Real Madrid wametoa taarifa ya KUKATAA VIKALI wazo la kuchezwa kwa mechi ya La Liga kati ya Villarreal na Barcelona huko Miami

Wazo hilo lilitekelezwa bila kushauriana awali na vilabu vinavyoshiriki La Liga, jambo linalokiuka kanuni muhimu ya "mshikamano wa maeneo" inayosimamia mfumo wa ligi wa mechi za nyumbani na ugenini.

Mabadiliko ya aina hii yanapaswa kuwa na idhini ya wazi na ya pamoja kutoka kwa vilabu vyote vinavyoshiriki, pamoja na kutimiza kikamilifu masharti ya kitaifa na kimataifa yanayosimamia uendeshaji wa mashindano rasmi.

Katika kutetea kanuni hii, Real Madrid imechukua hatua tatu mahsusi:

1. Kuwasilisha ombi kwa FIFA kuzuia mechi hiyo kuchezwa bila idhini ya awali kutoka kwa vilabu vyote vya La Liga.

2. Kuwasilisha ombi kwa UEFA kuomba RFEF iondoe au ikatae ombi hilo, ikisisitiza vigezo vilivyowekwa mwaka 2018 vinavyokataza kuchezwa kwa mechi rasmi za mashindano ya ndani nje ya ardhi ya taifa, isipokuwa kwa hali za kipekee na zilizo na sababu za msingi ambazo katika kesi hii hazikutimia.

3. Kuwasilisha ombi kwa Baraza Kuu la Michezo(Consejo Superior de Deportes) kuto kutoa vibali vya kiutawala vinavyohitajika bila kuwepo kwa idhini ya pamoja kutoka kwa vilabu vyote.

#SportsElite
❌⛔🇪🇸Real Madrid wametoa taarifa ya KUKATAA VIKALI wazo la kuchezwa kwa mechi ya La Liga kati ya Villarreal na Barcelona huko Miami Wazo hilo lilitekelezwa bila kushauriana awali na vilabu vinavyoshiriki La Liga, jambo linalokiuka kanuni muhimu ya "mshikamano wa maeneo" inayosimamia mfumo wa ligi wa mechi za nyumbani na ugenini. Mabadiliko ya aina hii yanapaswa kuwa na idhini ya wazi na ya pamoja kutoka kwa vilabu vyote vinavyoshiriki, pamoja na kutimiza kikamilifu masharti ya kitaifa na kimataifa yanayosimamia uendeshaji wa mashindano rasmi. Katika kutetea kanuni hii, Real Madrid imechukua hatua tatu mahsusi: 1. Kuwasilisha ombi kwa FIFA kuzuia mechi hiyo kuchezwa bila idhini ya awali kutoka kwa vilabu vyote vya La Liga. 2. Kuwasilisha ombi kwa UEFA kuomba RFEF iondoe au ikatae ombi hilo, ikisisitiza vigezo vilivyowekwa mwaka 2018 vinavyokataza kuchezwa kwa mechi rasmi za mashindano ya ndani nje ya ardhi ya taifa, isipokuwa kwa hali za kipekee na zilizo na sababu za msingi ambazo katika kesi hii hazikutimia. 3. Kuwasilisha ombi kwa Baraza Kuu la Michezo(Consejo Superior de Deportes) kuto kutoa vibali vya kiutawala vinavyohitajika bila kuwepo kwa idhini ya pamoja kutoka kwa vilabu vyote. #SportsElite
0 Commentaires ·0 Parts ·24 Vue