mji wa marathon hadi anthens.

    .....
    Mbio za kwanza za marathon zilifanyika mnamo mwaka 1896 kwenye michezo ya kwanza ya *olimpiki mpya.* -kama mtakuwa mnakumbuka vizuri nilitoa historia ya michezo ya olimpiki kwamba ilikuwa na awàmu mbili (ancients olimpic 776 BC na modern olimpik 1896.)

    Mbio hizi za marathon, zina umbali wa kilometa 40.2km
    Baada ya kufanyika marekebisho kutoka 40km.- Na huu umbali ni makadirio ya umbali kutoka mji wa marathon hadi Anthen.

    Mwisho.

    HISTORIA YA *MBIO ZA MARATHON* WATU WENGI TUMEZOEA KUANGALIA MASHINDANO YA MBIO ZA MARATHON KATIKA MICHEZO YA OLIMPIKI AU KWENGINEKO LAKINI HATUJAPATA KUFAHAMU NINI CHANZO AU HISTORIA YA MBIO HIZI. SASA UNGANA NAMI ILI KUJUA HISTORIA YAKE. Hebu fatilia kisa hiki👇🏿 Mnamo miaka ya 490 BC, Dola ya uajemi *(Persian empire)* ikiwa chini ya mfalme Darius ilikuwa inavamia mji wa *anthens* ambao ndio makao makuu ya *ugiriki* Uvamizi huo ulikuja kama shambulio la kutaka kulipa kisasi kwa anthens kufuatia kitendo chao cha kuwasaidia watu wa mji wa *Ionia* waliokuwa wanataka kupindua utawala wa *Darius*(mfalme wa Persia) katika mapambano yaliyofanyika katika mji wa lade *(battle of lade)*mnamo 493BC Ingawa Persia waliweza kushinda vita hiyo dhidi ya watu wa ionia , Mfalme Darius wa Persia aliapa kuwaadhibu miji ya anthens na eretria kwa kitendo chao cha kuisaidia Ionia. Hivyo basi, mwaka 490BC, mfalme Darius alipeleka majeshi yakiongozwa na kamanda Datis, kwenda kuvamia, kuangamiza na kuteka miji ya anthens na eretria, na hatimaye kuitawala ugiriki yote. Persian ilivamia miji ya Aegean, kupitia cyclade na kufanikiwa kuiteka eretrea, na kuendelea kuukaribia mji wa anthen. Lakini walipofika mji wa marathon, majeshi ya anthens wakawa tayari wamefika eneo hilo. Na ndipo mapigano yalifanyika katika mji huo wa *marathon* Anthens walimtuma mtu mmoja aitwaye *Philippides* kwenda mji wa Spartan ili kuwaomba msaada wa kuongezewa nguvu dhidi ya Persian. *Philippides* akakimbia mojakwa moja hadi mji wa Spartans, lakini siku ile akakuta watu wa mji huo (spartan) wapo katika sherehe za kuabudu, hivyo hawakuweza kuja kuwasaidia anthens kwenye vita. Vita iliendelea na hatimaye anthens wakaweza kushinda vita dhidi ya Persian empire. *philippides* kama ilivyo kawaida yake, alivoona anthens wameshinda vita akajawa na furaha kubwa, akakimbia bila kupumzika kutoka mji wa *marathon* ambapo vita vilifanyika hadi mji wa anthens kwenda kutoa ripoti ya ushindi. Alipofika offisini aliingia kwa pupa pasipo kubisha hodi. kulikuwa na viongozi kadhaa ofisini humo. Phillipides akatamka maneno haya *"we have won"* (tumeshinda) na akakata roho papo hapo. ...... Hivyo basi, haya mashindano ya mbio za marathon , yalianzishwa kama kumbukumbu ya shujaa *phillippides* ambaye alikimbia kutoka mji wa marathon hadi anthens. ..... Mbio za kwanza za marathon zilifanyika mnamo mwaka 1896 kwenye michezo ya kwanza ya *olimpiki mpya.* -kama mtakuwa mnakumbuka vizuri nilitoa historia ya michezo ya olimpiki kwamba ilikuwa na awàmu mbili (ancients olimpic 776 BC na modern olimpik 1896.) Mbio hizi za marathon, zina umbali wa kilometa 40.2km Baada ya kufanyika marekebisho kutoka 40km.- Na huu umbali ni makadirio ya umbali kutoka mji wa marathon hadi Anthen. Mwisho.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·705 مشاهدة
