• Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeziandikia klabu za mpira wa miguu barani Ulaya zinazoingia mikataba ya ufadhili kutoka Serikali ya Rwanda kutopokea, "Fedha zinazotokana na umwagikaji wa damu", unaoendelea mashariki mwa DR Congo.

    Kwa mujibu Waziri wa mambo ya kigeni Nchini DR Congo, Therese Kayikwamba Wagner ameziandikia klabu za Arsenal FC ya England , Paris Sint-Germaine ya Ufaransa na FC Bayern München ya Ujerumani kusitisha ushirikiano wao wa ufadhili wa mauzo chini ya mpango wa "Visit Rwanda" wakidai kwamba idadi kubwa ya Wanajeshi wa Rwanda wanapigana na Jeshi la FARDC huko Mjini Goma wakisaidiana na kundi la Waasi la M23.

    Kwenye barua hiyo kwa klabu ya Arsenal FC, Waziri Wagner amesema kwamba, Rwanda inastahili kulaumiwa kwa hatua zake ndani ya DR Congo kwani Umoja wa mataifa umeripoti kwamba kikosi cha Wanajeshi 4,000 kutoka Rwanda kiko ndani ya DR Congo na kinashikriki kwenye vita vinavyoendelea Nchini humo.

    Sanjari na klabu hizo kusubiriwa kufanya uamuzi kuhusu ombi hilo la DR Congo na shutuma dhidi ya Rwanda, DR Congo imeendelea kuwasilisha hoja yao ya hali mbaya inayoshuhudiwa mashariki mwa nchi hiyo.

    Waziri Wagner ameiambia klabu ya Arsenal kwamba, "maelfu ya Watu wamekwama Jijini Goma, ambapo hakuna njia ya kuingiza chakula, huku huduma za kusambaza maji na umeme zikiwa zimekatizwa. Hakuna usalama, Watu wameuawa na wizi unakithiri Mjini humo. Mfadhili wenu anahusika moja kwa moja kwa mahangaiko haya ya wengi"

    Barua hiyo inaangazia mpango wa, "Visit Rwanda" unafadhiliwa moja kwa moja na uchimbaji madini haramu unaoendelea katika maeneo kadhaa yaliyokaliwa mashariki mwa DR Congo na kuvukishwa mpaka hadi Rwanda ambayo inasafirisha ughaibuni kama madini yake asilii.

    Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo 🇨🇩 imeziandikia klabu za mpira wa miguu barani Ulaya zinazoingia mikataba ya ufadhili kutoka Serikali ya Rwanda 🇷🇼 kutopokea, "Fedha zinazotokana na umwagikaji wa damu", unaoendelea mashariki mwa DR Congo. Kwa mujibu Waziri wa mambo ya kigeni Nchini DR Congo, Therese Kayikwamba Wagner ameziandikia klabu za Arsenal FC ya England 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿, Paris Sint-Germaine ya Ufaransa 🇫🇷 na FC Bayern München ya Ujerumani 🇩🇪 kusitisha ushirikiano wao wa ufadhili wa mauzo chini ya mpango wa "Visit Rwanda" wakidai kwamba idadi kubwa ya Wanajeshi wa Rwanda wanapigana na Jeshi la FARDC huko Mjini Goma wakisaidiana na kundi la Waasi la M23. Kwenye barua hiyo kwa klabu ya Arsenal FC, Waziri Wagner amesema kwamba, Rwanda inastahili kulaumiwa kwa hatua zake ndani ya DR Congo kwani Umoja wa mataifa umeripoti kwamba kikosi cha Wanajeshi 4,000 kutoka Rwanda kiko ndani ya DR Congo na kinashikriki kwenye vita vinavyoendelea Nchini humo. Sanjari na klabu hizo kusubiriwa kufanya uamuzi kuhusu ombi hilo la DR Congo na shutuma dhidi ya Rwanda, DR Congo imeendelea kuwasilisha hoja yao ya hali mbaya inayoshuhudiwa mashariki mwa nchi hiyo. Waziri Wagner ameiambia klabu ya Arsenal kwamba, "maelfu ya Watu wamekwama Jijini Goma, ambapo hakuna njia ya kuingiza chakula, huku huduma za kusambaza maji na umeme zikiwa zimekatizwa. Hakuna usalama, Watu wameuawa na wizi unakithiri Mjini humo. Mfadhili wenu anahusika moja kwa moja kwa mahangaiko haya ya wengi" Barua hiyo inaangazia mpango wa, "Visit Rwanda" unafadhiliwa moja kwa moja na uchimbaji madini haramu unaoendelea katika maeneo kadhaa yaliyokaliwa mashariki mwa DR Congo na kuvukishwa mpaka hadi Rwanda ambayo inasafirisha ughaibuni kama madini yake asilii.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·14 Просмотры
  • Nchi ya Rwanda imekanusha taarifa ya madai iliyotolewa na Mkutano wa wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhusu uhusika wake na machafuko yanayoendelea Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo . Licha ya kukanusha madai hayo, imeinyooshea kidole DR Congo ikiishutumu kutaka kuipindua Serikali ya Rwanda iliyopo madarakani.

