• #PART7

    Baada ya kundi la RCD kuvunjika, yalizaliwa makundi mawili ambayo ni RCD Goma (liliungwa mkono na Rwanda) na RCD Kisangani (likiungwa mkono na Uganda). Aliyekua Kiongozi wa RCD Ernest Wamba Dia Wamba akaamua kukaa pembeni baada ya kugundua wanatumika kupigana kwa maslahi ya watu wengine.

    Kwahiyo makundi haya yakapata viongozi wapya. RCD-Goma ikaongozwa na Kanali Emile Ilunga na RCD-Kisangani, ikaongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi. Ikumbukwe kabla kundi la RCD halijavunjika, lilikuwa limeshikilia maeneo mengi ya migodi huko Goma, Bukavu, na Katanga. Sasa baada ya kuvunjika, ukatokea mgogoro wa kugawana maeneo. Mgodi upi uende RCD Goma na upi uende RCD Kisangani.

    Kwa hiyo wakaanza kupigana tena wao kwa wao. Ikapigwa vita moja kali sana pale Kisangani, ikabatizwa jina la ‘Six Day War’ maana ilipiganwa kwa siku sita. RCD-Goma, ikawatandika vibaya sana RCD-Kisangani. Tar.10 June 2000 RCD Kisangani ikaachia migodi yote na kukimbia. RCD-Goma wakataka RCD-Kisangani wabadili jina lao maana mji wa Kisangani haukuwa chini yao tena. Hatimaye, RCD-Kisangani wakabadili na kujiita RCD-ML, yaani Rally for Congolese Democracy - Liberation Movement.

    RCD - ML walikimbilia kwenye milima Mikeno karibu na hifadhi ya Virunga kujipanga upya. RCD-Goma wakaendeleza mapigano kuelekea Kinshasa. Lakini kufika Bukavu wakakumbana na upinzani kutoka wanamgambo wa Maï-Maï waliokua wamepewa silaha na serikali za majimbo kupigana na askari yoyote mgeni kwenye ardhi yao.

    Maï-Maï waliongozwa na Kanali Musa Sindi upande wa Kivu Kusini na Sheikh Ntabo Ntaberi kwa Kivu Kaskazini. Kwa hiyo safari ya RCD Goma kwenda Kinshasa kumng’oa Laurent Kabila ikakutana na kizuizi cha Maï-Maï. Wakachapana sana. Watu zaidi ya 1,000 wakapoteza maisha.

    Kwahiyo vita ya kumng'oa Laurent Kabila ikawa ngumu maana vikundi vingi vya waasi vilianza kupigana vyenyewe kwa vyenyewe. Hali hiyo ilifanya vita kuwa ngumu zaidi, maana watu walipigana bila mpangilio. Risasi zikafyatuliwa hovyo hovyo na wananchi wengi wakapoteza maisha.
    (Malisa GJ)

