Meneja wa Paris Saint Germain, Luis Enrique ameweka wazi kuwa Uongozi wa klabu hiyo unamuunga mkono kwenye uamuzi wake wa kuachana na Golikipa Gianluigi Donnarumma kutokuwa sehemu ya kikosi cha Timu hiyo hivyo ataanza kwa kuukosa mchezo wa UEFA Super Cup.

Kipa huyo raia wa Italia aliachwa nje ya kikosi kilichosafiri hadi Udine kwa mechi ya kirafiki leo dhidi ya Tottenham, huku Magolikipa Lucas Chevalier na Renato Marin wakichaguliwa badala yake.

Katika chapisho lake kwenye mtandao wake wa Instagram, Donnarumma alisema "amesikitishwa na kuvunjika moyo" kwa kukosekana kwake.
Nyota huyo alikuwa mmoja wa wachezaji wa PSG walioshinda taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na uamuzi huo umekuja kwa mshtuko kutokana na hadhi yake na wasifu wake.

Enrique alisema uamuzi wake ulikuwa na lengo la kutafuta Golikipa mwenye "wasifu tofauti" na Gigi.

"Uongozi unaniunga mkono na tunajaribu kutafuta suluhu bora," aliongea kwenye mkutano wa wanahabari Jumanne.

"Ni uamuzi mgumu, namkubali Donnarumma kwani ni mmoja wa makipa bora na mtu bora zaidi. Lakini tulikuwa tunatafuta wasifu tofauti, na ni vigumu sana kuchukua maamuzi ya aina hii." - alimaliza kwa kusema hivyo.

#SportsElite
🚨🚨Meneja wa Paris Saint Germain, Luis Enrique ameweka wazi kuwa Uongozi wa klabu hiyo unamuunga mkono kwenye uamuzi wake wa kuachana na Golikipa Gianluigi Donnarumma kutokuwa sehemu ya kikosi cha Timu hiyo hivyo ataanza kwa kuukosa mchezo wa UEFA Super Cup. Kipa huyo raia wa Italia aliachwa nje ya kikosi kilichosafiri hadi Udine kwa mechi ya kirafiki leo dhidi ya Tottenham, huku Magolikipa Lucas Chevalier na Renato Marin wakichaguliwa badala yake. Katika chapisho lake kwenye mtandao wake wa Instagram, Donnarumma alisema "amesikitishwa na kuvunjika moyo" kwa kukosekana kwake. Nyota huyo alikuwa mmoja wa wachezaji wa PSG walioshinda taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na uamuzi huo umekuja kwa mshtuko kutokana na hadhi yake na wasifu wake. Enrique alisema uamuzi wake ulikuwa na lengo la kutafuta Golikipa mwenye "wasifu tofauti" na Gigi. "Uongozi unaniunga mkono na tunajaribu kutafuta suluhu bora," aliongea kwenye mkutano wa wanahabari Jumanne. "Ni uamuzi mgumu, namkubali Donnarumma kwani ni mmoja wa makipa bora na mtu bora zaidi. Lakini tulikuwa tunatafuta wasifu tofauti, na ni vigumu sana kuchukua maamuzi ya aina hii." - alimaliza kwa kusema hivyo. #SportsElite
0 Commentarii ·0 Distribuiri ·3 Views