  • : Jifunze kukaa na dhoruba zako;
    Sio kila sikio linapaswa kusikia ngurumo yako ... Asili, upweke, maombi ya kina, kufunga na kufuli juu ya kinywa changu, ilinisaidia kushinda vitu vingi ambavyo watu walinirushia ili kuniangamiza. Baadhi ya wale ambao watakuchoma kisu, pia watatuma baadhi ya watu ambao watakuja kukufariji, ili wale watoa habari wanaojifanya kuwa marafiki, wapeleke habari kuhusu hali yako ya huzuni au kuhusu hatua yako inayofuata; Kuwa na busara na hekima. Baadhi ya waliokuumiza hawana huruma; Hawakudhuru na kupumzika, badala yake wanaleta watu ambao watasikia kutoka kwako na kuripoti kwao. Mara nyingi mimi hunusurika nyakati za dhoruba na misimu katika maisha yangu, na kutoka nje nikinuka kama Rose, kwa sababu mara nyingi mimi huketi na dhoruba zangu katika maombi ya kina, na mara nyingi huwa sisemi maneno kwa kujibu mtu yeyote. Ninajua vizuri sana kwamba wengi watataka kusikia kutoka kwako, si kwa sababu wanataka kukusaidia, lakini kwa sababu wanataka kuwa na kitu dhidi yako, lakini jaribu kuwa kama Kristo, kusimama mbele yao, bila kusema neno lolote. Nilizuia ulimi wangu wakati nilipaswa kuzungumza na kutoa sikio lolote la kusikiliza. Nilimgeukia Mungu na kuzungumza naye, badala ya kuzungumza nao, kwa sababu najua vizuri sana kwamba baadhi ya sauti hizo za kufariji zinazotuzunguka, ndiyo sababu hasa ya sisi kulia na kulia bila kujizuia. Nimejifunza kwamba si kila sikio linalopaswa kusikia ngurumo kubwa wakati wa majira ya dhoruba ya maisha yangu, na si kila bega linalopatikana ambalo ninapaswa kuegemea. Ninatumia goti langu na ninawaombea wasaidizi halali wajitokeze. Jifunze kutembea hadi kwenye kanisa na kupiga magoti huko kimya. Hata ukikosa maneno, kumbuka kwamba huhitaji maneno ili kumsukuma Mungu; Anasoma moyo wako kama barua na anafanya kwa njia ambazo hukuwahi kufikiria. Jifunze kunyamaza wanapotarajia uitikie na kuongea ovyo. Wakati mwingine, tabasamu na kucheka pamoja nao, lakini usiache maombi yako Kwa Yesu kwenye Sakramenti Takatifu. Yesu alijua Yuda alikuwa akipanga njama ya kumuuza, lakini alimwita "rafiki." Dhoruba hizo za maisha zinapokuja, kumbuka kuwa hauko peke yako. Kwangu mimi, ni bora kutoweka bila kuwaeleza, kuliko wewe kuzunguka kuzungumza na kila sikio linalosikiliza. Nilijifunza kwamba watu hawana wasiwasi sana juu ya wasiwasi wako; Ndiyo, wanaweza kukusemea neno moja au mawili ya kufariji, lakini mara nyingi, hakuna anayejali sana. Ni afadhali ngurumo zingurume ukiwa katika uwepo wa Mungu, badala ya kuzunguka huku na huku ukilia kama mtoto mchanga kwa kujihurumia. Ni bora kwenda kwa Yesu katika Sakramenti Takatifu na kulia na moyo wako huko, kuliko kuchukua simu yako na kwenda Whatsapp na kuwalilia kana kwamba wao ni Mungu. Sababu kwa nini baadhi yetu bado tunazunguka katika miduara katika maisha haya ni kwa sababu hatujajifunza jinsi ya kutumia kanuni ya kuweka ngurumo katika dhoruba za maisha yetu kutoka kwa kila sikio linalosikiliza. Mwambie Mungu na ufunge kinywa chako. Ongea na mtu sahihi, lakini sio kwa kila mtu. Jifunze kukaa na dhoruba zako;

    Si kila sikio linastahili kusikia ngurumo yako ...


