• 0 Comments ·0 Shares ·8 Views
  • Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·8 Views
  • Mkutano wa Kilele wa Marais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika hivi karibuni umemtaka Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, kukaa meza moja na Waasi wa M23 kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja ili kutafuta suluhu ya amani katika taifa hilo.

    Taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano huo, ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (Twitter), ilieleza kuwa Viongozi hao walikutana Januari 29, chini ya Uenyekiti wa Rais wa Kenya, William Ruto, kujadili hali ya usalama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

    Miongoni mwa makubaliano ya mkutano huo ni pendekezo la Rais Tshisekedi kushiriki mazungumzo na kundi la M23. Kadhalika, Viongozi hao walikubaliana kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapaswa kuitisha mkutano wa dharura na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kutafuta suluhisho la kudumu kwa mgogoro huo.

    Museveni aliambatanisha taarifa hiyo na orodha ya Viongozi waliohudhuria mkutano huo, wakiwemo Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Somalia Hassan Mohamud, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Rwanda Paul Kagame, na mwenyeji wao, Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

    Mkutano wa Kilele wa Marais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika hivi karibuni umemtaka Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, kukaa meza moja na Waasi wa M23 kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja ili kutafuta suluhu ya amani katika taifa hilo. Taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano huo, ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (Twitter), ilieleza kuwa Viongozi hao walikutana Januari 29, chini ya Uenyekiti wa Rais wa Kenya, William Ruto, kujadili hali ya usalama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Miongoni mwa makubaliano ya mkutano huo ni pendekezo la Rais Tshisekedi kushiriki mazungumzo na kundi la M23. Kadhalika, Viongozi hao walikubaliana kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapaswa kuitisha mkutano wa dharura na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kutafuta suluhisho la kudumu kwa mgogoro huo. Museveni aliambatanisha taarifa hiyo na orodha ya Viongozi waliohudhuria mkutano huo, wakiwemo Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Somalia Hassan Mohamud, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Rwanda Paul Kagame, na mwenyeji wao, Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·45 Views
  • Jeshi la Uganda (UPDF) limesema Wanajeshi wake walioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , watatafuta mbinu ya kujiimarisha kiulinzi ili kuyazuwia makundi mengine ya Waasi kuingia mashariki mwa Taifa hilo.

    Hali inazidi kuwa tete mashariki mwa Kongo, huku Waasi wa kujndi la M23 wanaosemekana kuungwa mkono na Rwanda wakiendelea kuyadhibiti maeneo kadhaa ya eneo hilo ukiwemo Mji wa Goma, hali iliyoisababisha Uganda kupitia Jeshi lake kusema inataka kujipanga upya kiulinzi, katika eneo inayofanyia operesheni zake hadi mzozo huo wa DR Congo utakapotulia. Imesema nia yake ni kuyazuwia makundi mengine ya Waasi yasitumie mwanya wa vita kuingia mashariki mwa Taifa hilo. 

    Nchi ya Uganda ina jukumu muhimu katika kanda hiyo. Inafanya kazi pamoja na Wanajeshi wa Kongo katika mpango wa Operesheni Shujaa dhidi ya makundi yaliyo na itikadi kali kama Allied Democratic Forces, ADF, ambalo limekuwa likifungamanishwa na kundi la dola la kiislamu. Lakini kando na hayo, Uganda pia imekuwa ikishutumiwa na Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kwa kuwaunga mkono Waasi wa M23 kwa kuwaruhusu kutumia ardhi yake kupitisha silaha zake madai ambayo Uganda imeyakanusha vikali.

    Jeshi la Uganda 🇺🇬 (UPDF) limesema Wanajeshi wake walioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, watatafuta mbinu ya kujiimarisha kiulinzi ili kuyazuwia makundi mengine ya Waasi kuingia mashariki mwa Taifa hilo. Hali inazidi kuwa tete mashariki mwa Kongo, huku Waasi wa kujndi la M23 wanaosemekana kuungwa mkono na Rwanda 🇷🇼 wakiendelea kuyadhibiti maeneo kadhaa ya eneo hilo ukiwemo Mji wa Goma, hali iliyoisababisha Uganda kupitia Jeshi lake kusema inataka kujipanga upya kiulinzi, katika eneo inayofanyia operesheni zake hadi mzozo huo wa DR Congo utakapotulia. Imesema nia yake ni kuyazuwia makundi mengine ya Waasi yasitumie mwanya wa vita kuingia mashariki mwa Taifa hilo.  Nchi ya Uganda ina jukumu muhimu katika kanda hiyo. Inafanya kazi pamoja na Wanajeshi wa Kongo katika mpango wa Operesheni Shujaa dhidi ya makundi yaliyo na itikadi kali kama Allied Democratic Forces, ADF, ambalo limekuwa likifungamanishwa na kundi la dola la kiislamu. Lakini kando na hayo, Uganda pia imekuwa ikishutumiwa na Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kwa kuwaunga mkono Waasi wa M23 kwa kuwaruhusu kutumia ardhi yake kupitisha silaha zake madai ambayo Uganda imeyakanusha vikali.
    0 Comments ·0 Shares ·40 Views
  • Mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) umesema lengo la Wanachama wa Jumuiya hiyo ni kuona amani inarejea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

    Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Zimbabwe , Emmerson Mnangagwa ambaye ni Mwenyekiti wa SADC wakati wa mkutano wa dharura wa Jumuiya hiyo ulioitishwa Jijini Harare, Zimbabwe kwa lengo la kujadili kutetereka kwa amani Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Hali ya usalama ilianza kuyumba Nchini Kongo baada ya kundi la Waasi wa M23 kuanza uvamizi na kuyashikilia maeneo ya mashariki mwa Kongo ikiwemo Mji wa Goma. Kwa mujibu wa Mnangagwa, suala la ulinzi wa Raia Nchini humo si la hiari, bali la kisheria kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa na Nchi Wanachama wa SADC.

    “Ni kwa bahati mbaya nasema kwamba tangu mkutano wetu wa mwisho hali ya amani imetetereka nchini DRC. Mashambulizi ya M23 yamegharimu maisha ya wanajeshi wetu wanaolinda amani DRC chini ya SAMIDRC na kuwaacha wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya,” - Mnangagwa.

    Amempongeza Rais wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua hatua za haraka za kuitisha mkutano wa dharura na Wakuu wa Nchi na Serikali kupitia Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Troika).

    Mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) umesema lengo la Wanachama wa Jumuiya hiyo ni kuona amani inarejea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Zimbabwe 🇿🇼, Emmerson Mnangagwa ambaye ni Mwenyekiti wa SADC wakati wa mkutano wa dharura wa Jumuiya hiyo ulioitishwa Jijini Harare, Zimbabwe kwa lengo la kujadili kutetereka kwa amani Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hali ya usalama ilianza kuyumba Nchini Kongo baada ya kundi la Waasi wa M23 kuanza uvamizi na kuyashikilia maeneo ya mashariki mwa Kongo ikiwemo Mji wa Goma. Kwa mujibu wa Mnangagwa, suala la ulinzi wa Raia Nchini humo si la hiari, bali la kisheria kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa na Nchi Wanachama wa SADC. “Ni kwa bahati mbaya nasema kwamba tangu mkutano wetu wa mwisho hali ya amani imetetereka nchini DRC. Mashambulizi ya M23 yamegharimu maisha ya wanajeshi wetu wanaolinda amani DRC chini ya SAMIDRC na kuwaacha wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya,” - Mnangagwa. Amempongeza Rais wa Tanzania 🇹🇿, Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua hatua za haraka za kuitisha mkutano wa dharura na Wakuu wa Nchi na Serikali kupitia Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Troika).
    0 Comments ·0 Shares ·46 Views
  • 0 Comments ·0 Shares ·6 Views
  • Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·5 Views
  • 0 Comments ·0 Shares ·5 Views
  • 0 Comments ·0 Shares ·5 Views
  • Kama utafuatilia kwa undani kinachoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , lazima utagundua kuwa Nchi ya Kongo ilikua na kila sababu kuweza kudhibiti hali ya Mashariki mwa Taifa hilo ila kutokana na mipango mibovu na kutegemea misaada na uthaifu wa Viongozi wa Nchi akiwemo Raisi Félix Tshisekedi ndio maana waliodharauliwa sasa wanasonga mbele kwa namna isiyo ya kawaida.

    Toka Rais Tshisekedi aingia madarakani mwaka 2018 ni mambo yapi ya kimkakati amefanya ili kuhakikisha anakomesha makundi ya uasi mashariki mwa Kongo utabaini hakuna, yeye anaongoza tu akiwa Kinshasa ukanda wa mashariki ni kama amewasusa hali imezidi kuwa mbaya. Hajafanikiwa kubadili upepo kwa namna yoyote sio kijeshi wala kimazungumzo.

