Upgrade to Pro

Nimewahi onekana msumbufu kwake, wiki moja baada ya kuniambia ahsante kwa kunijali.

Nilikuwa mstari wa mbele kwenye matatizo yake yanayohusu pesa, bila kujali umaskini wangu.

Nilimpenda sana yule mwanamke, aliyewahi niomba nisichoweza kukimudu, ili anikasirikie.

Kwangu haikuwa blue ticks zisizojibiwa, wala block, alikosa kabisa, muda wa kufungua jumbe nilizomtumia, licha ya kuwa online muda wote.

Kuna siku aliniahidi kuja, halafu akanizimia simu, dakika chache baada ya kumtumia nauli.

Hadi nikaitwa kitenzi king'ang'anizi, zilipokuja dalili za wazi, kuwa sitakiwi na yeye.

Aliyesema mapenzi upofu, ni kama alitaka nisione nafasi yangu kwenye dharau zake.

Corabo ya dunia isiyonihitaji, na shetani aliyefanikiwa, ikaniaminisha nipo sahihi, ili nizidi kupotea.

Huzuni ikawa kurasa ya kwanza, kwenye daftari lililoandikwa ninavyostahili.

Kabla yakuwa single, ilikuwa ngumu kuamini kama naweza kuishi bila yeye.

Baada ya kuvipa onyo viungo vyangu vya uzazi, siku hizi upweke umekuwa rafiki anayeongozana na mimi kila mahali, nainjoi.

Mwambieni nimemsamehe Farashuu, maana nikisema nilipize hastahili kuishi, ila msimtaje mbele yangu.

N.B, Hii Haina uhusiano wowote na mwandishi

#neliudcosiah
Nimewahi onekana msumbufu kwake, wiki moja baada ya kuniambia ahsante kwa kunijali. Nilikuwa mstari wa mbele kwenye matatizo yake yanayohusu pesa, bila kujali umaskini wangu. Nilimpenda sana yule mwanamke, aliyewahi niomba nisichoweza kukimudu, ili anikasirikie. Kwangu haikuwa blue ticks zisizojibiwa, wala block, alikosa kabisa, muda wa kufungua jumbe nilizomtumia, licha ya kuwa online muda wote. Kuna siku aliniahidi kuja, halafu akanizimia simu, dakika chache baada ya kumtumia nauli. Hadi nikaitwa kitenzi king'ang'anizi, zilipokuja dalili za wazi, kuwa sitakiwi na yeye. Aliyesema mapenzi upofu, ni kama alitaka nisione nafasi yangu kwenye dharau zake. Corabo ya dunia isiyonihitaji, na shetani aliyefanikiwa, ikaniaminisha nipo sahihi, ili nizidi kupotea. Huzuni ikawa kurasa ya kwanza, kwenye daftari lililoandikwa ninavyostahili. Kabla yakuwa single, ilikuwa ngumu kuamini kama naweza kuishi bila yeye. Baada ya kuvipa onyo viungo vyangu vya uzazi, siku hizi upweke umekuwa rafiki anayeongozana na mimi kila mahali, nainjoi. Mwambieni nimemsamehe Farashuu, maana nikisema nilipize hastahili kuishi, ila msimtaje mbele yangu. N.B, Hii Haina uhusiano wowote na mwandishi 😀😀🙌🙌 #neliudcosiah
Like
2
1 Comments ·76 Views