    Hayo yameelezwa leo Jumapili Februari 2, 2025 na taarifa iliyotolewa na kuchapishwa kwenye mtandao wa X wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda.

    “Rwanda inakana shutuma dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) iliyotolewa katika taarifa ya Mkutano wa Kilele wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Januari 31, 2025. RDF inatetea mipaka ya Rwanda dhidi ya vitisho na inalinda Raia, haishambulii Raia.

    “SADC imetuma kikosi cha mashambulizi, SAMIDRC, kusaidia vita vya Serikali ya DRC dhidi ya Watu wake wenyewe - M23 na Wanachama wa Jumuiya yao - wengi wao wamekimbilia kama Wakimbizi Nchini Rwanda na katika kanda nzima. Serikali ya DRC pia ina nia ya kushambulia Rwanda na kupindua Serikali yake, kama ilivyosemwa mara kwa mara na hadharani na Rais Tshisekedi,” imesema taarifa hiyo.

    Nchi ya Rwanda 🇷🇼 imekanusha taarifa ya madai iliyotolewa na Mkutano wa wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhusu uhusika wake na machafuko yanayoendelea Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩. Licha ya kukanusha madai hayo, imeinyooshea kidole DR Congo ikiishutumu kutaka kuipindua Serikali ya Rwanda iliyopo madarakani. Hayo yameelezwa leo Jumapili Februari 2, 2025 na taarifa iliyotolewa na kuchapishwa kwenye mtandao wa X wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda. “Rwanda inakana shutuma dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) iliyotolewa katika taarifa ya Mkutano wa Kilele wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Januari 31, 2025. RDF inatetea mipaka ya Rwanda dhidi ya vitisho na inalinda Raia, haishambulii Raia. “SADC imetuma kikosi cha mashambulizi, SAMIDRC, kusaidia vita vya Serikali ya DRC dhidi ya Watu wake wenyewe - M23 na Wanachama wa Jumuiya yao - wengi wao wamekimbilia kama Wakimbizi Nchini Rwanda na katika kanda nzima. Serikali ya DRC pia ina nia ya kushambulia Rwanda na kupindua Serikali yake, kama ilivyosemwa mara kwa mara na hadharani na Rais Tshisekedi,” imesema taarifa hiyo.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·15 Просмотры
  • Ukisikia madai ya Rwanda kuvuruga amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ukarudi kuangalia ramani na takwimu za mataifa hayo hakika utaamini ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi. Kitakwimu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeizidi Rwanda kila kitu ikiwemo ukubwa wa eneo, rasilimali, madini pamoja na idadi ya Watu.

    Eneo la Congo ni karibu mara mia (100) ya eneo la Rwanda. Idadi ya Watu wa Kongo ni takribani mara 10 Watu wa Rwanda. Pamoja na hayo yote Congo wanalalamika kwamba Rwanda ndio inayounga mkono makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamelemea majeshi ya serikali na kusonga mbele kiasi cha kutwaa miji mikubwa ya kimkakati yenye utajiri mkubwa wa madini.

    Rwanda pamoja na kuzidiwa takwimu hizo ila mipango thabiti na uwekezaji wa kimkakati katika masuala ya kijeshi, ulinzi na usalama katika eneo hilo ndio umeifanya ionekane kama ndio taifa kubwa. Yaani kiufupi ukiwa hujui ramani na takwimu unaweza kudhani Rwanda ndio taifa kubwa ndio maana inalalamikiwa kuionea Kongo. Kiufupi Rwanda inanufaika mno na mipango thabiti ya kiuongozi, wakati Kongo ikiwa na uongozi usio na mipango thabiti ya kikanda na kimkakati kulinda mipaka yake na majimbo ya Mashariki yenye utajiri mkubwa wa madini

    Rwanda ina idadi kubwa ya Watutsi ambao pia wanapatikana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wachache Burundi na Uganda. Historia ya watutsi inasemekana walitokea Ethiopia kuja maziwa makuu na sifa yao kuu wanapenda uongozi (kwa mnaowajua mtakua mashahidi). Jamii ya watutsi ni watu ambao huwa hawapendi unyonge wala kuonewa, ni wepesi kujitetea na huwa wanaumoja sana.

