• #PART2

    Na kweli, wakampigia kura, Obama akaingia madarakani.

    Mwaka wa kwanza ukapita.
    Mwaka wa pili ukapita.
    Mwaka wa tatu ukapita.

    Gereza bado liko palepale.

    Kila alipoulizwa juu ya ahadi yake, alitoa majibu yasiyoeleweka.

    Ndani ya miaka yake minane madarakani, Guantanamo Bay liliendelea kuwepo.

    Ndipo Wamarekani wakagundua kitu.
    Hata Rais hana nguvu juu ya gereza hili.

    Wakati Trump akaingia madarakani, yeye hakutumia Guantanamo kama njia ya kuombea kura.

    Hakusema atalifunga.
    Hakusema atalifungua.

    Lakini alipoingia, akatoa amri ya kuhamisha wafungwa zaidi ya 30,000.

    Lengo lake lilikuwa moja tu.

    "Tuhakikishe gereza linajaa wale ambao kweli wanastahili kuwepo humo."
    #PART2 Na kweli, wakampigia kura, Obama akaingia madarakani. Mwaka wa kwanza ukapita. Mwaka wa pili ukapita. Mwaka wa tatu ukapita. Gereza bado liko palepale. Kila alipoulizwa juu ya ahadi yake, alitoa majibu yasiyoeleweka. Ndani ya miaka yake minane madarakani, Guantanamo Bay liliendelea kuwepo. Ndipo Wamarekani wakagundua kitu. Hata Rais hana nguvu juu ya gereza hili. Wakati Trump akaingia madarakani, yeye hakutumia Guantanamo kama njia ya kuombea kura. Hakusema atalifunga. Hakusema atalifungua. Lakini alipoingia, akatoa amri ya kuhamisha wafungwa zaidi ya 30,000. Lengo lake lilikuwa moja tu. "Tuhakikishe gereza linajaa wale ambao kweli wanastahili kuwepo humo."
    0 Comments ·0 Shares ·311 Views
  • #PART2

    Baada ya mipaka ya Wakoloni walioangukia Rwanda na Burundi waliendelea kujiita Watutsi, lakini walioangukia Congo hawakujiita Watutsi, kwa sababu ya kukwepa ubaguzi. Ili wasitengwe wakajitambulisha kwa eneo wanalotoka, safu za Milima ya Mulenge. Kwahiyo wakajiita Banyamulenge, yani watu kutoka Mulenge. Lakini ukweli ni Watutsi, wametengwa na wenzao kwa mipaka ya wakoloni.

    Ni sawa na wamassai wa Tanzania na wale wa Kenya. Ni jamii moja ila wametengwa na mipaka ya Wakoloni. Huku Tanzania Wamasai ni wengi kuliko Kenya, lakini serikali ya Kenya haiwezi kuwafukuza wa Kenya waje Tanzania. Itakua dhambi ya ubaguzi. Mipaka ilipowekwa waliojikuta Kenya wakawa raia wa Kenya hivyo, hali kadhalika waliojikuta Tanzania.

    Watutsi wa Congo pamoja na kujiita Banyamulenge, bado wakikumbana na ubaguzi. Hawakupata ushirikiano kutoka kwa jamii nyingine za Kivu. Kwahiyo wakajikuta wameongeza "bond" na Watutsi wa Rwanda. Kukawa na mwingiliano mkubwa kati ya Watutsi wa Rwanda na wale wa Congo (Banyamulenge).

    Mwaka 1959, mfalme wa mwisho wa Rwanda, Mutara III, aliuawa kwa sumu. Baada ya kifo chake, Rwanda iliingia katika machafuko ambapo Wahutu waliokuwa zaidi ya 80% waliwashambulia Watutsi, wakiwatuhumu kupendelewa na Wakoloni wa Kibelgiji. Maelfu ya Watutsi walikimbilia Kivu kwa ajili ya usalama wao. Walipofika huko, waliungana na wenzao (Banyamulenge), idadi ikaongezeka.

