Massamba Intore na Kidum watangaza mpango wa albamu ya pamoja.
Msanii Mkongwe wa muziki wa jadi nchini Rwanda, Massamba Intore, ametangaza rasmi kuwa yuko katika maandalizi ya kutengeneza albamu ya pamoja na Msanii maarufu wa Afrika Mashariki kutoka Nchini Burundi, Kidum.
Kwa mujibu wa maelezo yao, mpango huo hautakuwa tu mkusanyiko wa nyimbo, bali ni uthibitisho wa urafiki wao wa muda mrefu na ushirikiano wa kisanii uliokua kwa miaka kadhaa. Wawili hao wanatarajia kuunganisha uzoefu wao mkubwa katika muziki wa maonyesho ya moja kwa moja (Live), ambao umekuwa alama ya mafanikio yao jukwaani.
Ikumbukwe kwamba Masamba na Kidum alishafanya wimbo wa pamoja uitwao "Wapi ye" zaidi ya 15 iliyopita na ulifanya vizuri kipindi hicho.
Massamba alitoa taarifa hiyo usiku wa Ijumaa, tarehe 13 Februari 2026, alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa albamu “Inganzo Ntahangarwa” ya Msanii Yvan Muziki.
Akiwa jukwaani pamoja na Kidum, Massamba hakuweza kuficha hisia zake. Alisisitiza kuwa anamshukuru sana Kidum kwa mchango wake mkubwa katika safari yake ya muziki.
Massamba alisema: “Namshukuru sana Kidum kwa mchango wake katika safari yangu ya muziki. Amenisaidia kupata ujasiri wa kupeleka kazi zangu studio na kuziwasilisha katika viwango vya kimataifa.”
Kauli hiyo ilishangiliwa na mashabiki waliokuwa ukumbini, wakionesha matumaini makubwa juu ya albamu hiyo inayotarajiwa kuleta ladha ya kipekee kwa Wapenzi wa muziki wa zamani na wa kisasa.
Kwa kuzingatia historia yao ndefu jukwaani, Wachambuzi wa muziki wanaamini kuwa albamu hiyo itakuwa daraja la kuunganisha mitindo tofauti ya muziki wa jadi wa Rwanda na ladha ya kimataifa inayobebwa na Kidum.
Mpango huu unatarajiwa kuimarisha zaidi ushirikiano wa Wasanii wa kanda ya Afrika Mashariki, huku ukitoa ujumbe wa mshikamano na urafiki kupitia sanaa.
Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu kutangazwa kwa tarehe rasmi ya uzinduzi wa albamu hiyo, ambayo tayari imeanza kuvutia mjadala mpana katika mitandao ya kijamii hasa Nchini Rwanda.
Toa maoni yako
#Habari

0 Yorumlar
0 hisse senetleri
16 Views