    #PART7 Baada ya kundi la RCD kuvunjika, yalizaliwa makundi mawili ambayo ni RCD Goma (liliungwa mkono na Rwanda) na RCD Kisangani (likiungwa mkono na Uganda). Aliyekua Kiongozi wa RCD Ernest Wamba Dia Wamba akaamua kukaa pembeni baada ya kugundua wanatumika kupigana kwa maslahi ya watu wengine. Kwahiyo makundi haya yakapata viongozi wapya. RCD-Goma ikaongozwa na Kanali Emile Ilunga na RCD-Kisangani, ikaongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi. Ikumbukwe kabla kundi la RCD halijavunjika, lilikuwa limeshikilia maeneo mengi ya migodi huko Goma, Bukavu, na Katanga. Sasa baada ya kuvunjika, ukatokea mgogoro wa kugawana maeneo. Mgodi upi uende RCD Goma na upi uende RCD Kisangani. Kwa hiyo wakaanza kupigana tena wao kwa wao. Ikapigwa vita moja kali sana pale Kisangani, ikabatizwa jina la ‘Six Day War’ maana ilipiganwa kwa siku sita. RCD-Goma, ikawatandika vibaya sana RCD-Kisangani. Tar.10 June 2000 RCD Kisangani ikaachia migodi yote na kukimbia. RCD-Goma wakataka RCD-Kisangani wabadili jina lao maana mji wa Kisangani haukuwa chini yao tena. Hatimaye, RCD-Kisangani wakabadili na kujiita RCD-ML, yaani Rally for Congolese Democracy - Liberation Movement. RCD - ML walikimbilia kwenye milima Mikeno karibu na hifadhi ya Virunga kujipanga upya. RCD-Goma wakaendeleza mapigano kuelekea Kinshasa. Lakini kufika Bukavu wakakumbana na upinzani kutoka wanamgambo wa Maï-Maï waliokua wamepewa silaha na serikali za majimbo kupigana na askari yoyote mgeni kwenye ardhi yao. Maï-Maï waliongozwa na Kanali Musa Sindi upande wa Kivu Kusini na Sheikh Ntabo Ntaberi kwa Kivu Kaskazini. Kwa hiyo safari ya RCD Goma kwenda Kinshasa kumng’oa Laurent Kabila ikakutana na kizuizi cha Maï-Maï. Wakachapana sana. Watu zaidi ya 1,000 wakapoteza maisha. Kwahiyo vita ya kumng'oa Laurent Kabila ikawa ngumu maana vikundi vingi vya waasi vilianza kupigana vyenyewe kwa vyenyewe. Hali hiyo ilifanya vita kuwa ngumu zaidi, maana watu walipigana bila mpangilio. Risasi zikafyatuliwa hovyo hovyo na wananchi wengi wakapoteza maisha. (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·1K Views




  • #paulswai
    😂😂 #paulswai
    Like
    Love
    4
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·918 Views ·9





  • #paulswai
    😂😂😂😂 #paulswai
    Like
    Love
    5
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·924 Views ·6
  • Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·208 Views
  • Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·206 Views
  • Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) cha Afrika Kusini kimeitaka Serikali ya Afrika Kusini kufunga ubalozi wa Rwanda Nchini humo, kikidai kuwa hakuna haja ya kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na nchi inayodhoofisha uhuru wa taifa hilo.

    Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Jumatatu, Februari 3, 2025, Kiongozi wa EFF, Julius Malema, amemtaka Rais Cyril Ramaphosa kuchukua hatua kali dhidi ya Nchi ya Rwanda endapo itabainika imehusika katika shambulio dhidi ya Wanajeshi wa Afrika Kusini waliopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa shughuli za ulinzi wa amani.

    "Haikubaliki kwa wanajeshi wetu kushiriki kwenye mzozo ambao hauleti amani katika eneo hilo. Kama itathibitishwa kuwa Rwanda ililenga vikosi vya Afrika Kusini kwa makusudi, basi Rais Cyril Ramaphosa lazima achukue hatua kali," Julius Malema, Kiongozi wa EFF.

    Aidha, Malema amesisitiza kuwa Nchi ya Afrika Kusini inapaswa kuondoa Wanajeshi wake kutoka DR Congo mara moja na kusitisha makubaliano yote ya kibiashara na Rwanda.

    "Iwapo Rwanda itathibitishwa kuhusika moja kwa moja katika mashambulizi dhidi ya wanajeshi wetu, basi makubaliano yote ya biashara na ushirikiano na nchi hiyo yafutwe mara moja. Ubalozi wa Rwanda unapaswa kufungwa bila kuchelewa," amemalizia kusema Malema.

    Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) cha Afrika Kusini 🇿🇦 kimeitaka Serikali ya Afrika Kusini kufunga ubalozi wa Rwanda Nchini humo, kikidai kuwa hakuna haja ya kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na nchi inayodhoofisha uhuru wa taifa hilo. Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Jumatatu, Februari 3, 2025, Kiongozi wa EFF, Julius Malema, amemtaka Rais Cyril Ramaphosa kuchukua hatua kali dhidi ya Nchi ya Rwanda endapo itabainika imehusika katika shambulio dhidi ya Wanajeshi wa Afrika Kusini waliopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 kwa shughuli za ulinzi wa amani. "Haikubaliki kwa wanajeshi wetu kushiriki kwenye mzozo ambao hauleti amani katika eneo hilo. Kama itathibitishwa kuwa Rwanda ililenga vikosi vya Afrika Kusini kwa makusudi, basi Rais Cyril Ramaphosa lazima achukue hatua kali," Julius Malema, Kiongozi wa EFF. Aidha, Malema amesisitiza kuwa Nchi ya Afrika Kusini inapaswa kuondoa Wanajeshi wake kutoka DR Congo mara moja na kusitisha makubaliano yote ya kibiashara na Rwanda. "Iwapo Rwanda itathibitishwa kuhusika moja kwa moja katika mashambulizi dhidi ya wanajeshi wetu, basi makubaliano yote ya biashara na ushirikiano na nchi hiyo yafutwe mara moja. Ubalozi wa Rwanda unapaswa kufungwa bila kuchelewa," amemalizia kusema Malema.
    Like
    2
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·505 Views
  • #PART8

    Kwahiyo wakati mapigano makali yakiendelea huko mashariki mwa Congo baina ya vikundi vya Waasi na wanamgambo wa Maimai, hali ikatulia mjini Kinshasa na Rais Kabila akapata nafasi ya kupumua kidogo. Maadui zako wakipigana wewe utafanya nini zaidi ya kunywa supu na chapati 2 kujipongeza?

    Lakini alichosahau Kabila ni kwamba Kagame ni Jasusi mwandamizi. Wakati wa kusaini mkataba Lemera, Kagame alimchomekea "watu wake" kwenye kikosi chake cha ulinzi. Mmojawapo ni Luteni Rashid Kasereka, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu Kusini. Januari 16, 2001, Luteni Kasereka alimfyatulia Rais Kabila risasi 4 za tumbo na kumuua papohapo.

    Jumuiya ya kimataifa ikamtuhumu Kagame kuhusika, lakini akakanusha na kusema ni madai yasiyo na msingi. Baada ya kifo cha Mzee Kabila, mwanae Joseph akaapishwa kuwa Rais akiwa na miaka 29 tu. Joseph akafanya jitihada mbalimbali za kukomesha vita kwa kushirikisha Jumuiya ya kimataifa.

    Julai 30, 2002, ukasainiwa Mkataba wa Pretoria (The Pretoria Agreement) uliotaka pande zote kusitisha mapigano. Desemba 17, 2002, ukasainiwa Mkataba mwingine ulioitwa Global &Inclusive Agreement (maarufu kama 2003 Peace Deal). Na hatimaye, Aprili 2, 2003, ukasainiwa Mkataba Maarufu wa Sun City Peace Agreement uliomaliza kabisa vita ya Congo.

    Pamoja na mambo mengine, mkataba huo ulitaka kuondolewa kwa majeshi yote ya kigeni nchini Congo, kuwepo na utaratibu wa uchaguzi wa kidemokrasia, na kuwaingiza jeshini askari wa vikundi vya waasi. Mkataba huo ulihitimisha Vita vya Pili vya Congo. Vita mbaya mno katika historia. Vita hivi vilibatizwa jina "The Great war of Africa" kwa jinsi vilivyoshirikisha mataifa mengi, na jinsi vilivyoleta madhara makubwa kwa watu ikiwemo vifo vya zaidi ya watu 500,000.

