• Rais wa Nchi ya Burundi , Evariste Ndayishimiye anasema kuwa Nchi ya Rwanda ina mpango wa kuivamia Burundi kupitia Congo ambapo anasema Nchi hiyo itakuwa imekosea sana.

    “Tunajua kwamba Rwanda inajaribu kutushambulia kupitia eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia vuguvugu la Red-Tabara. Lakini tunawaambia kwamba ikiwa wanataka kushambulia Bujumbura kupitia Congo na sisi Kigali hatuko mbali kupitia Kirundo,” alisema Rais Evariste Ndayishimiye

    Baada ya kauli hiyo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema kuwa, ameshangazwa na kauli ya Rais Evariste Ndayishimiye huku akihoji Rais Ndayishimiye anaeleza kuwa ana taarifa za kuaminika kuwa Rwanda ina mpango wa kushambulia Burundi ?. Msemaji huyo alisema pia endapo hali hiyo ikitokea basi migogoro inaweza kuwa na maafa kwani inaweza kusambaa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kati.

    Rais Ndayishimiye amemalizia kwa kusema kuwa tayari ameshatuma Wajumbe kadhaa kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame wa kumtaka atekeleze makubaliano ambayo yatazileta pamoja Nchi hizo mbili pamoja lakini hadi leo hii hakuna majibu yoyote yaliyotolewa na bado anayasubiri pia.

    Rais wa Nchi ya Burundi 馃嚙馃嚠, Evariste Ndayishimiye anasema kuwa Nchi ya Rwanda 馃嚪馃嚰 ina mpango wa kuivamia Burundi kupitia Congo ambapo anasema Nchi hiyo itakuwa imekosea sana. “Tunajua kwamba Rwanda inajaribu kutushambulia kupitia eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia vuguvugu la Red-Tabara. Lakini tunawaambia kwamba ikiwa wanataka kushambulia Bujumbura kupitia Congo na sisi Kigali hatuko mbali kupitia Kirundo,” alisema Rais Evariste Ndayishimiye Baada ya kauli hiyo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema kuwa, ameshangazwa na kauli ya Rais Evariste Ndayishimiye huku akihoji Rais Ndayishimiye anaeleza kuwa ana taarifa za kuaminika kuwa Rwanda ina mpango wa kushambulia Burundi ?. Msemaji huyo alisema pia endapo hali hiyo ikitokea basi migogoro inaweza kuwa na maafa kwani inaweza kusambaa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kati. Rais Ndayishimiye amemalizia kwa kusema kuwa tayari ameshatuma Wajumbe kadhaa kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame wa kumtaka atekeleze makubaliano ambayo yatazileta pamoja Nchi hizo mbili pamoja lakini hadi leo hii hakuna majibu yoyote yaliyotolewa na bado anayasubiri pia.
    0 Comments 0 Shares 17 Views
  • 0 Comments 0 Shares 1 Views
  • 0 Comments 0 Shares 2 Views
  • 0 Comments 0 Shares 2 Views
  • 0 Comments 0 Shares 2 Views
  • Mchambuzi Farhan JR.

    Nimeona andiko la Waukae @zakazakazi kuhusu TFF kutengeneza Vijana ambalo lilipaswa kuwa jukumu la Klabu na akienda mbali kusema kwamba TFF ndio Shirikisho pekee duniani ambalo lina kituo ambacho kinazalisha na kulea vipaji vya vijana, kwanza kabla ya kupingana nae kuna kitu kwanza nataka kukiweka sawa kwenye eneo hilo.

    Duniani kote Mashirikisho kama TFF yamejikita zaidi kwenye DEVELOPMENT PROJECTS yaani Miradi ya maendeleo kisha wakaachia Mashindano kadhaa yasimamiwe na Bodi zao za Ligi kwa 90% bila kuyaingilia, TFF anachokifanya ni sahihi lakini pia sio sahihi sana kufanya yeye alipaswa kuwa na CLINICS tu ila kuna changamoto sehemu ambayo imeletwa na TFF wenyewe.

    Duniani Klabu zinaweza kuendesha miradi ya Vijana kwasababu kuna kitu kinaitwa FALSAFA ya nchi kwenye mpira, kuanzia mifumo, afya tiba, afya lishe na miundo yote ambayo portifolio hutoka Shirikisho (TFF) Klabu zinaenda kutekeleza mifumo hiyo na kuadjust baadhi ya maeneo halafu Vijana wakienda Clinics za Kitaifa wanaenda kukazia tu.

