Atualize para o Pro

  • MANSA MUSA
    .
    Mansa Musa alizaliwa 1280 katika familia ya watawala. Nduguye , Mansa Abu-Bakr, alitawala ufamle huo hadi 1312, wakati alipoamua kwenda safari. Kulingana na mwanahistoria wa karne ya 14 Shibab al-Umari, Abu-Bakr alipendelea sana kuiona bahari ya Atlantic na kile ilichokuwa nacho. Aliripotiwa kuanza safari na msafara wa meli 2000 na maelfu ya wanaume na wanawake pamoja na watumwa. Walienda na hawakurudi tena. Wengine kama vile mwanahistoria wa Marekani Ivan Van Sertima anadai kwamba waliwasili Marekani Kusini. Lakini hakuna ushahidi. Ukweli ni kwamba Mansa Musa alirithi ufalme ulioachwa nyuma na nduguye. Chini ya uongozi wake ufalme wa Mali uliimarika kwa kiwango kikubwa.
    Watag marafk zako waje wapate kufahamu mengi wasiyo yajua kuhusu Mansa Musa pia isisahau ku follow hawa watu.
    .
    .
    .
    Mfalme huyo aliripotiwa kuondoka Mali na msafara wa watu 60,000. Alibeba ufalme wake wote na maafisa wake , wanajeshi, watumbuizaji , madereva wa ngamia na watumwa 12,000 mbali na idadi kubwa ya mbuzi , kondoo na chakula. Ulikuwa mji uliokuwa ukipitia katika jangwa. Mji ambao wakaazi wake hadi watumwa wake walikuwa wamevalia dhahabu na nguo za hariri. Kulikuwa na ngamia 100 ambao kila mmojawao alikuwa akibeba mamia ya pauni za dhahabu. Utajiri huo ulionekana zaidi wakati msafara huo ulipowasili mjini Cairo ambapo ulionekana.
    .
    .
    Kampuni ya kiteknolojia ya Marekani SmartAsset.com inakadiria kwamba kutokana na kuanguka kwa bei ya dhahabu, Hija ya Mansa Musa ilisababisha hasara ya $1.5bn (£1.1bn) katika uchumi wa eneo la mashariki ya kati. Alipokuwa akirudi nyumbani, Mansa Musa alpitia tena Misri na kulingana wachache akajaribu kusaidia uchumi wa taifa hilo kwa kuondoa dhahabu iliokuwepo kupitia kuiomba kwa kiwango cha juu kutoka kwa wafanyibiashara wa Misri. Wengine wanasema kuwa aligharamika sana hadi dhahabu alizokuwa nazo zikaisha. Lucy Duran wa Shule ya African and Oriental Studies mjini London anasema kwamba wanahistoria wa Mali walikasirishwa naye. ''Alitoa dhahabu nyingi ya Mali hali ambayo iliwafanya wanahistoria hao kutomsifu katika nyimbo zao na hadithi kwa kuwa wanaona kwamba alipoteza mali nyingi ya taifa hilo nje ya ufalme wake'', alisema.