    Baada ya kumalizika kwa vita hivyo, Congo ikarudi kwenye amani, japokuwa kulikuwa na vikundi vidogo vya wanamgambo katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, hasa eneo la Kivu lakini makundi makubwa yote ya Waasi yalikubali kuweka silaha chini. Kuanzia mwaka 2003 hadi 2006 hali ikatulia kabisa. Kwa mara ya kwanza raia wa Congo wakalala pasi na kusikia milio ya risasi.!
    (Malisa GJ)

    #PART8 Kwahiyo wakati mapigano makali yakiendelea huko mashariki mwa Congo baina ya vikundi vya Waasi na wanamgambo wa Maimai, hali ikatulia mjini Kinshasa na Rais Kabila akapata nafasi ya kupumua kidogo. Maadui zako wakipigana wewe utafanya nini zaidi ya kunywa supu na chapati 2 kujipongeza? Lakini alichosahau Kabila ni kwamba Kagame ni Jasusi mwandamizi. Wakati wa kusaini mkataba Lemera, Kagame alimchomekea "watu wake" kwenye kikosi chake cha ulinzi. Mmojawapo ni Luteni Rashid Kasereka, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu Kusini. Januari 16, 2001, Luteni Kasereka alimfyatulia Rais Kabila risasi 4 za tumbo na kumuua papohapo. Jumuiya ya kimataifa ikamtuhumu Kagame kuhusika, lakini akakanusha na kusema ni madai yasiyo na msingi. Baada ya kifo cha Mzee Kabila, mwanae Joseph akaapishwa kuwa Rais akiwa na miaka 29 tu. Joseph akafanya jitihada mbalimbali za kukomesha vita kwa kushirikisha Jumuiya ya kimataifa. Julai 30, 2002, ukasainiwa Mkataba wa Pretoria (The Pretoria Agreement) uliotaka pande zote kusitisha mapigano. Desemba 17, 2002, ukasainiwa Mkataba mwingine ulioitwa Global &Inclusive Agreement (maarufu kama 2003 Peace Deal). Na hatimaye, Aprili 2, 2003, ukasainiwa Mkataba Maarufu wa Sun City Peace Agreement uliomaliza kabisa vita ya Congo. Pamoja na mambo mengine, mkataba huo ulitaka kuondolewa kwa majeshi yote ya kigeni nchini Congo, kuwepo na utaratibu wa uchaguzi wa kidemokrasia, na kuwaingiza jeshini askari wa vikundi vya waasi. Mkataba huo ulihitimisha Vita vya Pili vya Congo. Vita mbaya mno katika historia. Vita hivi vilibatizwa jina "The Great war of Africa" kwa jinsi vilivyoshirikisha mataifa mengi, na jinsi vilivyoleta madhara makubwa kwa watu ikiwemo vifo vya zaidi ya watu 500,000. Baada ya kumalizika kwa vita hivyo, Congo ikarudi kwenye amani, japokuwa kulikuwa na vikundi vidogo vya wanamgambo katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, hasa eneo la Kivu lakini makundi makubwa yote ya Waasi yalikubali kuweka silaha chini. Kuanzia mwaka 2003 hadi 2006 hali ikatulia kabisa. Kwa mara ya kwanza raia wa Congo wakalala pasi na kusikia milio ya risasi.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·1K Views
  • Like
    Love
    Yay
    Angry
    5
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·352 Views
  • Usichanganye hivi vitu viwili, ni tofauti sana. Mapenzi na upendo, hivi ni vitu tofauti. Mapenzi Yana utumwa lakini upendo una uhuru, mapenzi yana visasi lakini upendo una msamaha, mapenzi yanamiliki lakini upendo una utu, mapenzi yana mwisho lakini upendo ni wa milele.

    Mahusiano ya mwanaume na mwanamke ni mapenzi siyo upendo. Huu ni muungano wa kimaslahi, utake usitake ni maslahi. Kila upande una maslahi yake na siyo upendo. Angalia wanavyohesabiana waliyofanyiana aidha mema au mabaya siku wanapoachana. Upendo huwa hauhesabu na hauna kumbukumbu kabisa.

