Nyota wa Soka Kaslin Soza atangaza kusilimu
Mchezaji wa soka kutoka Brazil, Kaslin Soza, ametangaza rasmi kuwa amesilimu na kuanza maisha mapya ya imani ya Kiislamu.
Kaslin, ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Wanawake ya Real Madrid Femenino nchini Hispania na kwa sasa anakipiga katika klabu ya Saudia ya Al-Nassr Women, alitoa taarifa hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Katika ujumbe wake, Kaslin aliandika kwa hisia na msisitizo akisema: “Nimechagua kuingia katika dini ya Uislamu kwa hiari yangu mwenyewe, nikiwa na amani moyoni na imani thabiti juu ya uamuzi huu.”
Nyota huyo wa kandanda alieleza kuwa safari yake ya kiroho haikuwa ya ghafla, bali ni matokeo ya tafakari ya muda mrefu na kujifunza kwa kina kuhusu mafundisho ya dini hiyo.
“Huu ni mwanzo wa ukurasa mpya katika maisha yangu, safari ya kujitambua zaidi na kumkaribia Mwenyezi Mungu,” aliongeza katika ujumbe wake.
Hatua hiyo imeibua mjadala mpana mtandaoni, huku mashabiki wake na wadau wa soka wakitoa pongezi na salamu za heri kwa uamuzi wake. Wapo waliomsifu kwa ujasiri wa kusimama hadharani na kutangaza mabadiliko hayo ya kiimani.
Kaslin Soza amekuwa miongoni mwa Wachezaji wa Brazil waliopata nafasi ya kucheza katika Ligi kubwa barani Ulaya kabla ya kuhamia Mashariki ya Kati, ambako soka la Wanawake linaendelea kukua kwa kasi.
Kwa sasa, macho ya mashabiki wake yapo si tu kwenye kiwango chake Uwanjani, bali pia katika safari yake mpya ya maisha nje ya Uwanja.
Toa maoni yako
#Sports
#Habari

🇧🇷 Nyota wa Soka Kaslin Soza atangaza kusilimu

0 Yorumlar
0 hisse senetleri
36 Views