MTUNZI WA JINA LA 'TANZANIA' AFARIKI
Hicho ni kipande cha gazeti la The Nationalist la Oktoba 30, 1964. Habari kubwa kwenye gazeti hili na Nchi kwa ujumla ni jina jipya la TANZANIA. Ni kwamba baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa April 26, 1964, jina la nchi mpya lilikuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Lakini jina hili lilikuwa refu sana na kuwa kero kwa Watumiaji.
Serikali kupitia wizara ya habari na utalii chini ya waziri Dkt. Idrisa Abdul Wakili, ikaanzisha mchakato wa kutafuta jina jipya litakalokuwa fupi na rahisi. Ikatoa tangazo kupitia gazeti la Tanganyika Standard, ambalo sasa ni Daily News, kuwataka Watanzania wenye kuweza kubuni jina jipya la Nchi kufanya hivyo. Ndipo kijana wa miaka 18 kutoka Morogoro, Mohamed Iqbal Dar, Mwanafunzi wa Sekondari ya Aga Khan Morogoro, akaliona tangazo hilo na kushiriki.
Akatunga jina la Tanzania na kulituma kwenye anwani iliyotangazwa. Baada ya muda kupita, akapata barua kutoka serikalini ikimtaja na kumpongeza yeye kama mmoja wa Washindi 16 na wakatakiwa kufika ofisi za wizara. Kwa pamoja watu hawa walitakiwa kugawana zawadi ya shilingi 200, wakati huo shilingi moja ilikuwa sawa na dola 8 za Marekani.
Siku ilipofika, watu wawili tu walijitokeza; yeye Mohamed Iqbal Dar na Yusufal Pir Mohamed. Lakini huyo mwenzake hakuwa na ile barua ya kutajwa kama mshindi na kupongezwa... Serikali ikashindwa kumthibitisha hivyo kumtangaza Mohamed Iqbal Dar kama Mshindi pekee. Ndipo Jumatano ya Oktoba 29, 1964 serikali ikatangaza rasmi kwamba jina jipya la nchi ni Tanzania na gazeti la The Nationalist likaichapisha habari hii kubwa, Alhamisi ya Oktoba 30, 1964. Jina la Tanzania likaanza kutumika rasmi Novemba Mosi, 1964.
- Alitungaje jina?
TAN - kutoka Tanganyika
ZAN - kutoka Zanzibar
I - kutoka jina lake la Iqbal.
A - kutoka dini yake ya Ahmadiya. Hii pia ikawa rahisi zaidi kwake kwani majina ya nchi nyingi za Afrika yaliishia na A kama Ethiopia, Zambia, Gambia nk.
- Ni nani huyu Mohamed Iqbal Dar?
Ni mtoto wa Dkt. Dar, ambaye alikuja Tanzania mwaka 1930 kutoka India. Alifikia Tanga, na ndiko alikozaliwa Mohamed, hakafu akahamia Morogoro. Mohamed amefarikia huko Birmingham Nchini Uingereza .

Ni mtoto wa Dkt. Dar, ambaye alikuja Tanzania mwaka 1930 kutoka India. Alifikia Tanga, na ndiko alikozaliwa Mohamed, hakafu akahamia Morogoro. Mohamed amefarikia huko Birmingham Nchini Uingereza 🇬🇧.