Matendo ya Mitume 20:29-32
[29]Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kuangusha mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;

[30]tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.
.
[31]Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi.

[32]Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa.

Ukitizama vizuri utagundua Paulo alipo taka kurudi Yerusalemu kwa ajiri ya pentecost alilipitia kanisa na kuliaga .

Alipo kuwa akiwaaga alisikia hakika ya kuwa hatorudi ikabidi aliachie kanisa mausia au maagizo .

Na moja ya maagizo ni kuwa ili kanisa lizidi kukua katika roho na kuishi maisha ya Kristo lazima wakeshe wakiomba .

Si tu kukesha katika kuomba bali wakeshe pia wakikumbuka kuwa ndani ya MAOMBI lazima pia wawe watu sakuonyana na kuchukuliana kwa ajiri ya mwili wa Kristo.

Na pia kanisa lisiyakubali mfundisho ya wanikolai maana uamsho ukipoa watakuja watu na mafundisho ya kila aina ambayo kwa sehemu kubwa ni kulipotezq kanisa.

.Matendo ya Mitume 20:28
[28]Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

Kumbe maombi ni kitu muhimu sana kwa huduma kwani hata muasisu wa huduma akitoka bado huduma haitateteleka.


Kanisa la kwanza lilikuwa imara kwa sababu Yesu alipo ondoka kanisa aliliachia maagizo wakae wakisubiri roho ,na si kuwa walikuwa wakila na kunywa hapana bali walikuwa wakiomba mchana na usiku na ndio mana walifanya ishara na maajabu mengi na uamsho mkubwa sana.

Ili Mungu alionekanie kanisa lazima liwe hai katika maombi na wala si kitu kingine chochote.

Kanisa la maombi mengi ndilo kanisa la wapindua meza .

Mungu alisaidie kanisa la uamsho la Tanzania kwani ni muda wa kanisa kukesha kuomba umefika .

Yesu mwenyewe pia alisema kesheni mkiomba maana hamjui saa ya mwana wa adamu kurejea.
.

Ok naitwa sylvester mwakabende Kutoka (build new eden)

#build new eden
#restore men position
Matendo ya Mitume 20:29-32 [29]Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kuangusha mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; [30]tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. . [31]Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi. [32]Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa. Ukitizama vizuri utagundua Paulo alipo taka kurudi Yerusalemu kwa ajiri ya pentecost alilipitia kanisa na kuliaga . Alipo kuwa akiwaaga alisikia hakika ya kuwa hatorudi ikabidi aliachie kanisa mausia au maagizo . Na moja ya maagizo ni kuwa ili kanisa lizidi kukua katika roho na kuishi maisha ya Kristo lazima wakeshe wakiomba . Si tu kukesha katika kuomba bali wakeshe pia wakikumbuka kuwa ndani ya MAOMBI lazima pia wawe watu sakuonyana na kuchukuliana kwa ajiri ya mwili wa Kristo. Na pia kanisa lisiyakubali mfundisho ya wanikolai maana uamsho ukipoa watakuja watu na mafundisho ya kila aina ambayo kwa sehemu kubwa ni kulipotezq kanisa. .Matendo ya Mitume 20:28 [28]Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Kumbe maombi ni kitu muhimu sana kwa huduma kwani hata muasisu wa huduma akitoka bado huduma haitateteleka. Kanisa la kwanza lilikuwa imara kwa sababu Yesu alipo ondoka kanisa aliliachia maagizo wakae wakisubiri roho ,na si kuwa walikuwa wakila na kunywa hapana bali walikuwa wakiomba mchana na usiku na ndio mana walifanya ishara na maajabu mengi na uamsho mkubwa sana. Ili Mungu alionekanie kanisa lazima liwe hai katika maombi na wala si kitu kingine chochote. Kanisa la maombi mengi ndilo kanisa la wapindua meza . Mungu alisaidie kanisa la uamsho la Tanzania kwani ni muda wa kanisa kukesha kuomba umefika . Yesu mwenyewe pia alisema kesheni mkiomba maana hamjui saa ya mwana wa adamu kurejea. . Ok naitwa sylvester mwakabende Kutoka (build new eden) #build new eden #restore men position
0 Commentarii ·0 Distribuiri ·119 Views