"Kwamba TFF impige mvua ya miaka miwili Kijana wake Ally Kamwe? Nimeona taarifa kwa Ndugu yangu Mkomwa, nimewaza sana kwamba TFF kama Taasisi yetu tunayoiamini ifikie maamuzi kama haya? Labda wacha tusubiri taarifa rasmi, lakini kama ni kweli basi inafikirisha sana.
Kamwe ametiwa hatiani kwa kosa liloitwa la UDHALILISHAJI, kwamba udhalilishaji aliofanya ni kupost “Leo Mjadala redioni 90% ni kuhusu Makolo na Waamuzi” hapo ndipo wakamtia hatiani kwa kudharirisha, lakini nimewaza sana, Ally ni wa kwanza kulaumu? Hao Makolo ni nani? Wanashiriki ligi gani? Ni timu gani? Bado inafikirisha sana, kwamba kuna timu inachezeshwa na Marefa wetu inaitwa Makolo?
Tufanye ni kosa lakini ije na adhabu ya miaka miwili? Nakumbuka kuna Msemaji alifanya kosa kama hili alifungiwa miezi mitatu, je utofauti wake na Ally ni upi? Miaka miwili imetokana na nini? Je ni TFF tu au kuna Mtu ndani pale au nje yupo nyuma ya mchezo akisukuma kete zake kwa umakini? Ni kosa kubwa kiasi hicho mpaka tumpoteze Kijana wetu kwa miaka miwili?
Kwamba tunashindwa kuvumiliana? Kuadhibiana kwa kuhurumiana? Kama ambavyo Wadau wa soka wamekuwa wakiwavumilia Waamuzi? Sikatai amekosea lakini nakataa ukubwa wa adhabu, sitaki kuamini mpaka nione taarifa rasmi ila kama kweli ni miaka miwili basi huenda ikawa adhabu kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa kosa dogo zaidi, inafikirisha, siamini kama taasisi yetu penda ikatoa adhabu kama hii, unless kuwa na Mtu anashawishi.
Makofi hayamkuzi Mtoto bali yanamuumiza, sheria haipo kusaka haki bali Mshindi, hiyo ni kweli na inafahamika ila Mshindi anapaswa kuwa mpira wa miguu sio Mtu mmoja, kama kweli ni miaka miwili ipo haja ya kupunguza adhabu, kwa maslahi mapana ya mpira kwakuwa Ally ni Kijana wetu, Mtoto wetu ambaye ameutumikia mpira huu kwa mapenzi makubwa sana, itabaki kuwa ni mmoja kati yetu.
Nachofahamu Chura hawezi kuruka mchana wa jua kali tena nchi kavu kama hakuna kitu kinachomkimbiza" - Farhan JR, Mchambuzi.

0 Comments
路0 Shares
路15 Views