    Credit Albert Nwosu
    : Jifunze kukaa na dhoruba zako; Sio kila sikio linapaswa kusikia ngurumo yako ... Asili, upweke, maombi ya kina, kufunga na kufuli juu ya kinywa changu, ilinisaidia kushinda vitu vingi ambavyo watu walinirushia ili kuniangamiza. Baadhi ya wale ambao watakuchoma kisu, pia watatuma baadhi ya watu ambao watakuja kukufariji, ili wale watoa habari wanaojifanya kuwa marafiki, wapeleke habari kuhusu hali yako ya huzuni au kuhusu hatua yako inayofuata; Kuwa na busara na hekima. Baadhi ya waliokuumiza hawana huruma; Hawakudhuru na kupumzika, badala yake wanaleta watu ambao watasikia kutoka kwako na kuripoti kwao. Mara nyingi mimi hunusurika nyakati za dhoruba na misimu katika maisha yangu, na kutoka nje nikinuka kama Rose, kwa sababu mara nyingi mimi huketi na dhoruba zangu katika maombi ya kina, na mara nyingi huwa sisemi maneno kwa kujibu mtu yeyote. Ninajua vizuri sana kwamba wengi watataka kusikia kutoka kwako, si kwa sababu wanataka kukusaidia, lakini kwa sababu wanataka kuwa na kitu dhidi yako, lakini jaribu kuwa kama Kristo, kusimama mbele yao, bila kusema neno lolote. Nilizuia ulimi wangu wakati nilipaswa kuzungumza na kutoa sikio lolote la kusikiliza. Nilimgeukia Mungu na kuzungumza naye, badala ya kuzungumza nao, kwa sababu najua vizuri sana kwamba baadhi ya sauti hizo za kufariji zinazotuzunguka, ndiyo sababu hasa ya sisi kulia na kulia bila kujizuia. Nimejifunza kwamba si kila sikio linalopaswa kusikia ngurumo kubwa wakati wa majira ya dhoruba ya maisha yangu, na si kila bega linalopatikana ambalo ninapaswa kuegemea. Ninatumia goti langu na ninawaombea wasaidizi halali wajitokeze. Jifunze kutembea hadi kwenye kanisa na kupiga magoti huko kimya. Hata ukikosa maneno, kumbuka kwamba huhitaji maneno ili kumsukuma Mungu; Anasoma moyo wako kama barua na anafanya kwa njia ambazo hukuwahi kufikiria. Jifunze kunyamaza wanapotarajia uitikie na kuongea ovyo. Wakati mwingine, tabasamu na kucheka pamoja nao, lakini usiache maombi yako Kwa Yesu kwenye Sakramenti Takatifu. Yesu alijua Yuda alikuwa akipanga njama ya kumuuza, lakini alimwita "rafiki." Dhoruba hizo za maisha zinapokuja, kumbuka kuwa hauko peke yako. Kwangu mimi, ni bora kutoweka bila kuwaeleza, kuliko wewe kuzunguka kuzungumza na kila sikio linalosikiliza. Nilijifunza kwamba watu hawana wasiwasi sana juu ya wasiwasi wako; Ndiyo, wanaweza kukusemea neno moja au mawili ya kufariji, lakini mara nyingi, hakuna anayejali sana. Ni afadhali ngurumo zingurume ukiwa katika uwepo wa Mungu, badala ya kuzunguka huku na huku ukilia kama mtoto mchanga kwa kujihurumia. Ni bora kwenda kwa Yesu katika Sakramenti Takatifu na kulia na moyo wako huko, kuliko kuchukua simu yako na kwenda Whatsapp na kuwalilia kana kwamba wao ni Mungu. Sababu kwa nini baadhi yetu bado tunazunguka katika miduara katika maisha haya ni kwa sababu hatujajifunza jinsi ya kutumia kanuni ya kuweka ngurumo ⚡ katika dhoruba za maisha yetu kutoka kwa kila sikio linalosikiliza. Mwambie Mungu na ufunge kinywa chako. Ongea na mtu sahihi, lakini sio kwa kila mtu. Jifunze kukaa na dhoruba zako; Si kila sikio linastahili kusikia ngurumo yako ⚡... Credit Albert Nwosu
    Like
    Love
    2
    · 1 التعليقات ·0 المشاركات ·1كيلو بايت مشاهدة
  • hello
    hello
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·401 مشاهدة
  • Rais Samia Suluhu amempangia Balozi Dkt. Stephen John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil akichukua nafasi ya Prof. Adelardus Kilangi ambaye amepangiwa majukumu mengine.

    Rais Samia Suluhu amempangia Balozi Dkt. Stephen John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil akichukua nafasi ya Prof. Adelardus Kilangi ambaye amepangiwa majukumu mengine.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·232 مشاهدة