    Mojawapo ya jukumu kuu la Rais wa Nchi yoyote Duniani ni kuhakikisha usalama na amani ya Raia anaowaongoza, sasa Tshisekedi zaidi ya miaka saba (7) sasa yupo madarakani huku Raia wakiendelea kuteswa na vita Mashariki mwa Nchi hiyo huku yeye akiwa hana jipya alilofanya kama Rais kuwanusuru Raia wake, sasa hapo mnatarajia nini kama sio kuvamiwa?

    Kilichotokea na kinachoelea kwa sasa hivi Nchini Kongo, Viongozi Wakuu wanapaswa kujilaumu wenyewe, maadui zao wanatumia udhaifu wa kimkakati na kufanikisha ajenda zao.Tshisekedi alipaswa baada ya kutwaa Urais tu angehakikisha nguvu kubwa na mipango anaelekeza Mashariki mwa Nchi kwa sababu kule ndipo kwenye changamoto kubwa Nchini Kongo ila hadi sasa anatoa hotuba za kuilaumu Rwanda tu, yeye hajaja na mpango kwamba amejipanga vipi kukomesha uasi eneo hilo la mashariki na kuweka amani ya kudumu.

    Inashauriwa kabla ya kutaka uongozi wa juu wa Nchi, jipime kwanza. Je, wanafaa? utaweza majukumu? au unafikiri kuongoza Nchi ni rahisi tu kama kumsukuma Mlevi kwenye shimo!

    Kwa kumalizia, kama Kongo ingekuwa na uongozi thabiti, wenye maono, nguvu, mipango na mikakati madhubuti kupitia tu Jeshi la ndani ilikua na uwezo wa kukomesha Maadui wote. Mipaka ya Kongo inaimgilika kama maji ya kunywa, misitu kama yote haina uangalizi au ulinzi wowote ule. Tuendelee kuiombea Nchi ya Kongo ipate kwanza Viongozi bora na sio bora Viongozi.

    Kama utafuatilia kwa undani kinachoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, lazima utagundua kuwa Nchi ya Kongo ilikua na kila sababu kuweza kudhibiti hali ya Mashariki mwa Taifa hilo ila kutokana na mipango mibovu na kutegemea misaada na uthaifu wa Viongozi wa Nchi akiwemo Raisi Félix Tshisekedi ndio maana waliodharauliwa sasa wanasonga mbele kwa namna isiyo ya kawaida. Toka Rais Tshisekedi aingia madarakani mwaka 2018 ni mambo yapi ya kimkakati amefanya ili kuhakikisha anakomesha makundi ya uasi mashariki mwa Kongo utabaini hakuna, yeye anaongoza tu akiwa Kinshasa ukanda wa mashariki ni kama amewasusa hali imezidi kuwa mbaya. Hajafanikiwa kubadili upepo kwa namna yoyote sio kijeshi wala kimazungumzo. Mojawapo ya jukumu kuu la Rais wa Nchi yoyote Duniani ni kuhakikisha usalama na amani ya Raia anaowaongoza, sasa Tshisekedi zaidi ya miaka saba (7) sasa yupo madarakani huku Raia wakiendelea kuteswa na vita Mashariki mwa Nchi hiyo huku yeye akiwa hana jipya alilofanya kama Rais kuwanusuru Raia wake, sasa hapo mnatarajia nini kama sio kuvamiwa? Kilichotokea na kinachoelea kwa sasa hivi Nchini Kongo, Viongozi Wakuu wanapaswa kujilaumu wenyewe, maadui zao wanatumia udhaifu wa kimkakati na kufanikisha ajenda zao.Tshisekedi alipaswa baada ya kutwaa Urais tu angehakikisha nguvu kubwa na mipango anaelekeza Mashariki mwa Nchi kwa sababu kule ndipo kwenye changamoto kubwa Nchini Kongo ila hadi sasa anatoa hotuba za kuilaumu Rwanda tu, yeye hajaja na mpango kwamba amejipanga vipi kukomesha uasi eneo hilo la mashariki na kuweka amani ya kudumu. Inashauriwa kabla ya kutaka uongozi wa juu wa Nchi, jipime kwanza. Je, wanafaa? utaweza majukumu? au unafikiri kuongoza Nchi ni rahisi tu kama kumsukuma Mlevi kwenye shimo! Kwa kumalizia, kama Kongo ingekuwa na uongozi thabiti, wenye maono, nguvu, mipango na mikakati madhubuti kupitia tu Jeshi la ndani ilikua na uwezo wa kukomesha Maadui wote. Mipaka ya Kongo inaimgilika kama maji ya kunywa, misitu kama yote haina uangalizi au ulinzi wowote ule. Tuendelee kuiombea Nchi ya Kongo ipate kwanza Viongozi bora na sio bora Viongozi.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·41 Views