    .
    SHUKRANI
    MANSA MUSA . Mansa Musa alizaliwa 1280 katika familia ya watawala. Nduguye , Mansa Abu-Bakr, alitawala ufamle huo hadi 1312, wakati alipoamua kwenda safari. Kulingana na mwanahistoria wa karne ya 14 Shibab al-Umari, Abu-Bakr alipendelea sana kuiona bahari ya Atlantic na kile ilichokuwa nacho. Aliripotiwa kuanza safari na msafara wa meli 2000 na maelfu ya wanaume na wanawake pamoja na watumwa. Walienda na hawakurudi tena. Wengine kama vile mwanahistoria wa Marekani Ivan Van Sertima anadai kwamba waliwasili Marekani Kusini. Lakini hakuna ushahidi. Ukweli ni kwamba Mansa Musa alirithi ufalme ulioachwa nyuma na nduguye. Chini ya uongozi wake ufalme wa Mali uliimarika kwa kiwango kikubwa. Watag marafk zako waje wapate kufahamu mengi wasiyo yajua kuhusu Mansa Musa pia isisahau ku follow hawa watu. . . . Mfalme huyo aliripotiwa kuondoka Mali na msafara wa watu 60,000. Alibeba ufalme wake wote na maafisa wake , wanajeshi, watumbuizaji , madereva wa ngamia na watumwa 12,000 mbali na idadi kubwa ya mbuzi , kondoo na chakula. Ulikuwa mji uliokuwa ukipitia katika jangwa. Mji ambao wakaazi wake hadi watumwa wake walikuwa wamevalia dhahabu na nguo za hariri. Kulikuwa na ngamia 100 ambao kila mmojawao alikuwa akibeba mamia ya pauni za dhahabu. Utajiri huo ulionekana zaidi wakati msafara huo ulipowasili mjini Cairo ambapo ulionekana. . . Kampuni ya kiteknolojia ya Marekani SmartAsset.com inakadiria kwamba kutokana na kuanguka kwa bei ya dhahabu, Hija ya Mansa Musa ilisababisha hasara ya $1.5bn (£1.1bn) katika uchumi wa eneo la mashariki ya kati. Alipokuwa akirudi nyumbani, Mansa Musa alpitia tena Misri na kulingana wachache akajaribu kusaidia uchumi wa taifa hilo kwa kuondoa dhahabu iliokuwepo kupitia kuiomba kwa kiwango cha juu kutoka kwa wafanyibiashara wa Misri. Wengine wanasema kuwa aligharamika sana hadi dhahabu alizokuwa nazo zikaisha. Lucy Duran wa Shule ya African and Oriental Studies mjini London anasema kwamba wanahistoria wa Mali walikasirishwa naye. ''Alitoa dhahabu nyingi ya Mali hali ambayo iliwafanya wanahistoria hao kutomsifu katika nyimbo zao na hadithi kwa kuwa wanaona kwamba alipoteza mali nyingi ya taifa hilo nje ya ufalme wake'', alisema. . SHUKRANI 🙏🙏🙏🙏🙏
    Like
    1
    ·40 Visualizações
  • NDOTO YA MWANA MFALME WA SAUD ARABIA YA KUJENGA MJI UNAOJITEGEMEA KWA KILA KITU INAELEKEA KUTIMIA
    .
    .
    Mwana wa mfalme wa saud Arabia MOHAMMED BIN SALMAN alifikia uamuzi huo baada ya kutembelea ukanda wa kusinimagharibi mwa SAUDI ARABIA na kujionea eneo kubwa likiwa kame na lisilo na mvuto.Mradi huo utagharimu zaidi ya dola za kimarekani billioni miatano (500$) hii ni zaidi ya mara mia mbili ya bajeti ya Tanzania watu wanapesa bhana......
    .
    .
    Mradi huo utachukua maili za mraba elfu kumi (10,000 square miles) na katika huo mji vitu vingi vitakuwa ni BANDIA yaani vitu vingi vitakuwa ni vyakuundwa na binadamu kuanzia mchanga, mwezi nk.
    .
    .
    Amesema amekusudia kufanya hivyo kuonyesha na kuushangaza ulimwengu kwa kutoa wazo zuri na litakalo tukuzwa na kila mtu
    .
    .
    VITU VITAKAVYO KUWEPO HUMO
    .
    .
    MWEZI BANDIA (GIANT ARTIFICIAL MOON)
    Mwezi huo ndio utakuwa chanzo cha mwanga nyakati za usiku utakua ukiangaza na kutoa mwanga mkubwa kiasi kwamba usiku utakua ukionekana kama mchana.
    .
    MAGARI YANAYO PAA (FLYING CARS)
