
-
Nchi za Niger , Burkina Faso na Mali zimetangaza rasmi kujiondoa katika Shirika la Kimataifa la Mataifa yanayozungumza Kifaransa la ‘Francophonie’ (OIF). Uamuzi huo umefanywa na Viongozi wa mataifa hayo yenye Serikali za kijeshi, Niger inaongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani, Mali inaongozwa na Kanali Assimi Goïta na Burkina Faso inayoongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré.
Viongozi hao wamedai OIF na taasisi zingine zilizo chini ya Ufaransa ni ukoloni mamboleo. OIF ni Shirila lililoundwa kwa madhumuni ya kukuza lugha ya Kifaransa na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zinazozungumza Kifaransa.
Gazeti la Le Monde la Nchini Ufaransa limeripoti kuwa taarifa ya pamoja ya Nchi hizo tatu ilisema kwamba OIF imegeuka kuwa ‘chombo cha kisiasa’ kinachoendeshwa na Ufaransa ili kuongeza unyonyaji wa rasilimali za mataifa hayo.
Nchi za Niger 🇳🇪, Burkina Faso 🇧🇫 na Mali 🇲🇱 zimetangaza rasmi kujiondoa katika Shirika la Kimataifa la Mataifa yanayozungumza Kifaransa la ‘Francophonie’ (OIF). Uamuzi huo umefanywa na Viongozi wa mataifa hayo yenye Serikali za kijeshi, Niger inaongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani, Mali inaongozwa na Kanali Assimi Goïta na Burkina Faso inayoongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré. Viongozi hao wamedai OIF na taasisi zingine zilizo chini ya Ufaransa 🇫🇷 ni ukoloni mamboleo. OIF ni Shirila lililoundwa kwa madhumuni ya kukuza lugha ya Kifaransa na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zinazozungumza Kifaransa. Gazeti la Le Monde la Nchini Ufaransa limeripoti kuwa taarifa ya pamoja ya Nchi hizo tatu ilisema kwamba OIF imegeuka kuwa ‘chombo cha kisiasa’ kinachoendeshwa na Ufaransa ili kuongeza unyonyaji wa rasilimali za mataifa hayo.0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·121 Visualizações -
Rais wa Nchi ya Ukraine , Volodymyr Zelensky, ametabiri kuea Rais wa Urusi , Vladimir Putin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kuwa afya ya Kiongozi huyo wa Urusi inazorota. Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Waandishi wa habari Jijini Paris, Ufaransa baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusema kuwa "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika."
Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kuwa huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume.
Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na Daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Sanjari na hayo, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.
Rais wa Nchi ya Ukraine 🇺🇦, Volodymyr Zelensky, ametabiri kuea Rais wa Urusi 🇷🇺, Vladimir Putin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kuwa afya ya Kiongozi huyo wa Urusi inazorota. Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Waandishi wa habari Jijini Paris, Ufaransa 🇫🇷 baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusema kuwa "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika." Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kuwa huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume. Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na Daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani 🇺🇸 ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Sanjari na hayo, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·125 Visualizações -
Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limetangaza zawadi zitakazotolewa kwa Washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu (FIFA CLUB WORLD CUP), ambapo bingwa wa michuano hiyo atapata dola milioni 125 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 300 za kitanzania huku kukitarajiwa kutolewa jumla ya dola bilioni 1 kwa klabu 32 zitakavyoshiriki na dola milioni 250 zitatolewa kwa mashirikisho kwa ajili kukuza mpira wa miguu kwa ngazi ya klabu Duniani.
Shirikisho hilo limepanga kutoa dola milioni 250 ili kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu kwa kiwango cha kimataifa ambapo fedha hizi zitatumika kusaidia klabu ndogo, kuboresha miundombinu, kuwekeza katika mafunzo ya Wachezaji na Makocha pamoja na kuimarisha ushirikiano wa klabu kimataifa.
Aidha, pango huu unalenga kuhakikisha kuwa maendeleo ya mpira wa miguu hayaishii kwa klabu kubwa pekee, bali pia yanawanufaisha hadi klabu dogo na kuinua mpira wa Duniani kote. FIFA pia imesisitiza kuwa, mapato yote ya mashindano haya yatasambazwa kwa klabu bila kugusa akiba yake, ambayo inatumiwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu kupitia Vyama (211) Wanachama wa FIFA.
Mfumo huu ni mkubwa zaidi katika historia ya mpira wa miguu, ukiwa na mechi saba (7) kwenye hatua ya makundi na mfumo wa mchujo.
Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limetangaza zawadi zitakazotolewa kwa Washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu (FIFA CLUB WORLD CUP), ambapo bingwa wa michuano hiyo atapata dola milioni 125 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 300 za kitanzania huku kukitarajiwa kutolewa jumla ya dola bilioni 1 kwa klabu 32 zitakavyoshiriki na dola milioni 250 zitatolewa kwa mashirikisho kwa ajili kukuza mpira wa miguu kwa ngazi ya klabu Duniani. Shirikisho hilo limepanga kutoa dola milioni 250 ili kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu kwa kiwango cha kimataifa ambapo fedha hizi zitatumika kusaidia klabu ndogo, kuboresha miundombinu, kuwekeza katika mafunzo ya Wachezaji na Makocha pamoja na kuimarisha ushirikiano wa klabu kimataifa. Aidha, pango huu unalenga kuhakikisha kuwa maendeleo ya mpira wa miguu hayaishii kwa klabu kubwa pekee, bali pia yanawanufaisha hadi klabu dogo na kuinua mpira wa Duniani kote. FIFA pia imesisitiza kuwa, mapato yote ya mashindano haya yatasambazwa kwa klabu bila kugusa akiba yake, ambayo inatumiwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu kupitia Vyama (211) Wanachama wa FIFA. Mfumo huu ni mkubwa zaidi katika historia ya mpira wa miguu, ukiwa na mechi saba (7) kwenye hatua ya makundi na mfumo wa mchujo.0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·178 Visualizações -
The ground we walk on today, will be our roof tomorrowThe ground we walk on today, will be our roof tomorrow ‼️
-
-
-
-
-
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama na kibinadamu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku hali ikizidi kuzorota. Mwakilishi Maalum wa Umoja huo (UN) Nchini DR Congo, Bintou Keita, amesema Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na kutishia kupanua mashambulizi yao hadi Mkoani Tshopo na Maniema.
"Hivi karibuni M23 imesimika utawala wake kwa kuteua gavana, makamu gavana na meya huko Bukavu, Kivu Kusini," amesema Keita.
Ameeleza kuwa mgogoro huo unahusiana na unyonyaji wa madini mashariki mwa DR Congo na kuzua wasiwasi wa kikanda. Pia amegusia hali mbaya ya kibinadamu, akisema kumekuwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ajira ya kulazimishwa kwa Vijana, wakiwemo Watoto.
Licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marais wa Rwanda na DR Congo Nchini Qatar , amani bado haijapatikana. Keita ametoa wito wa kuteuliwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika ili kuongoza juhudi za kusitisha mapigano.
Balozi wa DR Congo katika Baraza la Umoja wa kimataifa (UN), Zénon Mukongo Ngay, ameishutumu Rwanda kwa kutotekeleza usitishaji mapigano, huku Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, akisema Nchi yake itaendelea kuchukua "hatua za ulinzi" mpaka kuwe na mfumo wa kudumu wa usalama.
Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa DR Congo inakabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa kuwahi kutokea, ambapo Watu zaidi ya milioni 27.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na vita na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Nchi hiyo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama na kibinadamu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 huku hali ikizidi kuzorota. Mwakilishi Maalum wa Umoja huo (UN) Nchini DR Congo, Bintou Keita, amesema Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda 🇷🇼 sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na kutishia kupanua mashambulizi yao hadi Mkoani Tshopo na Maniema. "Hivi karibuni M23 imesimika utawala wake kwa kuteua gavana, makamu gavana na meya huko Bukavu, Kivu Kusini," amesema Keita. Ameeleza kuwa mgogoro huo unahusiana na unyonyaji wa madini mashariki mwa DR Congo na kuzua wasiwasi wa kikanda. Pia amegusia hali mbaya ya kibinadamu, akisema kumekuwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ajira ya kulazimishwa kwa Vijana, wakiwemo Watoto. Licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marais wa Rwanda na DR Congo Nchini Qatar 🇶🇦, amani bado haijapatikana. Keita ametoa wito wa kuteuliwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika ili kuongoza juhudi za kusitisha mapigano. Balozi wa DR Congo katika Baraza la Umoja wa kimataifa (UN), Zénon Mukongo Ngay, ameishutumu Rwanda kwa kutotekeleza usitishaji mapigano, huku Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, akisema Nchi yake itaendelea kuchukua "hatua za ulinzi" mpaka kuwe na mfumo wa kudumu wa usalama. Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa DR Congo inakabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa kuwahi kutokea, ambapo Watu zaidi ya milioni 27.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na vita na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Nchi hiyo.0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·125 Visualizações