    Mtu akikuambia nilikupenda sana, wala usijione na hatia, huyo muongo mkubwa. Neno analotakiwa kusema ni "nilikuwa na hisia kali za mapenzi kwako". Huwezi kumpiga mtu unayempenda, wala huwezi kutamani apatwe na mabaya sababu amekuacha. Mtu unayempenda utamtakia mema hata kama kukuacha kwake kulikuumiza. Siku zote utamuunga mkono kwa lolote linalompa furaha na amani hata kama ni kukuacha.

    Usichanganye upendo na mapenzi ni vitu tofauti. Upendo ni nishati ya asili inayoishi ndani ya mtu lakini mapenzi ni hisia inayotokana na mvuto wa kimahaba.
    Usichanganye hivi vitu viwili, ni tofauti sana. Mapenzi na upendo, hivi ni vitu tofauti. Mapenzi Yana utumwa lakini upendo una uhuru, mapenzi yana visasi lakini upendo una msamaha, mapenzi yanamiliki lakini upendo una utu, mapenzi yana mwisho lakini upendo ni wa milele. Mahusiano ya mwanaume na mwanamke ni mapenzi siyo upendo. Huu ni muungano wa kimaslahi, utake usitake ni maslahi. Kila upande una maslahi yake na siyo upendo. Angalia wanavyohesabiana waliyofanyiana aidha mema au mabaya siku wanapoachana. Upendo huwa hauhesabu na hauna kumbukumbu kabisa. Mtu akikuambia nilikupenda sana, wala usijione na hatia, huyo muongo mkubwa. Neno analotakiwa kusema ni "nilikuwa na hisia kali za mapenzi kwako". Huwezi kumpiga mtu unayempenda, wala huwezi kutamani apatwe na mabaya sababu amekuacha. Mtu unayempenda utamtakia mema hata kama kukuacha kwake kulikuumiza. Siku zote utamuunga mkono kwa lolote linalompa furaha na amani hata kama ni kukuacha. Usichanganye upendo na mapenzi ni vitu tofauti. Upendo ni nishati ya asili inayoishi ndani ya mtu lakini mapenzi ni hisia inayotokana na mvuto wa kimahaba.
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·831 Views
  • #PART9

    Baada ya miaka mitatu ya utulivu, ghafla 2006 Jenerali Laurent Nkunda, aliasi jeshi kwa madai serikali imeshindwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa SunCity. Ikumbukwe kabla ya kujiunga na Jeshi, alikua mpiganaji wa RCD - Goma, kundi lililoungwa mkono na Rwanda. Baada ya mkataba wa Suncity waasi wote waliingizwa jeshini akiwemo Nkunda.

    Lakini Juni 29, 2006, Nkunda akaasi jeshi na kuunda kundi la Congrès National pour la Défense du Peuple (CNDP). Madai yake:
    - Askari wa vikundi vya waasi walioingizwa jeshini hawakupewa vyeo.
    - Serikali ya Congo kushindwa kuwatanbua Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo kama raia wa Congo.
    - Serikali ya Congo kushindwa kuwakamata wanamgambo wa kihutu wa FDLR (Intarahanwe) waliojificha Congo baada ya kufanya mauaji ya kimbari Rwanda 1994.

    Nkunda akasema lengo la kuanzisha kundi la waasi la CNDP ni kupigania haki za Watutsi waishio mashariki mwa Congo (Banyamulenge) na kukabiliana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR. Nkunda akaungwa mkono na Rwanda na Uganda, akapewa silaha, vita ikaanza upyaaaaa (tamka kwa sauti ya mbunge Bwege).

    CNDP ikaua raia wengi wenye asili ya Kihutu ikiwatumu kuwa wafuasi wa FDLR. Serikali ya Burundi ikiongozwa na Piere Nkurunzinza (Mhutu) ikaingiza jeshi Congo kupambana na CNDP ili kulinda raia wake waliokua Congo. Kwa miaka mitatu kukawa na mapigano makali sana mashariki mwa Congo.