    katika mji huo kutakuwepo na magari yanayo paa ,yaani huduma nyingi za usafiri wa magari kama daladala na taxi zitakuwa zinatolewa na magari yanayopaa
    .
    MCHANGA BANDIA (ARTIFICIAL SHINNING SAND)
    Mwana mfalme huyo amekusudia kutengeneza mchanga ambao utakuwa unang'aa nyakati za mchana na usiku taswila ambayo itaongeza mvuto na uzuri wa mji huo
    .
    MVUA BANDIA (ARTIFICIAL RAIN)
    Pia amekusudia kutengeneza mvua mbadala yaani mvua ambayo itakuwa ikinyesha muda wowote anaotaka haijalishi ni kiangazi wala masika.Kumbuka mji huo utajengwa kwenye jangwa lililopo pembezoni mwa SAUDI ARABIA .
    .
    WAHUDUMU MAROBOTI (ROBOT WORKERS)
    Kumbuka mji huo utakuwa kama sehemu ya kiutalii hivyo amekusudia kuajiri wafanya maroboti.Maroboti hao watakuwa wakitoa huduma mbalimbali kama kuhudumia vinywaji kwenye bar chakuka kwenye hotel na hata kuendesha baadhi ya taxi.
    .
    .
    NB
    Teknolojia ya gari zinazopaa ilisha wekwa wazi na baadhi ya wasafiri wa kinadharia (TIME TRAVELERS) wengi wa time travelers wanasema mpaka kufikia mwaka 2030 teknolojia ya magari yanayopaa itakuwa ishaanza kushamiri katika miji mingi mikubwa duniani kama TEXAS,NEW YORK CITY,PARIS,BEIJING nk
    NDOTO YA MWANA MFALME WA SAUD ARABIA YA KUJENGA MJI UNAOJITEGEMEA KWA KILA KITU INAELEKEA KUTIMIA . . Mwana wa mfalme wa saud Arabia MOHAMMED BIN SALMAN alifikia uamuzi huo baada ya kutembelea ukanda wa kusinimagharibi mwa SAUDI ARABIA na kujionea eneo kubwa likiwa kame na lisilo na mvuto.Mradi huo utagharimu zaidi ya dola za kimarekani billioni miatano (500$) hii ni zaidi ya mara mia mbili ya bajeti ya Tanzania watu wanapesa bhana...... . . Mradi huo utachukua maili za mraba elfu kumi (10,000 square miles) na katika huo mji vitu vingi vitakuwa ni BANDIA yaani vitu vingi vitakuwa ni vyakuundwa na binadamu kuanzia mchanga, mwezi nk. . . Amesema amekusudia kufanya hivyo kuonyesha na kuushangaza ulimwengu kwa kutoa wazo zuri na litakalo tukuzwa na kila mtu . . VITU VITAKAVYO KUWEPO HUMO . . 🔴 MWEZI BANDIA (GIANT ARTIFICIAL MOON) Mwezi huo ndio utakuwa chanzo cha mwanga nyakati za usiku utakua ukiangaza na kutoa mwanga mkubwa kiasi kwamba usiku utakua ukionekana kama mchana. . 🔴MAGARI YANAYO PAA (FLYING CARS) katika mji huo kutakuwepo na magari yanayo paa ,yaani huduma nyingi za usafiri wa magari kama daladala na taxi zitakuwa zinatolewa na magari yanayopaa . 🔴MCHANGA BANDIA (ARTIFICIAL SHINNING SAND) Mwana mfalme huyo amekusudia kutengeneza mchanga ambao utakuwa unang'aa nyakati za mchana na usiku taswila ambayo itaongeza mvuto na uzuri wa mji huo . 🔴MVUA BANDIA (ARTIFICIAL RAIN) Pia amekusudia kutengeneza mvua mbadala yaani mvua ambayo itakuwa ikinyesha muda wowote anaotaka haijalishi ni kiangazi wala masika.Kumbuka mji huo utajengwa kwenye jangwa lililopo pembezoni mwa SAUDI ARABIA . . 🔴WAHUDUMU MAROBOTI (ROBOT WORKERS) Kumbuka mji huo utakuwa kama sehemu ya kiutalii hivyo amekusudia kuajiri wafanya maroboti.Maroboti hao watakuwa wakitoa huduma mbalimbali kama kuhudumia vinywaji kwenye bar chakuka kwenye hotel na hata kuendesha baadhi ya taxi. . . NB Teknolojia ya gari zinazopaa ilisha wekwa wazi na baadhi ya wasafiri wa kinadharia (TIME TRAVELERS) wengi wa time travelers wanasema mpaka kufikia mwaka 2030 teknolojia ya magari yanayopaa itakuwa ishaanza kushamiri katika miji mingi mikubwa duniani kama TEXAS,NEW YORK CITY,PARIS,BEIJING nk
    Like
    1
    ·19 Visualizações
  • MAMBO 8 YA KUSHANGAZA YANAYOFANYWA NA MWILI WAKO KUKULINDA PASIPO WEWE KUJUA.

