KAULI YA JESHI LA POLISI VURUGU BAADA YA MECHI KATI YA SIMBA SC NA CS SFAXIEN
Leo Desemba 15, 2024 majira ya saa 11. 50 jioni katika Uwanja wa Benjamin William Mkapa Temeke Dar es salaam kwenye mchezo wa mpira wa miguu wa kimataifa wa kombe la Shirikisho Afrika kati ya timu ya Simba ya Tanzania na CS SFAXIEN ya Tunisia kulitokea fujo iliyosababishwa na mashabiki wa Timu ya CS SFAXIEN kutoridhika na maamuzi ya refa wa mchezo huo kuchezesha mechi hiyo kwa zaidi ya dakika saba ambazo aliziongeza kama dakika za nyongeza jambo lililo pelekea timu ya Simba kupata goli la pili na la ushindi.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro, Wachezaji wa ndani ya uwanja na "benchi" la ufundi la timu ya CS SFAXIEN walikasirika, wakamfuata mwamuzi wa mchezo na kuanza kufanya vitendo vya kumshambulia.
Katika fujo hizo shabiki mmoja wa timu ya CS SFAXIEN aliumia na kupatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa, huku viti vya rangi ya blue 156 na Orange 100 viling’olewa na mashabiki hao.
"Jeshi la Polisi litashirikiana na mamlaka zingine za kisheria na soka kuona hatua za kuchukua dhidi ya vitendo hivyo ambavyo havikubaliki" Taarifa hiyo imeeleza.
#neliudcosiah