    January 2009 Waasi wa CNDP wakazidiwa. Laurent Nkunda akakimbilia Rwanda. Alipofika akakamatwa na kuwekwa kizuizini. Mpaka leo, bado anashikiliwa bila kufikishwa mahakamani. Jenerali Bosco Ntaganda, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu akateuliwa kuongoza CNDP. Akafanya vitendo vingi vya kikatili kwa raia kuliko mtangulizi wake, kama ubakaji, mauaji ya halaiki, na kutumikisha watoto jeshini.

    Machi 23, 2009 serikali ya Congo na CNDP wakasaini Mkataba wa Amani, ulioitwa "March 23 Agreement" wenye masharti yafuatayo:
    - Kusitisha mapigano kwa pande zote.
    - Kuingiza askari wa CNDP kwenye jeshi la Congo.
    - Kutowashtaki askari wa CNDP kwa makosa waliyofanya wakati wa vita.
    - Wananchi wa Kivu wanufaike na rasilimali zao
    - Kulinda haki za binadamu Kivu
    (Malisa GJ)

    #PART9 Baada ya miaka mitatu ya utulivu, ghafla 2006 Jenerali Laurent Nkunda, aliasi jeshi kwa madai serikali imeshindwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa SunCity. Ikumbukwe kabla ya kujiunga na Jeshi, alikua mpiganaji wa RCD - Goma, kundi lililoungwa mkono na Rwanda. Baada ya mkataba wa Suncity waasi wote waliingizwa jeshini akiwemo Nkunda. Lakini Juni 29, 2006, Nkunda akaasi jeshi na kuunda kundi la Congrès National pour la Défense du Peuple (CNDP). Madai yake: - Askari wa vikundi vya waasi walioingizwa jeshini hawakupewa vyeo. - Serikali ya Congo kushindwa kuwatanbua Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo kama raia wa Congo. - Serikali ya Congo kushindwa kuwakamata wanamgambo wa kihutu wa FDLR (Intarahanwe) waliojificha Congo baada ya kufanya mauaji ya kimbari Rwanda 1994. Nkunda akasema lengo la kuanzisha kundi la waasi la CNDP ni kupigania haki za Watutsi waishio mashariki mwa Congo (Banyamulenge) na kukabiliana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR. Nkunda akaungwa mkono na Rwanda na Uganda, akapewa silaha, vita ikaanza upyaaaaa (tamka kwa sauti ya mbunge Bwege). CNDP ikaua raia wengi wenye asili ya Kihutu ikiwatumu kuwa wafuasi wa FDLR. Serikali ya Burundi ikiongozwa na Piere Nkurunzinza (Mhutu) ikaingiza jeshi Congo kupambana na CNDP ili kulinda raia wake waliokua Congo. Kwa miaka mitatu kukawa na mapigano makali sana mashariki mwa Congo. January 2009 Waasi wa CNDP wakazidiwa. Laurent Nkunda akakimbilia Rwanda. Alipofika akakamatwa na kuwekwa kizuizini. Mpaka leo, bado anashikiliwa bila kufikishwa mahakamani. Jenerali Bosco Ntaganda, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu akateuliwa kuongoza CNDP. Akafanya vitendo vingi vya kikatili kwa raia kuliko mtangulizi wake, kama ubakaji, mauaji ya halaiki, na kutumikisha watoto jeshini. Machi 23, 2009 serikali ya Congo na CNDP wakasaini Mkataba wa Amani, ulioitwa "March 23 Agreement" wenye masharti yafuatayo: - Kusitisha mapigano kwa pande zote. - Kuingiza askari wa CNDP kwenye jeshi la Congo. - Kutowashtaki askari wa CNDP kwa makosa waliyofanya wakati wa vita. - Wananchi wa Kivu wanufaike na rasilimali zao - Kulinda haki za binadamu Kivu (Malisa GJ)
    0 Commentarios ·0 Acciones ·1K Views