    Baada ya Wakoloni kugawa mipaka ndio walisababisha watutsi kujikuta ndani ya nchi nyingi tofauti ila ni wazawa wa maeneo hayo na historia yao katika nchi hizo ni toka zama za kale hivyo ni ngumu kuwaita Wahamiaji. Watutsi ndio waliomsaidia Hayati Laurent Kabila kumpindua Mobutu Seseseko na inasemekana Mama mzazi wa Joseph Kabila alikua Mtutsi pia. Kimsingi Kongo haikupaswa kuilalamikia Rwanda, bali Rwanda ndio ingepaswa kuilalamikia Kongo.

    Ukisikia madai ya Rwanda 🇷🇼 kuvuruga amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 ukarudi kuangalia ramani na takwimu za mataifa hayo hakika utaamini ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi. Kitakwimu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeizidi Rwanda kila kitu ikiwemo ukubwa wa eneo, rasilimali, madini pamoja na idadi ya Watu. Eneo la Congo ni karibu mara mia (100) ya eneo la Rwanda. Idadi ya Watu wa Kongo ni takribani mara 10 Watu wa Rwanda. Pamoja na hayo yote Congo wanalalamika kwamba Rwanda ndio inayounga mkono makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamelemea majeshi ya serikali na kusonga mbele kiasi cha kutwaa miji mikubwa ya kimkakati yenye utajiri mkubwa wa madini. Rwanda pamoja na kuzidiwa takwimu hizo ila mipango thabiti na uwekezaji wa kimkakati katika masuala ya kijeshi, ulinzi na usalama katika eneo hilo ndio umeifanya ionekane kama ndio taifa kubwa. Yaani kiufupi ukiwa hujui ramani na takwimu unaweza kudhani Rwanda ndio taifa kubwa ndio maana inalalamikiwa kuionea Kongo. Kiufupi Rwanda inanufaika mno na mipango thabiti ya kiuongozi, wakati Kongo ikiwa na uongozi usio na mipango thabiti ya kikanda na kimkakati kulinda mipaka yake na majimbo ya Mashariki yenye utajiri mkubwa wa madini Rwanda ina idadi kubwa ya Watutsi ambao pia wanapatikana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wachache Burundi na Uganda. Historia ya watutsi inasemekana walitokea Ethiopia kuja maziwa makuu na sifa yao kuu wanapenda uongozi (kwa mnaowajua mtakua mashahidi). Jamii ya watutsi ni watu ambao huwa hawapendi unyonge wala kuonewa, ni wepesi kujitetea na huwa wanaumoja sana. Baada ya Wakoloni kugawa mipaka ndio walisababisha watutsi kujikuta ndani ya nchi nyingi tofauti ila ni wazawa wa maeneo hayo na historia yao katika nchi hizo ni toka zama za kale hivyo ni ngumu kuwaita Wahamiaji. Watutsi ndio waliomsaidia Hayati Laurent Kabila kumpindua Mobutu Seseseko na inasemekana Mama mzazi wa Joseph Kabila alikua Mtutsi pia. Kimsingi Kongo haikupaswa kuilalamikia Rwanda, bali Rwanda ndio ingepaswa kuilalamikia Kongo.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·16 Просмотры
  • Raisi wa Rwanda , Paul Kagame ameipongeza klabu ya Arsenal FC baada ya ushindi wake dhidi ya klabu ya Manchester City wa mabao matano kwa moja (5-1).

    NB : Hawa ni baadhi ya Viongozi na Watu maarufu wanaopenda klabu ya Arsenal FC.

    - Paul Kagame
    - Aliko Dangote
    - Malkia Elisabeth (Marehemu)
    - Osama Bin Laden (Marehemu)
    Etc...

    Raisi wa Rwanda 🇷🇼, Paul Kagame ameipongeza klabu ya Arsenal FC baada ya ushindi wake dhidi ya klabu ya Manchester City wa mabao matano kwa moja (5-1). NB : Hawa ni baadhi ya Viongozi na Watu maarufu wanaopenda klabu ya Arsenal FC. - Paul Kagame - Aliko Dangote - Malkia Elisabeth (Marehemu) - Osama Bin Laden (Marehemu) Etc...
    Love
    1
    · 0 Комментарии ·0 Поделились ·15 Просмотры