    C&P

    Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa.

    Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote 7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu.

    Yafuatayo ni mambo yanayofanywa na mwili ambayo ni kati ya hiyo mifumo ya ulinzi wa mwili wa binadamu.

    1. KUPIGA MIAYO (YAWNING)
    Lengo kubwa la kupiga muayo ni kuupoza ubongo baada ya joto kuzidi kwenye ubongo au baada ya ubongo kuchoka kufanya kazi.

    Vile vile kama ukiwa umechoka au una njaa husabababisha oxygen kupungua kwenye damu na kwenye mapafu, hii hupelekea tatizo la kupumua, hivyo kupiga miayo husaidia kuingiza oxygen ya ziada mwilini ili irudishe mwili katika hali yake ya kawaida.

    2. KUPIGA CHAFYA (SNEEZING)
    Mara nyingi tunapiga chafya pale pua zetu zinapokua zimejaa bakteria wa magonjwa ambao hawahitajiki mwilini, Vumbi pamoja na takataka mbali mbali zilizoingia kupitia pua.

    Hivyo kupiga chafya ni kitenda cha mwili kujisafisha kwa kuyatoa hayo matakataka nje yaliyoingia mwilini.

    3. KUJINYOOSHA (STRETCHING)
    Kuninyoosha mwili ni kitendo kisicho cha hiari ambacho lengo lake ni kuuandaa mwili kwa ajili ya kazi mbalimbali za kutumia nguvu utakazokabiliana nazo kwa siku nzima. Lakini pia kujinyoosha kunaipa misuli ya mwili mazoezi na kuiweka sawa vilevile kunarudisha mzunguko wa damu katika hali yake ya kawaida na kumtoa mtu katika uchovu.

    4. KWIKWI (HICCUPING)
    Najua umewahi kupata kwikwi, na mara nyingi mara baada ya kumaliza kula chakula. Je umeshawahi kujiuliza ile sauti ya ajabu ya kwikwi inasababishwa na nini au kwa sabababu gani watu hushikwa na kwikwi?

    Hiyo yote husababishwa na DIAPHRAGM (tamka DAYA - FRAM) kiungo kinachopatikana ndani ya mwili wa binadamu chini kabisa ya kifua baada ya mapafu(lungs). Kazi kubwa ya diaphragm ni kusaidia katika upumuaji, (inhale) na (exhale). Pale unapoingiza hewa ndani (inhale) diaphragm hushuka chini ili kusaidia kuivuta hewa ifike kwenye mapafu. Na unapotoa hewa nje (exhale) diaphragm hutulia kwa kubakia sehem yake ili kuwezesha hewa chafu kutoka nje kupitia pua na mdomo.

    Sasa basi, kuna wakati diaphragm kubugudhiwa na kuisababisha kushuka chini kwa kasi sana jambo linalosababisha wewe kuvuta hewa (inhale) kwa kasi isiyo ya kawaida kupitia koromeo la sauti, hewa ikifika kwenye box la sauti (larynx), sehem hiyo hujifunga kwa haraka sana ili kuzuia hewa isipite huko na ndipo KWIKWI hutokea.

    Mambo mengine yanayoweza kuibugudhi diaphragm na kuisababisha kufanya kazi vibaya mpaka kupelekea kwikwi ni kitendo cha kula haraka haraka au kuvimbewa.

    5. KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI.
    Je umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada ya kukaa sana kwenye maji?

    Watu wengi kabla walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na maji kuingia kwenye ngozi na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa.

    Lakini wanasayansi baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini hasa hupelekea ngozi kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi kulowana. Na walikuja na majibu haya.

    Mwili unapokutana na majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri kwamba mazingira hayo yana UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono kushindwa kushika (Grip) au kukamata vitu kwa urahisi kutokana na utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya haraka kuikunja ngozi ya mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu vinavyoteleza ndani ya maji pamoja na kutembea kwenye utelezi.

    6. VIPELE VIPELE VYA BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS)
    Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana.

    7. MACHOZI (TEARS)
    Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka zunguka (blink).

    Vilevile machozi yana kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa mwilini. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo (stress) mwili hutengeneza kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu maumivu yote ambayo mtu anajisikia. Hivyo machozi yanayozalishwa hapa huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL PAINKILLER. Machozi haya ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la kuzalishwa ni kwa ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini

    Hivyo mpaka hapa tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni
    i. Basal tears (vilainishi)
    ii. Reflex tears (mlinzi)
    iii. Emotion tears (mtuliza maumivu)

    8. KUSHTUKA USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK).
    Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote?

    Basi usiogope au kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya mwili.na ni njia moja wapo katika ile mifumo ya mwili kujilinda.