    Swali linakuja Je Waukaye @zakazakazi FALSAFA ya Tanzania kwenye mpira wa Miguu ni ipi? Iliwasilishwa lini? Anayo nani? Hilo ni Jukumu la TFF ambalo halijatekelezwa, kuna kitu kinaitwa TALENT ID FRAMEWORK ili kupata Vijana je tunayo? Ipoje, anayo nani? Inasemaje? Klabu hazina Mwongozo kutoka kwa TFF? Academy zote nchini zipite humo LAZIMA TFF wafanye wanachoweza, tupo katikati, TFF ASIMAMIE HILO KIKAMILIFU.

    TFF wasiende mbali waende tu hapo Uganda ilipo FUFA, wana Talent ID Framework ambayo Mashirikisho yoote yalipigwa huo Msasa sambamba na Kamati zao tendaji, ndio maana Uganda wapo mbali mno kwenye soka la Vijana kwenye Klabu zao na National Team, kwasababu wana ramani wanaifuata, wameintergrate mfumo wao na FIFA Talent Development Schemes (TDS) je sisi lini tutaforce Klabu zipite humo?

    TFF anajipa majukumu ambayo mengine sio ya kwake, kujadili mikataba ya kibiashara sio Jukumu lake bali Vilabu na Bodi yao, TFF anabaki kama Baba pekee, duniani kote TFF zao zina majukumu yao ukitoa michuano ya FA na Ngao basi Ligi Kuu sio mali yao, TFF ASIMAMIE HASWA JUKUMU LA MAENDELEO NI LAKE.

    Mchambuzi Farhan JR. Nimeona andiko la Waukae @zakazakazi kuhusu TFF kutengeneza Vijana ambalo lilipaswa kuwa jukumu la Klabu na akienda mbali kusema kwamba TFF ndio Shirikisho pekee duniani ambalo lina kituo ambacho kinazalisha na kulea vipaji vya vijana, kwanza kabla ya kupingana nae kuna kitu kwanza nataka kukiweka sawa kwenye eneo hilo. Duniani kote Mashirikisho kama TFF yamejikita zaidi kwenye DEVELOPMENT PROJECTS yaani Miradi ya maendeleo kisha wakaachia Mashindano kadhaa yasimamiwe na Bodi zao za Ligi kwa 90% bila kuyaingilia, TFF anachokifanya ni sahihi lakini pia sio sahihi sana kufanya yeye alipaswa kuwa na CLINICS tu ila kuna changamoto sehemu ambayo imeletwa na TFF wenyewe. Duniani Klabu zinaweza kuendesha miradi ya Vijana kwasababu kuna kitu kinaitwa FALSAFA ya nchi kwenye mpira, kuanzia mifumo, afya tiba, afya lishe na miundo yote ambayo portifolio hutoka Shirikisho (TFF) Klabu zinaenda kutekeleza mifumo hiyo na kuadjust baadhi ya maeneo halafu Vijana wakienda Clinics za Kitaifa wanaenda kukazia tu. Swali linakuja Je Waukaye @zakazakazi FALSAFA ya Tanzania kwenye mpira wa Miguu ni ipi? Iliwasilishwa lini? Anayo nani? Hilo ni Jukumu la TFF ambalo halijatekelezwa, kuna kitu kinaitwa TALENT ID FRAMEWORK ili kupata Vijana je tunayo? Ipoje, anayo nani? Inasemaje? Klabu hazina Mwongozo kutoka kwa TFF? Academy zote nchini zipite humo LAZIMA TFF wafanye wanachoweza, tupo katikati, TFF ASIMAMIE HILO KIKAMILIFU. TFF wasiende mbali waende tu hapo Uganda ilipo FUFA, wana Talent ID Framework ambayo Mashirikisho yoote yalipigwa huo Msasa sambamba na Kamati zao tendaji, ndio maana Uganda wapo mbali mno kwenye soka la Vijana kwenye Klabu zao na National Team, kwasababu wana ramani wanaifuata, wameintergrate mfumo wao na FIFA Talent Development Schemes (TDS) je sisi lini tutaforce Klabu zipite humo? TFF anajipa majukumu ambayo mengine sio ya kwake, kujadili mikataba ya kibiashara sio Jukumu lake bali Vilabu na Bodi yao, TFF anabaki kama Baba pekee, duniani kote TFF zao zina majukumu yao ukitoa michuano ya FA na Ngao basi Ligi Kuu sio mali yao, TFF ASIMAMIE HASWA JUKUMU LA MAENDELEO NI LAKE.
    0 Comments 0 Shares 10 Views
  • "Pengine ulitegemea baada ya kutumikia kifungo cha 'kikatili’ dhidi yangu na kilichojaa Uonevu usiomithilika,labda tukikutana ntaleta nongwa ya Kizaramo? Hapana laa hasha!! Sipo hivyo na nilishasamehe.