    Mwaka 1962, Rwanda ilipata uhuru, na Gregoire Kayibanda akawa Rais. Kwa mara ya kwanza, Wahutu walishika madaraka baada ya utawala wa kifalme wa Watutsi kwa miaka mingi. Kayibanda alikakandamiza Watutsi na kupendelea Wahutu wenzake. Watutsi wengi walikimbilia uhamishoni, hasa maeneo ya Kivu. Wakaenda kuungana na wenzao (Banyamulenge).

    Mwaka 1973, Kayibanda alipinduliwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Juvénal Habyarimana, ambaye alijiapiza kuwatokomeza Watutsi. Kwa miaka 21 ya utawala wake, Watutsi waliteswa vikali. Waliondolewa kwenye nafasi za kijeshi, mashirika ya umma, na siasa. Wengi walifungwa gerezani au kuuawa. Hali hii iliwafanya Watutsi wengi zaidi kukimbia Rwanda na kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Kivu. Walioenda Kivu wakaenda kuongeza idadi ya Banyamulenge.!
    (Malisa GJ)

    #PART2 Baada ya mipaka ya Wakoloni walioangukia Rwanda na Burundi waliendelea kujiita Watutsi, lakini walioangukia Congo hawakujiita Watutsi, kwa sababu ya kukwepa ubaguzi. Ili wasitengwe wakajitambulisha kwa eneo wanalotoka, safu za Milima ya Mulenge. Kwahiyo wakajiita Banyamulenge, yani watu kutoka Mulenge. Lakini ukweli ni Watutsi, wametengwa na wenzao kwa mipaka ya wakoloni. Ni sawa na wamassai wa Tanzania na wale wa Kenya. Ni jamii moja ila wametengwa na mipaka ya Wakoloni. Huku Tanzania Wamasai ni wengi kuliko Kenya, lakini serikali ya Kenya haiwezi kuwafukuza wa Kenya waje Tanzania. Itakua dhambi ya ubaguzi. Mipaka ilipowekwa waliojikuta Kenya wakawa raia wa Kenya hivyo, hali kadhalika waliojikuta Tanzania. Watutsi wa Congo pamoja na kujiita Banyamulenge, bado wakikumbana na ubaguzi. Hawakupata ushirikiano kutoka kwa jamii nyingine za Kivu. Kwahiyo wakajikuta wameongeza "bond" na Watutsi wa Rwanda. Kukawa na mwingiliano mkubwa kati ya Watutsi wa Rwanda na wale wa Congo (Banyamulenge). Mwaka 1959, mfalme wa mwisho wa Rwanda, Mutara III, aliuawa kwa sumu. Baada ya kifo chake, Rwanda iliingia katika machafuko ambapo Wahutu waliokuwa zaidi ya 80% waliwashambulia Watutsi, wakiwatuhumu kupendelewa na Wakoloni wa Kibelgiji. Maelfu ya Watutsi walikimbilia Kivu kwa ajili ya usalama wao. Walipofika huko, waliungana na wenzao (Banyamulenge), idadi ikaongezeka. Mwaka 1962, Rwanda ilipata uhuru, na Gregoire Kayibanda akawa Rais. Kwa mara ya kwanza, Wahutu walishika madaraka baada ya utawala wa kifalme wa Watutsi kwa miaka mingi. Kayibanda alikakandamiza Watutsi na kupendelea Wahutu wenzake. Watutsi wengi walikimbilia uhamishoni, hasa maeneo ya Kivu. Wakaenda kuungana na wenzao (Banyamulenge). Mwaka 1973, Kayibanda alipinduliwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Juvénal Habyarimana, ambaye alijiapiza kuwatokomeza Watutsi. Kwa miaka 21 ya utawala wake, Watutsi waliteswa vikali. Waliondolewa kwenye nafasi za kijeshi, mashirika ya umma, na siasa. Wengi walifungwa gerezani au kuuawa. Hali hii iliwafanya Watutsi wengi zaidi kukimbia Rwanda na kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Kivu. Walioenda Kivu wakaenda kuongeza idadi ya Banyamulenge.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·589 Views