    Je hutokeaje?

    Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu mara tu wamejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na mtu hushtuka katika hali kama vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza kupelekea mtu hata kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini.

    Wanasayansi wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua, misuli inatulia kwa ku-relax, Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's misinterpretation of muscle relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida.

    Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa na jasho jingi.

    Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia hukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kuna tatizo gani?

    MWILI WAKO NI ZAIDI YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.

    Share pia wengine wajue sio kila kitu ni uchawi
    MAMBO 8 YA KUSHANGAZA YANAYOFANYWA NA MWILI WAKO KUKULINDA PASIPO WEWE KUJUA. C&P Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa. Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote 7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu. Yafuatayo ni mambo yanayofanywa na mwili ambayo ni kati ya hiyo mifumo ya ulinzi wa mwili wa binadamu. 1. KUPIGA MIAYO (YAWNING) Lengo kubwa la kupiga muayo ni kuupoza ubongo baada ya joto kuzidi kwenye ubongo au baada ya ubongo kuchoka kufanya kazi. Vile vile kama ukiwa umechoka au una njaa husabababisha oxygen kupungua kwenye damu na kwenye mapafu, hii hupelekea tatizo la kupumua, hivyo kupiga miayo husaidia kuingiza oxygen ya ziada mwilini ili irudishe mwili katika hali yake ya kawaida. 2. KUPIGA CHAFYA (SNEEZING) Mara nyingi tunapiga chafya pale pua zetu zinapokua zimejaa bakteria wa magonjwa ambao hawahitajiki mwilini, Vumbi pamoja na takataka mbali mbali zilizoingia kupitia pua. Hivyo kupiga chafya ni kitenda cha mwili kujisafisha kwa kuyatoa hayo matakataka nje yaliyoingia mwilini. 3. KUJINYOOSHA (STRETCHING) Kuninyoosha mwili ni kitendo kisicho cha hiari ambacho lengo lake ni kuuandaa mwili kwa ajili ya kazi mbalimbali za kutumia nguvu utakazokabiliana nazo kwa siku nzima. Lakini pia kujinyoosha kunaipa misuli ya mwili mazoezi na kuiweka sawa vilevile kunarudisha mzunguko wa damu katika hali yake ya kawaida na kumtoa mtu katika uchovu. 4. KWIKWI (HICCUPING) Najua umewahi kupata kwikwi, na mara nyingi mara baada ya kumaliza kula chakula. Je umeshawahi kujiuliza ile sauti ya ajabu ya kwikwi inasababishwa na nini au kwa sabababu gani watu hushikwa na kwikwi? Hiyo yote husababishwa na DIAPHRAGM (tamka DAYA - FRAM) kiungo kinachopatikana ndani ya mwili wa binadamu chini kabisa ya kifua baada ya mapafu(lungs). Kazi kubwa ya diaphragm ni kusaidia katika upumuaji, (inhale) na (exhale). Pale unapoingiza hewa ndani (inhale) diaphragm hushuka chini ili kusaidia kuivuta hewa ifike kwenye mapafu. Na unapotoa hewa nje (exhale) diaphragm hutulia kwa kubakia sehem yake ili kuwezesha hewa chafu kutoka nje kupitia pua na mdomo. Sasa basi, kuna wakati diaphragm kubugudhiwa na kuisababisha kushuka chini kwa kasi sana jambo linalosababisha wewe kuvuta hewa (inhale) kwa kasi isiyo ya kawaida kupitia koromeo la sauti, hewa ikifika kwenye box la sauti (larynx), sehem hiyo hujifunga kwa haraka sana ili kuzuia hewa isipite huko na ndipo KWIKWI hutokea. Mambo mengine yanayoweza kuibugudhi diaphragm na kuisababisha kufanya kazi vibaya mpaka kupelekea kwikwi ni kitendo cha kula haraka haraka au kuvimbewa. 5. KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI. Je umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada ya kukaa sana kwenye maji? Watu wengi kabla walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na maji kuingia kwenye ngozi na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa. Lakini wanasayansi baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini hasa hupelekea ngozi kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi kulowana. Na walikuja na majibu haya. Mwili unapokutana na majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri kwamba mazingira hayo yana UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono kushindwa kushika (Grip) au kukamata vitu kwa urahisi kutokana na utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya haraka kuikunja ngozi ya mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu vinavyoteleza ndani ya maji pamoja na kutembea kwenye utelezi. 6. VIPELE VIPELE VYA BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS) Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana. 7. MACHOZI (TEARS) Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka zunguka (blink). Vilevile machozi yana kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa mwilini. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo (stress) mwili hutengeneza kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu maumivu yote ambayo mtu anajisikia. Hivyo machozi yanayozalishwa hapa huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL PAINKILLER. Machozi haya ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la kuzalishwa ni kwa ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini Hivyo mpaka hapa tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni i. Basal tears (vilainishi) ii. Reflex tears (mlinzi) iii. Emotion tears (mtuliza maumivu) 8. KUSHTUKA USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK). Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote? Basi usiogope au kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya mwili.na ni njia moja wapo katika ile mifumo ya mwili kujilinda. Je hutokeaje? Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu mara tu wamejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na mtu hushtuka katika hali kama vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza kupelekea mtu hata kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini. Wanasayansi wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua, misuli inatulia kwa ku-relax, Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's misinterpretation of muscle relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida. Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa na jasho jingi. Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia hukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kuna tatizo gani? MWILI WAKO NI ZAIDI YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO. Share pia wengine wajue sio kila kitu ni uchawi
    ·21 Visualizações
  • Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limewaonya wananchi waliotaka kumshambulia mwananchi mmoja wakimtuhumu kuwa ni mbakaji maarufu kwa jina la ‘Teleza’.

    Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema kumekuwa na uvumi wa taarifa potofu zinazoenezwa kwenye maeneo hususan Kata ya Mkolani na Buhongwa mkoani humo zikieleza juu ya mtu aitwaye Teleza anayedaiwa kubaka, kulawiti wanawake pamoja na kuwajeruhi.

    Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limewaonya wananchi waliotaka kumshambulia mwananchi mmoja wakimtuhumu kuwa ni mbakaji maarufu kwa jina la ‘Teleza’. Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema kumekuwa na uvumi wa taarifa potofu zinazoenezwa kwenye maeneo hususan Kata ya Mkolani na Buhongwa mkoani humo zikieleza juu ya mtu aitwaye Teleza anayedaiwa kubaka, kulawiti wanawake pamoja na kuwajeruhi.
    Like
    1
    ·14 Visualizações
  • Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limethibitisha kumshikilia aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa kwa ajili ya mahojiano ya baadhi ya mambo.

    Kamanda Jumanne Muliro ambaye hakuweka wazi sababu za kumshikilia, amesema mahojiano yanakwenda vizuri, hivyo wanaangalia mifumo ya kisheria itakayowaelekeza nini cha kufanya.
    Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limethibitisha kumshikilia aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa kwa ajili ya mahojiano ya baadhi ya mambo. Kamanda Jumanne Muliro ambaye hakuweka wazi sababu za kumshikilia, amesema mahojiano yanakwenda vizuri, hivyo wanaangalia mifumo ya kisheria itakayowaelekeza nini cha kufanya.
    Like
    1
    1 Comentários ·14 Visualizações
  • “Mimi nina haki ya kuhukumiwa [kwenye uchaguzi] kwa kazi niliyoifanya. Kama nitahukumiwa kwamba nimeiumiza CHADEMA nimeifelisha CHADEMA, nina haki ya kuhukumiwa. Kwahiyo maamuzi hayo nawaachia wajumbe wa mkutano mkuu wafanye maamuzi.” – Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
    “Mimi nina haki ya kuhukumiwa [kwenye uchaguzi] kwa kazi niliyoifanya. Kama nitahukumiwa kwamba nimeiumiza CHADEMA nimeifelisha CHADEMA, nina haki ya kuhukumiwa. Kwahiyo maamuzi hayo nawaachia wajumbe wa mkutano mkuu wafanye maamuzi.” – Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
    Like
    1
    ·12 Visualizações
  • “Kazi niliyoifanya CHADEMA inapimika na dunia yote inaona. Kwa yeyote mwenye akili timamu na nia njema, ataona kazi niliyoifanya" - Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
    “Kazi niliyoifanya CHADEMA inapimika na dunia yote inaona. Kwa yeyote mwenye akili timamu na nia njema, ataona kazi niliyoifanya" - Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
    Like
    1
    ·13 Visualizações
  • Zuchu✍
    Zuchu✍
    ·39 Visualizações
  • ·36 Visualizações
  • ·35 Visualizações