    Ila haiondoi ukweli pamoja na ‘ cheko hili tukikutana’ inabidi akubali kuwajibika yeye na wenzie.
    Tutacheka lakini tutaendelea kushinikiza aombe radhi na apumzike uongozi kwa sasa.

    #KariaMustGo" - Haji Manara baada ya kukutana na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Nchini Tanzania (TFF).

    "Pengine ulitegemea baada ya kutumikia kifungo cha 'kikatili’ dhidi yangu na kilichojaa Uonevu usiomithilika,labda tukikutana ntaleta nongwa ya Kizaramo? Hapana laa hasha!! Sipo hivyo na nilishasamehe. Ila haiondoi ukweli pamoja na ‘ cheko hili tukikutana’ inabidi akubali kuwajibika yeye na wenzie. Tutacheka lakini tutaendelea kushinikiza aombe radhi na apumzike uongozi kwa sasa. #KariaMustGo" - Haji Manara baada ya kukutana na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Nchini Tanzania (TFF).
    0 Comments 0 Shares 8 Views
  • Rais wa Nchi Burkina Faso , Kapteni IbrahimTraoré (37) amekataa ongezeko lolote kwenye mshahara wake anaoupata kama kapteni, akisisitiza kuwa anajitolea kwa ajili ya Wananchi wa Nchi hiyo.

    Rais huyo kijana zaidi Duniani, ambaye alichukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi, alitangaza kuwa makadirio ya utajiri wake wote ni Shilingi milioni 340 za Kitanzania na ataendelea kupokea mshahara wake uleule wa kawaida kama kapteni wa Jeshi.

    Uamuzi huo wa kukataa ongezeko la mshahara ni tofauti kubwa na hatua za baadhi ya watangulizi wake, ambapo anaonyesha taswira ya Uongozi mpya kabisa katika Nchi ya Burkina Faso.

    Rais wa Nchi Burkina Faso 馃嚙馃嚝, Kapteni IbrahimTraoré (37) amekataa ongezeko lolote kwenye mshahara wake anaoupata kama kapteni, akisisitiza kuwa anajitolea kwa ajili ya Wananchi wa Nchi hiyo. Rais huyo kijana zaidi Duniani, ambaye alichukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi, alitangaza kuwa makadirio ya utajiri wake wote ni Shilingi milioni 340 za Kitanzania na ataendelea kupokea mshahara wake uleule wa kawaida kama kapteni wa Jeshi. Uamuzi huo wa kukataa ongezeko la mshahara ni tofauti kubwa na hatua za baadhi ya watangulizi wake, ambapo anaonyesha taswira ya Uongozi mpya kabisa katika Nchi ya Burkina Faso.
    0 Comments 0 Shares 10 Views
  • Nchi ya China imeanzisha utafiti wa Wataalam kuwa na uwezo kutambua (kubaini) ugonjwa wa Mtu kupitia mshuzi wake ambapo wataandaliwa Watu maalum ambao watapewa mafunzo kisa kupewa kibali baada ya mafunzo hayo ili kuonyesha kuwa wao ni "Professional Fart Smeller" na watakuwa na kazi maalum ya kubaini ugonjwa wa Mtu kupitia mshuzi wake.

    Nchi ya China 馃嚚馃嚦 imeanzisha utafiti wa Wataalam kuwa na uwezo kutambua (kubaini) ugonjwa wa Mtu kupitia mshuzi wake ambapo wataandaliwa Watu maalum ambao watapewa mafunzo kisa kupewa kibali baada ya mafunzo hayo ili kuonyesha kuwa wao ni "Professional Fart Smeller" na watakuwa na kazi maalum ya kubaini ugonjwa wa Mtu kupitia mshuzi wake.
    0 Comments 0 Shares 6 Views
  • Balozi wa Afrika Kusini Nchini Marekani , Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini.

    Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia.

    Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa.

    "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool.

    Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.

    Balozi wa Afrika Kusini 馃嚳馃嚘 Nchini Marekani 馃嚭馃嚫, Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini. Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia. Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa. "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool. Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 10 Views