0 Commentarios
·0 Acciones
·115 Views
-
“Sisi tumeitwa na serikali tumekuja kusikiliza ila msimamo wa Klabu upo wazi na unafahamika ila hapa tumekuja kusikiliza na tutayabeba yale ambayo tuna uwezo nayo ambayo hatuna uwezo nayo tutayaacha, ilipofikia sio suala la maslahi ya mpira wa Tanzania bali maslahi ya Klabu yetu kwanza” - Alex Ngai, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga SC.
“Sisi tumeitwa na serikali tumekuja kusikiliza ila msimamo wa Klabu upo wazi na unafahamika ila hapa tumekuja kusikiliza na tutayabeba yale ambayo tuna uwezo nayo ambayo hatuna uwezo nayo tutayaacha, ilipofikia sio suala la maslahi ya mpira wa Tanzania bali maslahi ya Klabu yetu kwanza” - Alex Ngai, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga SC.0 Commentarios ·0 Acciones ·794 Views -
-
Nchi za Niger , Burkina Faso na Mali zimetangaza rasmi kujiondoa katika Shirika la Kimataifa la Mataifa yanayozungumza Kifaransa la ‘Francophonie’ (OIF). Uamuzi huo umefanywa na Viongozi wa mataifa hayo yenye Serikali za kijeshi, Niger inaongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani, Mali inaongozwa na Kanali Assimi Goïta na Burkina Faso inayoongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré.
Viongozi hao wamedai OIF na taasisi zingine zilizo chini ya Ufaransa ni ukoloni mamboleo. OIF ni Shirila lililoundwa kwa madhumuni ya kukuza lugha ya Kifaransa na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zinazozungumza Kifaransa.
Gazeti la Le Monde la Nchini Ufaransa limeripoti kuwa taarifa ya pamoja ya Nchi hizo tatu ilisema kwamba OIF imegeuka kuwa ‘chombo cha kisiasa’ kinachoendeshwa na Ufaransa ili kuongeza unyonyaji wa rasilimali za mataifa hayo.
Nchi za Niger 🇳🇪, Burkina Faso 🇧🇫 na Mali 🇲🇱 zimetangaza rasmi kujiondoa katika Shirika la Kimataifa la Mataifa yanayozungumza Kifaransa la ‘Francophonie’ (OIF). Uamuzi huo umefanywa na Viongozi wa mataifa hayo yenye Serikali za kijeshi, Niger inaongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani, Mali inaongozwa na Kanali Assimi Goïta na Burkina Faso inayoongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré. Viongozi hao wamedai OIF na taasisi zingine zilizo chini ya Ufaransa 🇫🇷 ni ukoloni mamboleo. OIF ni Shirila lililoundwa kwa madhumuni ya kukuza lugha ya Kifaransa na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zinazozungumza Kifaransa. Gazeti la Le Monde la Nchini Ufaransa limeripoti kuwa taarifa ya pamoja ya Nchi hizo tatu ilisema kwamba OIF imegeuka kuwa ‘chombo cha kisiasa’ kinachoendeshwa na Ufaransa ili kuongeza unyonyaji wa rasilimali za mataifa hayo. -
Rais wa Nchi ya Ukraine , Volodymyr Zelensky, ametabiri kuea Rais wa Urusi , Vladimir Putin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kuwa afya ya Kiongozi huyo wa Urusi inazorota. Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Waandishi wa habari Jijini Paris, Ufaransa baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusema kuwa "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika."
Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kuwa huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume.
Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na Daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Sanjari na hayo, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.
Rais wa Nchi ya Ukraine 🇺🇦, Volodymyr Zelensky, ametabiri kuea Rais wa Urusi 🇷🇺, Vladimir Putin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kuwa afya ya Kiongozi huyo wa Urusi inazorota. Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Waandishi wa habari Jijini Paris, Ufaransa 🇫🇷 baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusema kuwa "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika." Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kuwa huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume. Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na Daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani 🇺🇸 ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Sanjari na hayo, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.0 Commentarios ·0 Acciones ·1K Views -
Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limetangaza zawadi zitakazotolewa kwa Washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu (FIFA CLUB WORLD CUP), ambapo bingwa wa michuano hiyo atapata dola milioni 125 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 300 za kitanzania huku kukitarajiwa kutolewa jumla ya dola bilioni 1 kwa klabu 32 zitakavyoshiriki na dola milioni 250 zitatolewa kwa mashirikisho kwa ajili kukuza mpira wa miguu kwa ngazi ya klabu Duniani.
Shirikisho hilo limepanga kutoa dola milioni 250 ili kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu kwa kiwango cha kimataifa ambapo fedha hizi zitatumika kusaidia klabu ndogo, kuboresha miundombinu, kuwekeza katika mafunzo ya Wachezaji na Makocha pamoja na kuimarisha ushirikiano wa klabu kimataifa.
Aidha, pango huu unalenga kuhakikisha kuwa maendeleo ya mpira wa miguu hayaishii kwa klabu kubwa pekee, bali pia yanawanufaisha hadi klabu dogo na kuinua mpira wa Duniani kote. FIFA pia imesisitiza kuwa, mapato yote ya mashindano haya yatasambazwa kwa klabu bila kugusa akiba yake, ambayo inatumiwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu kupitia Vyama (211) Wanachama wa FIFA.
Mfumo huu ni mkubwa zaidi katika historia ya mpira wa miguu, ukiwa na mechi saba (7) kwenye hatua ya makundi na mfumo wa mchujo.
Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limetangaza zawadi zitakazotolewa kwa Washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu (FIFA CLUB WORLD CUP), ambapo bingwa wa michuano hiyo atapata dola milioni 125 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 300 za kitanzania huku kukitarajiwa kutolewa jumla ya dola bilioni 1 kwa klabu 32 zitakavyoshiriki na dola milioni 250 zitatolewa kwa mashirikisho kwa ajili kukuza mpira wa miguu kwa ngazi ya klabu Duniani. Shirikisho hilo limepanga kutoa dola milioni 250 ili kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu kwa kiwango cha kimataifa ambapo fedha hizi zitatumika kusaidia klabu ndogo, kuboresha miundombinu, kuwekeza katika mafunzo ya Wachezaji na Makocha pamoja na kuimarisha ushirikiano wa klabu kimataifa. Aidha, pango huu unalenga kuhakikisha kuwa maendeleo ya mpira wa miguu hayaishii kwa klabu kubwa pekee, bali pia yanawanufaisha hadi klabu dogo na kuinua mpira wa Duniani kote. FIFA pia imesisitiza kuwa, mapato yote ya mashindano haya yatasambazwa kwa klabu bila kugusa akiba yake, ambayo inatumiwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu kupitia Vyama (211) Wanachama wa FIFA. Mfumo huu ni mkubwa zaidi katika historia ya mpira wa miguu, ukiwa na mechi saba (7) kwenye hatua ya makundi na mfumo wa mchujo.0 Commentarios ·0 Acciones ·907 Views -
The ground we walk on today, will be our roof tomorrowThe ground we walk on today, will be our roof tomorrow ‼️
-
-
-