Manchester United Yavunja Rekodi ya Mapato ya £666.5m, Licha ya Kukosa Ligi ya Mabingwa Ulaya
Manchester United imetangaza mapato ya rekodi ya £666.5 milioni kwa mwaka wa fedha 2025, licha ya kutoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (#UCL). Hata hivyo, klabu hiyo imerekodi hasara ya uendeshaji ya £18.4 milioni, ikilinganishwa na hasara kubwa zaidi ya £69.3 milioni mwaka 2024.
Kiasi cha £36.6 milioni kilitumiwa kama gharama maalum, ikiwemo kuondoka kwa aliyekuwa meneja Erik ten Hag pamoja na benchi lake la ufundi.
United pia imeweka historia kwa kupata mapato ya juu zaidi ya siku za mechi, yaliyoongezeka kwa 17%, kutokana na mauzo makubwa ya tiketi na uanachama. Aidha, klabu ilipata mapato ya juu zaidi ya kibiashara, yaliyoongezeka kwa 10%, kutokana na ushirikiano mpya wa jezi kuu na kampuni ya teknolojia Snapdragon.
Kwa mwaka wa fedha 2026, klabu hiyo imeweka makadirio ya mapato kati ya £640 milioni na £660 milioni, huku EBITDA iliyorekebishwa ikitarajiwa kuwa kati ya £180 milioni na £200 milioni.
Afisa Mtendaji Mkuu, Omar Berrada, alisema kuwa klabu inaendelea na mikakati ya muda mrefu ndani na nje ya uwanja:
> "Tunafurahishwa na wachezaji wapya tulioongeza kwenye vikosi vyetu vya wanaume na wanawake. Nje ya uwanja, tunapitia mabadiliko ya kiuongozi na kimuundo, na sasa tuna taasisi iliyo tayari kufanikisha malengo yetu. Kupunguza gharama kutatupa nafasi kubwa ya kuboresha matokeo ya kifedha, jambo litakalosaidia kipaumbele chetu kikuu — mafaanikio uwanjani."
Manchester United sasa ina matumaini kwamba mafanikio ya kifedha yatasaidia kurejesha ubingwa na heshima uwanjani.
#SportsElite

⚽ Manchester United Yavunja Rekodi ya Mapato ya £666.5m, Licha ya Kukosa Ligi ya Mabingwa Ulaya

📌 Manchester United sasa ina matumaini kwamba mafanikio ya kifedha yatasaidia kurejesha ubingwa na heshima uwanjani.
#SportsElite